Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana

Tetesi: Godlisten Malisa avamiwa na watu wasiojulikana

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,174
Reaction score
16,794
BREAKING NEWS

NYUMBA YA MALISSA GJ IMEVAMIWA MUDA HUU NA WATU WASIOJULIKANA.

Wako hapo mpk muda huu wakilazimisha milango ifunguliwe hili waingie ndani

Msaada tafadhali
_______

Update
Habari makamanda...

Malisa yupo salama..

tuliwasiliana nae mpk mida ya saa kumi alfajiri na kutokana na uchunguzi wa swali iligundulika kua ni majambazi, anapoishi pembeni yake kuna godown na mida hiyo kuna gari ilikuja kupakia mizgo, sasa inasemekana jamaa walikua wanafuatilia hilo gari, bado hatujajua dhamira yao mpaka kwenda kwa Malisa.

Mwenyekiti wetu mkoa wa Tabora aliwasiliana na RPC mkoa na akaagiza OCD vijana wake waende kwa Malisa, kama mjuavyo kua watu wa usalama wanamtafuta kwa muda mrefu, hivyo tukakubaliana kua asikubali kutoka na ikiwezekana azime simu zake zote halafu asubuhi hii tutajua nini la kufanya tukiwa wote.

Nadhan kwa ufupi nimewaondo hofu ya swali.

=======

Habari :
Kumekuwa na taharuki tangu jana, baada ya kutoka kwa taarifa ya kuvamiwa kwa mwenyekiti wa UTG, na kada wa chadema, kamanda Malisa GJ. Taarifa hizo ni za kweli, na polisi walifika usiku wa Saa 9 kutoa msaada. Leo asubuhi tumewasiliana na RPC na ametoa maelezo nini kifanyike. Hivyo hadi muda huu Malisa yupo salama na anashughulika na utaratibu wa kipolisi.

Imetolewa na :-
Noel Shao
N/Katibu Mkuu UTG.
 
Wanataka nini na wamejitambulishaje? Kama ni polisi wampe kitambulisho hata kwa kupitishia dirishani.

Naomba wawe ni polisi na si maharamia
 
Back
Top Bottom