Godbless Lema: Wanaopigana na mimi wataadhibiwa na Mungu muda siyo mwingi

Godbless Lema: Wanaopigana na mimi wataadhibiwa na Mungu muda siyo mwingi

Yeye kama mjumbe wa kamati kuu, kwanini ashupaze shingo leo, kutangaza maridhiano hayo wakati, Makamu Mwenyekiti wake yupo? Katibu wa Chama yupo, Makamu Mwenyekiti Zanzibar yupo?
Makamu Mwenyekiti kwa wiki mbili sasa yupo kortini anatoa ushahidi, kwanini yeye ajitokeze leo kutangaza na kuyataka maridhiano hayo?

Kama nia yake ni kumtoa Mwenyekiti kwa mgongo wa maridhiano, Mwenyekiti ameshakataa watu kumfuata Ukongo, wafike mahakamani. Mwenyekiti kakataa vikao vya usiku.

Kuhusu maridhiano; Mwenyekiti yeye mwenyewe anaweza anzisha mazungumzo hayo.

Katibu wake, Naibu Katibu Bara, Makamu Mwenyekiti bara na visiwani, wote wanaongea na Mwenyekiti mahakamani, karibu wiki mbili zote, anakutana nao kama mashahidi wake, kama angetaka (Mwenyekiti) maridhiano angeweza kuayaanzisha muda wowote kwa utaratibu na protokali za kichama, sababu wasaidizi wake wote kiitifaki wanakutana nae mahakamani.

Mwenyekiti amepewa nafasi na mahakama kuongea nao (Sababu ni mashahidi wake lazima akae nao) ili kuwaandaa kiushahidi. Hilo la maridhiano kwanini litoke kwa Lema???

Lema lazima ajibu, kwanini anahitaji maridhiano hayo nje ya utaratibu wa kichama?
Ana haraka gani?
Anataka kumfurahisha nani?
Nani yupo nyuma yake?
Anataka maridhiano kwa maslahi ya nani?
Hivi huyu Lema kwa haya aliyoyaongea angekuwa yupo CCM je angebaki salama kwa watoto kama akina Kawaida? si hapo tayari angeitwa kwenye vikao vyao na kuvuliwa kila nyadhifa, eti leo CCM wanamuona Lema kafanya jambo zuri wakati wao wenyewe mauozo yao wanayafunika lakini baado yanatoa uvundo.
 
Back
Top Bottom