Godbless Lema: Makamu wa Rais si Mungu, ukiumwa sema, ukisafiri kikazi sema

Godbless Lema: Makamu wa Rais si Mungu, ukiumwa sema, ukisafiri kikazi sema

Inakuwaje serikali nzima kule juu wasione vitu vidogo kama hivi. Hivi tunaongozwa na watu wazima vichwani kweli?
 
Kila aliyetukana ataenda kutubu, hata kubwa jinga Lisu aliomba kwenda akakataliwa.
 
Tatizo huyu Lema na wenzake wenye pigo kama zake wote ni wapuuzi, sababu Kairuki kwenye mkutano aliomwakilisha alisema Makamu yupo nje kikazi, sasa ni taarifa gani mnayotaka zaidi??

Lakini kwa jinsi walivyo mapunguani, wakadai hiyo ni danganya toto jamaa kashakata moto tuambiwe mapema, na yule kigogo akaropoka amemalizwa kwa sumu sijui na hila nyinginezo

Haya karudi mzima wote wamepoteana, punguzeni unaa
Kusema uongo ni dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti.
 
Makamu wa Rais nakusalimu. Wewe sio makamu wa Rais wa familia yako.Wewe ni Makamu wa Rais wa Nchi.Watu wanapofuatilia taarifa zako wako sawa asilimia 100. Ukuonekana kwa muda mrefu na serikali na ofisi yako wakawa kimya,watu wakaanza huko wapi? Tena ni jambo jema kwako,nilifikiri ungefurahi badala yake nimekuona tofauti.

Wewe sio Mungu ukiumwa sema, ukisafiri kikazi sema.Cheo chako sio utakatifu. Wewe ni mfanyakazi wetu,uwe unatoa taarifa ya mienendo ya kazi zetu. Sasa umewashukuru waliokuwa wanakuombea, je,walikuwa wanakuombea kitu gani ?uwe na amani na afya njema.
Ime wahi tokea wapi duniani makamu wa rais kukaa nje ya nchi mwezi mzima bila wananchi wake kujua?
Hiyo gharama ni nani ana beba?
Hiyo kazi maalum ni kazi gani ambayo wasaidizi waandamizi iliwashinda hadi awe yeye?
By the way yeye yuko pale kisiasa na sio kiutendaji. Ccm waache kuficha ukweli.
 
Tatizo huyu Lema na wenzake wenye pigo kama zake wote ni wapuuzi, sababu Kairuki kwenye mkutano aliomwakilisha alisema Makamu yupo nje kikazi, sasa ni taarifa gani mnayotaka zaidi??

Lakini kwa jinsi walivyo mapunguani, wakadai hiyo ni danganya toto jamaa kashakata moto tuambiwe mapema, na yule kigogo akaropoka amemalizwa kwa sumu sijui na hila nyinginezo

Haya karudi mzima wote wamepoteana, punguzeni unaa
Ni jambo gani lenye maslahi kwa nchi huyo makamu wa rais ameenda kufanya huko nje hadi iwe safari ya Siri? Wakati mwingine mnaendekeza mambo ya kijinga Hadi inakuwa kero. Toka alivyoondoka mngesema, sio kusubiri watu wanaopenda udaku kueneza uvumi, kisha ndio mnatoa majibu ya kuokoteza okoteza.
 
Yeah! Mbona Mzee wa msogaland enzi zake alipoenda kutibiwa mshipa wa ngiri Marekani tulijua?
Hapa umetania mkuu...jamaa si alitujuza baada ya kufika, na ilikuwa ni katika kuzima kelele zile kipindi kile, au umesahau mkuu?
 
Mambo ya watu kupotea bila taarifa na badae wanarudi au kutokurudi yalianzia awamu ya 5

Muasisi naye siku yake ikafika akapotea tangu February 27 akarudi maiti March 17.

RIP Ben Saanane , Azori Gwanda na wengineo wengi.
 
Kwani Lema kaishia darasa la ngapi?
Kuna makosa ya kiuandishi mengi kwenye bandiko lake, makosa ambayo Mimi nisingeyafanya kipindi nilipokuwa kidato cha kwanza au darasa la saba.
Ukuonekana [emoji777]
Hukuonekana [emoji3581].
Huko wapi [emoji777]
Uko wapi [emoji3581].
Kwani hapo kaandika Lema ?
 
Kwani hapo kaandika Lema ?
Soma thread vizuri utaona bandiko la Lema ndilo nililoambatanisha
Screenshot_2023-12-12-20-49-27-480_com.twitter.android-edit.jpg
 
Back
Top Bottom