Godbless Lema: Wanaopigana na mimi wataadhibiwa na Mungu muda siyo mwingi

Mpumbavu kabisa baba wa watu yupo jela muda mrefu unaona msimamo wako haueleweki.Kwanini usijiuzulu kama wengine uende chaumma ukale hizo hela si ni hela unataka?Wenzako waliacha unafki wakaondoka na wewe do the same ondoka.
 
Wanaopigana na mimi wataanza kuadhibiwa muda siyo mwingi maana namjua Mungu ninayemwamini.

Msimamo wa kukataa maridhiano ni wa kamati kuu ya chama na siyo mtu.
Mkuu Lodi Atikini, Asante kwa taarifa hii, nawashauri Chadema wasiipuuzie, Godbless Lema ni mtu mwenye upako, ni kama Nabii fulani, hivyo msimchezee , msimgizie wala msimpuuze! https://www.jamiiforums.com/threads...a-sasa-ni-makonda-itatimia-asipuuzwe.2279680/

Mzee Pasco
 
Kama anasingiziwa kweli Mungu kwenye mambo serious hana masihara! Ila kama Lema anafanya usaliti kwa wenzake na bado anamtaja Mungu kuaminisha watu uongo itakuwa mbaya! Mungu amsaidie maana haya mambo si mepesi.

Hapa naona ni mkanganyiko wa ajabu!!

Mbona Lema ameweka wazi kuwa CHADEMA haitaki maridhiano mpaka baadhi ya mambo yatekelezwe, na ameweka wazi kuwa yeye alikuwa ni miongoni mwa wajumbe walioshiriki kufikia azimio hilo la chama.

Sasa hawa wanaosema Lema anataka maridhiano, hiyo habari wameiokota wapi? Au kutaka kutengeneza mvurugano ndani ya CHADEMA kwa hadithi za kutengenezwa?


Lema ameweka wazi kuwa CHADEMA hakitaki maridhiano mpaka masharti yawe yametimizwa
 
Hiyo kauli ya familia yake "kuja kusalimia mwezi Mmoja kisha kurudi kwao Canada" alikusudia nn kwamba ni wacanada rasmi sasa sio waTz? Siasa mchezo mchafu sana.
 
Inaonekana wewe sio mfuatiliaji mzuri wa habari anazopost Lema mtandaoni. Lema alianza kwa kutamka kuwa hela za tonetone zinapitia kwenye account binafsi za Heche kitu ambacho hata kama ni kweli haikuwa busara kwa wakati uliopo kutoa allegation kama hizo. Pili Lema ameonekana kuwa soft sana kwa utawala huu “kwa sasa” kitu kinachotia mashaka. Lema amepost gazeti lefu kujustfy kwa nini ni busara kwenda kutoa pole Kizimkazi kitu ambacho wachunguzi wa mambo wanahisi kuna kitu kimejificha ndani yake, Lema kaongea blah blah nyingi kuhusu chadema kwenda Kizimkazi kwenda kutoa pole. Of course kutoa pole ni jambo la kiungwana ila kulitamka Lema kwa wakati huu chadema ikiwa inapitia madhila kama haya, ukiunganisha na propaganda anazozushiwa Heche na maccm, mind you Lema pia anatoa maneno yanayomchafua Heche kuhusu tonetone unaweza kuhisi kuna kitu nyuma ya Lema. Pia Lema jana ameandika gazeti kuashiria Lisu anaunga mkono kwenda kutoa pole Kizimkazi hivyo impliedly in suggest Lisu yupo tayari kwa maridhiano na anamuweka Heche kwenye wakati mgumu kuwa Heche ndio hataki maridhiano ila Lisu anayataka. So Lema ni kama anamanipulate public ionekane kuwa Lisu yupo tayari kwa maridhiano ila kikwazo ni Heche. So to conclude wanaosema Lema kafika bei na anapush maridhiano wana hoja based on that circumstantial evidences
 

Huyo Ni dalali na Tapeli km kaka Malienge.
 
ok.🐒
 
Mkuu Lodi Atikini, Asante kwa taarifa hii, nawashauri Chadema wasiipuuzie, Godbless Lema ni mtu mwenye upako, ni kama Nabii fulani, hivyo msimchezee , msimgizie wala msimpuuze!

Mzee Pasco

Nabii wa kwako na familia zenu, wee mzee ndio maana Magufuli alikuchambaa, una njaa sana wewee.
Huna tofauti nae, pindi muonapo hela mnawaka mnoo. Lol
 
Chadema wamekosa utulivu kabisa.
zitto junior
Tatizo ni kukesha mitandaoni, Lema huwezi kuta amepost itikadi, sera au mafanikio ya chadema bali kuwa reactive tu na trend zozote za kisiasa Tanzania.

Inabidi chadema waweke sheria kali kwa viongozi kutumia social media kumwaga taarifa sensitive za chama.

Hii chaos huwezi ikuta hata ACT au CHAUMMA, kuna namna huku chadema kila mtu ni msemaji kuanzia Hilda Newton mpaka Lema as if ndio Katibu Mkuu wa chama.
 
Unajua kusoma na kuelewa kweli?!

Lema ametoka wapi kuelezea tofauti na maazimio ya KK iliyoketi?

Vichwa vyenu vidogo ndio chanzo cha migogoro.
 
Kama Lema anashambuliwa mitandaoni hutaki ajitetetee?

Waambieni wale wanaokesha kumshambulia Lema mitandaoni wamuache tuone kama ataendelea kuhangaika na mitandao.

Mara ngapi before Lema amekuwa akionesha maovu ya serikali kupitia mitandao na hatukuwahi kumuona mbaya?

Hao wanaojidai wapo kimya hawahangaiki na mitandao ndio wanaowatuma hao kina Hilda kuendelea kumshambukia Lema, huu utoto wao umeshajulikana.

Msilee tatizo, Lema ana haki ya kujitetea akiendelea kushambuliwa, namuunga mkono.
 
Heche ma Prado na masemi ya mizigo amenunua kwa hela ya nani?

Sea cliff ipo kwa ajili ya wakina nani? Yeye hawezi kulala?
 
Unajua kusoma na kuelewa kweli?!

Lena ametoka wapi kuelezea tofauti na maazimio ya KK iliyoketi?

Vichwa vyenu vidogo ndio chanzo cha migogoro.

Kuna posti amegusia maamuzi ya kamati kuu waliyoketi ku justify, alichokifanya. Vichwa kweli ni vidogo, lakini tuna pua kubwa kunusa harufu ya hili la Lema. Hatutakaa kimya kwa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…