God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Mungu wako katengenezwa kwa a priori fallacy kwamba yupo.

Ukiiondoa hiyo a priori fallacy kwamba yupo, useme hujui kwamba yupo au hayupo, halafu ukataka ku prove yupo, logically, huwezi ku prove kwamba yupo.

Kwa sababu hayupo.
 
Hujafikiri kwamba kuna uwezekano pia wa kumtengeneza character ambaye hayupo kabisa?
Upo, haikatai bablai. Uwezekano upo na hilo halimaanishi kuwa ndicho kilichofanyika.

Umeamua kuamini kuwa tulidanganywa? Mh hivi ni kwa nini wapinga Mungu wanapenda kuamini kuwa kitu fulani ni uongo kuliko kuamini kuwa hicho kitu ni ukweli? I am the truth, the way, the life. WAO wanataka tne lies, the no-way and death.!!! why?

Mnathibitisha kuwa katika dunia yenu mnayoona ni sahihi, uongo ndio unaotawala, ooh freewill ni uongo, ooh Mungu ni uongo, oooh ukweli ni uongo seriously?
 
Huwezi kusema una limited will halafu ukasema una free will.

Hapo ni sawa na kumwmbia mtu anaweza kuchagua gari la rangi yoyote, as long as ni rangi nyeusi, halafu ukasema umempa uhuru wa kuchagua gari la rangi yoyote.
No mfano wako ni umetengeneza kamtu kamabua[straw man], bora hata ungetengeneza magari ya bluu, silver, nyeupe na nyeusi halafu mtu akachagua rangi 'yoyote'

Akiwa na akili kama zako ndo aje kulialia kwamba hajachagua freely eti kisa kulikuwa hakuna gari la rangi ya udhurungi! kwa hiyo ni sawa na hajachagua chochote.

Mi nitasema alikuwa na limited will ambayo ni free kabisa tukichukulia suala zima la rangi za magari duniani. Kiujumla alikuwa na free will ya kuchagua gari la rangi yoyote as far as rangi za magari is concerned wala hakuwa limited
 
Mungu wako katengenezwa kwa a priori fallacy kwamba yupo.

Ukiiondoa hiyo a priori fallacy kwamba yupo, useme hujui kwamba yupo au hayupo, halafu ukataka ku prove yupo, logically, huwezi ku prove kwamba yupo.

Kwa sababu hayupo.
Ni kweli logic ina limit bila premise yoyote hutembei. Nafikiri kuelewa kwako suala la cause and effect sio sheria kali kutakusaidia hapa. Kuna wakati logic yenyewe inafeli maana kuna mazingira ni premiseless!

Logic si inasema tuwe na sababu ndio tufanye maamuzi sasa unafanyeje katika mazingira ambayo sababu yenyewe ndio kwanzaa inatafutwa.?

Lakini uamuzi wa God or No God ulifanywa kwa mtindo wa tofauti kiasi. Ilibidi kuamua kwanza upande na kuuishi kama trial version [ya kama siku kadhaa] halafu ndio kutafuta sababu! Nikaingia upande A nikauishi kisha nikatazama sababu zake nikaona na faida zake na maisha yake yapojepoje, na sikuona furaha ya kweli ya kuishi huko na mwisho wake. Baada ya kuingia upande B trial version na kuuishi kikamilifu nikagundua ni upande unaoresonate vizuri na maisha na ubinadamu. Ndio kufanya uamuzi wa kumbe chema ni cha [For mankind], mungu alikuja baadae kuienhance hiyo choice maana hata Yeye ni For mankind and everything. Ndo tukapata 'of God for mankind' kwa hiyoo hiyo statement in fact ni kitu kilekile kinajirudia tu.

Ni kweli maamuzi katika kitengo hiki kwa kuondoa a-priori haiwezekaniki. Iliwezekana tu kuiweka ya hayupo na kuona yaliyomo, kisha kuweka apriori ya yupo na kuona yaliyomo. Unayoyapenda zaidi ndio unayoyachagua -- FREE WILL🐣
 
Unachanganya mambo, nani kasema everything is meaningless?

Maana ni nini?

Mungu unaweza kuthibitisha yupo na si hadithi za watu tu za uongo?
Kabla sijaitafuta official definition ya meaning sidhani kama itakosa namna fulani ya akili na kusudi.

Sasa kutokana na wewe kupinga mambo mengi yanayoendana na kusudi na mpangilio imeonekana salama kuassume tu kukuunganisha na wanaosema everything is meaningless.

Labda wewe utuambie kama unakubali kuna vitu vyenye maana na visivyo na maana pia? Je unakubali vipo? Je unakubali kuwa kuna vitu ni sahihi na vingine sio sahihi?

Let us not get caught in semantics - Niliskia ushauri toka kwenye katuni.
 
Ebhana ee, si nimeenda kugoogle hiyo 'the concept of meaning' huko google nilichokipata huwezi amini!! bado haina maelezo ya kueleweka! Imefanya kama mwenzake abbreviation anawapunguza wenzake halafu yeye mwenyewe kabakia neno reeefu! Meaning nayo anawatolea maelezo na maana wenzake halafu yeye kabakia kitu kisichoeleweka wazi.

Kwa wakana Mungu sasa si mtapata tabu sana jamani, kama tukisema kila kitu ni mpaka ukithibitishe na kukielewa kikamilifu ndio ukitumie/ukiishi sasa tutabaki na nini.?

Kwa sisi watoto wa Mungu wala hatuna shida, huwa tunavijua vitu hata kama hatujavifafanua exhaustively. Na tunaviishi na tunavifurahia. Kwa hiyo Kiranga ulitaka niijue kwanza tafsiri ya maana kabla sijaitumia kukuuliza swali kwamba je unaona vitu vina maana au hamna? Hapana mimi nataka wewe kwa uelewa wako wa maana katika dunia yako ndio ujibu hilo swali personally hukohuko kikwako.

Mimi najua vipo vya maana na visivyo na maana. Katika dunia yangu ni kitu cha kawaida mtoto sio lazima aelewe kila kitu, kwanza hawezi hadi akue. Baba yupo atatuongoza yeye anajua zaidi.
 
Mungu wako, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu uliopo unaoruhusu mabaya.

Hii si imani, hii ni mantiki.

 
Wapi nimekutisha?

Mi nachallenge hoja yako uliyoipitishia mlango wa nyuma kinyemela na namna isivyo faa kusimama kama uthibitisho kwa kukosa vigezo vya msingi we unakuja kusema nakutisha
Kuniambia kwamba ooh! hiki kitu sio logical, mara ni fallacy ili nione nakosea ama?

Hujamsoma Kisai anakuambia alishagatumia logic na kuichambua hadi akagundua kumbe ukiiendekeza inakuharibu akili.

Nadhani wewe na mwenzio hujawahi kukutana na situation ambapo logic haiapplai yaani inabidi utumie mbinu nyingine. Kwa sasa inawezekana unahisi logic ndio kila kitu. Kuna mazingira unakuta ni otherwise premiseless, premise pekee itakayoweza kukubeba ni kuwa tu wewe upo na unafanya maamuzi na unakuta haina connection yoyote ya moja kwa moja na uamuzi unaotakiwa kufanya! Ndo utajua
 
Mtu ambaye kapewa magari meusi tu, akaambiwa achague gari la rangi yoyote ile, as long as ni nyeusi, amepewa free will ya kuchagua gari la rangi yoyote ile?
 
God this, God that.

Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Hayupo kwa sababu ulimwengu uliopo unamkanusha.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Hayupo kwa sababu ulimwengu uliopo unamkanusha.
 
Mungu wako, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu uliopo unaoruhusu mabaya.

Hii si imani, hii ni mantiki.

View attachment 2250549
Je hutaki kazi ya kufanya, hutaki kukua, hutaki kuishi?

Hivi mfano kuna tofauti yoyote kati ya kuishi ukiwa umekamilisha kila kitu na kufa. Imagine uwepo duniani na hauhitaji chochote, una elimu yote, hadi vitu vyote vinavyohitaji muda uwe tayari unavyo, huhitaji kukua wala kuzaliana [una watoto wote] yaani una kila kitu then maisha kwako yatakuwa ni kitu gani. Kwa nini unataka usipambane na challenge yoyote? unajiona umekamilika?

Tuuache ukamilifu kwa Mungu yeye ndo anayejua namna ya kuexist namna hiyo, na inawezekana sio kitu kitamu[kwa mawazo yangu ya kibinadamu] zaidi ya kujipa kazi ya kulea viumbe na ulimwengu ndio maana akatuumba. Yeye anajua zaidi.

This is the best word for us to experience life, remember we are for the truth[something that you grow with], way [something you travel with, not stay static] and life. Life is for the living let us live it.
 
Mtu ambaye kapewa magari meusi tu, akaambiwa achague gari la rangi yoyote ile, as long as ni nyeusi, amepewa free will ya kuchagua gari la rangi yoyote ile?
Hapana, na ni itakuwa ni ujinga kuzungumzia suala la rangi katika mazingira kama hayo. Labda achague baina ya sifa nyingine ila rangi hata isitajwe.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Hayupo kwa sababu ulimwengu uliopo unamkanusha.
Hapana binafsi nimethibitisha kuwa Mungu yupo

Ndiyo siwezi kukuthibitishia kuwa Mungu yupo kwako.

Ki ukweli yupo [huku kwangu] na we unakaribishwa kumtambua na kuishi naye.

Yupo kwa sababu ulimwengu niliopo unamthibitisha ✅
 
Mungu wako anapenda watoto wanaokufa kwa njaa na utapiamlo wafe hivyo?

Kwa nini unaniuliza sitaki au nataka nini mimi, wakati hoja ni logical consistency ya Mungu wako?
 
Hapana, na ni itakuwa ni ujinga kuzungumzia suala la rangi katika mazingira kama hayo. Labda achague baina ya sifa nyingine ila rangi hata isitajwe.
Hapana nini? Amepewa freewill au hajapewa?
 
Hapana binafsi nimethibitisha kuwa Mungu yupo

Ndiyo siwezi kukuthibitishia kuwa Mungu yupo kwako.

Ki ukweli yupo [huku kwangu] na we unakaribishwa kumtambua na kuishi naye.

Yupo kwa sababu ulimwengu niliopo unamthibitisha ✅
Ulimwengu uliopo unathibitisha vipi Mungu yupo? Hebu dadavua hapo tupachambue.
 
Ukikataa logic umekataa ukweli

Huyo uliye mtag alijifanya kukataa logic lakini hajui hata logic ni nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…