Tetesi: Godless Lema kumfuata mchungaji Msigwa alipo

Kwa nini umsemee Lema au kumnukuu ndivyo sivyo? Kuvembewa huko
Unauhakika na unachokisema kuwa nimemnukuu vibaya? Kwa kuwa hujasoma Cuba huwezi kuelewa andiko hili kijana
 
Mara 3 nyingi mara 2 tu kwisha habari yake
Hilo la Lema kwenda ccm sina shaka nalo. Kimmsingi Lema ameshajua ccm inatumia hela kwa namna yoyote ili kupata ushawishi, na Lema ni mpenda hela lazima atumie nafasi hiyo kufanya yake.
 
Wao wana kauli fulani ya kijusura kwamba hata wakiondoka woote - wanachama na viongozi wao - CDM ushindi uko palepale.

Bado najiuliza iwapo hilo linamantikika kihalisia na kifalsafa; ntakupelekeeni majibu yenu baadaye.
Waende ccm ili na sisi wengine tuingie Chadema kuchukuwa nafasi zao, maana kila siku wao tu.
 
Waende ccm ili na sisi wengine tuingie Chadema kuchukuwa nafasi zao, maana kila siku wao tu.
Una lengo la kuchukua nafasi tu, au una viingizo rasifu (quality inputs) vinavyoakisi matakwa makuu ya Watanzania kwa sasa?

Kuitwa kiongozi ni jambo moja, lakini kuwa kiongozi au kutimiza azma ya uongozi ni ncha nyingine kabisa.

Kuna wengi sana wanaoitwa viongozi lakini ni hasara kwa taifa maradufu. Ni heri wasingekuwepo hapo kabisa.
 
Kina Msigwa wanatuthibitishia hivyo vyeo ni ulaji.

Hupendi kula na wewe?
 
Bado Lisu 🤣🤣
 
Mbona hakuna shida, watu wahame tu na kwenda kule ambako mioyo yao iliko? Tena ni bora kuliko kuishi kinafiki.
 
Na baada ya Msigwa kushindwa uchaguzi, mara moja, haraka sana, alienda kwa Lissu akajiunga na mikutano yake ya hadhara, je walijadiliana nini na Lissu kabla ya kujiunga na CCM? Lissu alimpa kibali Msigwa atangulie CCM?
 
Kina Msigwa wanatuthibitishia hivyo vyeo ni ulaji.

Hupendi kula na wewe?
Cheo chochote kina (au chapaswa kuwa na) manufaa kwa mchewaji, ila sasa kujinufaisha kwa cheo husika ni kosa kubwa la jinai.

Hufurahii kuona katiba ikitendewa haki ili Tanzania pawe mahali sahihi pa kuishi na kufanikiwa kihalali?
 

Aha ha ha 😛
Jobless Lema bana.
 
Chadema hata sisi tuliokuwa si wachambuzi na wadadavuaji wa mambo tayari tumeshagundua madhaifu yao kutoka juu hadi chini.

Chadema sio chama strong kama tulivyodhania kabla, chadema wana madhaifu sana kwenye uongozi, maslahi binafsi chadema ni zaidi ata kuliko ccm, kiongozi wa chadema haijalishi ana hadhi gani muda wowote anaweza kuamua chochote bila kuangalia nyuma yake kuna nani, chadema kuna unafiki kuliko siasa za mahali popote hapa Africa.

Ukiangalia msururu wa viongozi wa chadema kutoka Dr Salaa, zitto kabwe hadi kufikia sasa utagundua mambo mengi madhaifu yao nadhan labda hapa kama ntaandika ntajaza page zote za jamii forums.

Mbowe na tundu lissu naamini pasina shaka yoyote wamebaki chadema kutokana nafasi zao tu walizonazo otherwise na wao wangesharudi kujiunga na ccm mapema zaid ata kuliko huo msururu uliopita, chadema ni waongo sana hakuna dalili yoyote inayoonyesha wana nia ya dhati kuleta mageuzi ya kisasa tanzania wala kuwasaidia wananchi kutokana na idhilali ya utawala wa ccm mimi.

Kule zanzibar pia walikueko wanafiki wa kisiasa kutoka upinzani lakini haikuwa kwa kiwango hichi cha chadema na ni bahati mbaya sana watanganyika tulio na matumaini na upinzani kutukombowa tumelala usingizi wa pono, yaani hakuna chochote.

Mimi nadhan Tanzania sijui ni miaka mingapi ijayo lakini kunahitajika vyama vipya vya upinzani na watu wapya sio hawa tulionao. mambo ni mengi sana ukianza kufikiria siasa za tanzania, ata kenya mabo haya hakuna, uganda hamna, south africa hakuna sijuwi ni unafiki Tanzania umetokea wapi asili yake.

Maalim seif alikuwa kiongozi pekee wa upinzani Tanzania kuwahi kutokea nimejifunza hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…