Bado unafikiri ki-utoto na kujipa majukumu ya ki-baba kufanya maamuzi ya namna ya kuwasimamia watoto, wewe ukiwamo! Bado hatujakua kufikia hapo.
Hauna tofauti na watoto waliokaa kikao shuleni/nyumbani halafu waseme viboko havina faida yoyote. Wote tunajua viboko vinaumiza lakini je? Viboko kwa mtoto sio kitu chema?
Purpose is the king. Kusudi, kusudi, kusudi.
Kwa hiyo nikisema kitu ni chema simaanishi vile kilivyolivyo at face value. La. Bali tunaangalia kusudi lake.
Mtu anayetenda kinyume na wema na akapokea kitu kinachoendana na matendo yake hicho ni kitu chema kwake. Mtu amekataa uhai na akafa kweli, wewe nani hata useme amepata kitu kibaya. Mungu mwenyewe hatuchagulii pa kwenda leo wewe ndio umchagulie mtu hata kama hataki. Mtu amekataa kuwa karibu na Mungu, wewe unamchukua unamuweka karibu na Mungu huoni kama unampa shida? Na ki kwake hiyo pia ni jehanamu tosha kama hujui.
Halafu jehanamu yaweza kuwa ni concept tu ya kifo don't take it too literal man. Wanaomkataa Mungu yawezekana wakacease to be tu, wakaacha kuishi baada ya hapa wala wasijue lolote litakaloendelea yaani badala ya kuendelea kuishi uweponi mwa Bwana wakajikata na kupotea zzip, bassi hivyo tu sambamba na walichokiamini kwamba ndio uhalisia uliopo. Kwa hiyo ki kwao hicho ndio kitu kizuri all along.