God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Freewill haipo kwasababu Mungu ndiye anayetengeneza fate

Refer kwa kisa cha yuda kumsaliti yesu, Yuda hata kabla hajazaliwa alikuwa amekwisha andaliwa kutimiza mpango wa Mungu

Kwa maana ya kwamba hakuwa na freewill yeyote ya kuweza kuepuka usaliti

Mungu alimuumba Yuda akiwa tayari msaliti angali yupo tumboni, hakuwa na option ya kuepuka na kwamba usaliti ule aufanye zakayo au mtu mwingine yeyote.

Sasa kama mtu hufanya kile ambacho ameumbiwa aje afanye utasemaje kuwa ni freewill?

Mbali zaidi kwanini mtu ambaye anafanya kile alichoumbiwa aje afanye, aje kuadhibiwa tena?
Sawa best 🙏✨ ngoja nikuweke vizuri upande wa kiroho kuhusu kwa nini Mungu alimruhusu Yuda kumsaliti Yesu.

1. Sehemu ya mpango wa Mungu wa wokovu​

  • Kabla hata Yuda hajazaliwa, maandiko yalikuwa yametabiri juu ya kusalitiwa kwa Yesu (Zaburi 41:9, Isaya 53).
  • Ili wokovu utimie, Yesu alipaswa kusulubiwa kama dhabihu ya dhambi za wanadamu wote. Kwa hiyo Mungu aliruhusu hili kutokea ili lengo kuu—ukombozi wa wanadamu—litimie.

2. Uhuru wa kuchagua (free will)​

  • Yuda hakulazimishwa. Alikuwa na nafasi ya kubadilisha moyo wake, lakini alichagua tamaa ya fedha (vipande 30 vya fedha).
  • Mungu anatuonyesha kuwa kila mtu anawajibika na maamuzi yake, hata kama yanatimiza mpango wa Mungu.

3. Kufunua mioyo ya watu​

  • Kupitia usaliti wa Yuda, tunaona tofauti ya upendo wa kweli wa Yesu (aliyekubali kufa kwa ajili yetu) na ubinafsi wa Yuda (aliyemsaliti kwa tamaa).
  • Hii inatufundisha kuwa sio wote waliokaribu na Yesu kimwili au kikazi walikuwa na upendo wa kweli moyoni.

4. Mamlaka ya Mungu juu ya maovu​

  • Hata jambo baya kama usaliti, Mungu alilitumia kwa wema mkubwa (Warumi 8:28).
  • Shetani alitaka kuharibu, lakini Mungu aliruhusu kwa sababu alijua mwisho wake utakuwa ushindi wa wokovu.

Kwa kifupi:
👉 Yesu alimruhusu Yuda kumsaliti kwa sababu ilikuwa lazima ili wokovu utimie.
👉 Yuda alibaki na dhamana ya maamuzi yake, kwa kuwa hakulazimishwa.
👉 Mungu alitumia usaliti huo kugeuza kitu kibaya kuwa ushindi wa milele kwa wanadamu.

Unataka nikutafsirie hii kwa lugha rahisi ya maisha ya kila siku ili iwe mfano unaoeleweka zaidi?
 
Freewill ni illusion tu wala haipo in reality

Nataka nianze na Mfano wako wa kusema malaika hawana freewill na kwamba wamekuwa programmed kutii kile ambacho Mungu anawaagiza

Kumbuka freewill ni dhana yenye kuambatana na selection ya mambo mawili "ubaya na uzuri"

Sasa kama malaika hawana freewill na kwamba hawawezi kufanya ubaya, unaelezeaje ishu ya malaika muovu lucifer ambaye alifanya ubaya kwa kumsaliti Mungu?

Alitumia njia gani kufanya ubaya huo bila kuhusisha freewill?

Vipi kuhusu robo tatu ya malaika walioshawishiwa na shetani na kuungana naye katika mkakati wa kumsaliti Mungu na kupelekea vita huko mbinguni?

Hayo yote yaliwezekanaje kufanyika kama malaika wako programmed na hawana freewill ya kuwawezesha kuchagua kufanya ubaya?

Mnaofikiria kwamba mateso na migogoro ipo duniani na kwmaba mbinguni ni raha tu, mnabidi mkumbuke kuwa vita ya kwanza ilianzia huko huko

Mpaka hapo tushajua mbinguni sio sehemu salama na kwamba kuepuka kwako vikwazo huku duniani unakumbushwa kuwa na mwendelezo huo huo wa kinidhamu hata ukiwa huko.
Hoja nzito na fikirishi sana
 
Dhana ya freewill inamatatizo mengi sana
Sidhani kama binadamu ana freewill,
Kuna watu wanazaliwa na kukuzwa katika hali ya kuwa Psychopathy/sadists n.k yani hata ukijaribu kutafakari machaguzi mengine bora hawakuwa nayo maishani mwao bali ni kuelekea njia hiyo tu ya uharibifu.
 
Naam, labda yaje maelekezo mengine mkuu , haya ya sasa yana changamoto
 
Mimi nakubaliana na watu wanaosema genes, mazingira watu wanayokulia na bahati ndivyo vinaamua machaguzi na hatma za watu zaidi kwa kiasi kikubwa.
 
NAam, "freewill" labda uamue tu kuikubali ndo inaeleweka
 
Hoja nzito na fikirishi sana
Heri,ngoja nifafanue hii hoja na uhalisia ulivyo na jinsi inavyopaswa kuwa.twende sote

Muonekano tulionao ni vessel au chombo kwa iyo ufahamu utakao kuwa nao ndio utadetermine ww ni mtu wa aina gani na katika maamuzi(free will) uliyonayo ni yapi utayafanya.

Mfano hai chupa ikiwa na maziwa huitwa chupa ya maziwa na chupa iyoiyo ikiwa na maji huitwa chupa ya maji na chupa hiyohiyo ikiwa na mafuta huitwa chupa ya mafuta.

Muonekano tulionao (moyo) ni kama chupa so ufahamu utakao kuwa nao ndani yako ndio utakuwa na freewill ya nn ufanye either kibaya au kizuri japo wengi hupenda vizuri ila huishia kufanya vibaya wasijue ni sababu ya ufahamu uliotangulia ndani yao.rejea

Warumi 7:15
Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.

Tangu unazaliwa kuna maarifa na ufahamu umesoma,umexperience na umejifunza katika maisha yako,huo ndio ufahamu uliotangulia ndani yako au asili iliyotangulia ndani yako ambayo ndio mostly ww hutumia kufanya maamuzi.

Ila kusudi la Muumba ni sote tuwe na ufahamu wake yeye kupitia yeye kuishi ndani yetu na ufahamu wake ni mmoja ambao ni wa mema tu ndipo hapo tutaweza kuishi umilele(Mhubiri 3:11) na kuweza kufanya yale tunayoyapenda ambayo ni mazuri.

Ukiona mtu anafanya mabaya jua ufahamu ukiotangulia ndani yake wa mabaya (kinyume na Muumba) au ufaham wa nyoka ndio unatawala.
 
1.Mungu hafungwi na time dimension
2.Kwa Mungu kila kitu kiko clear kwenye umilele, na kabla au nyuma kwenye umilele vilevile
3.Mungu ni nini, ni nani - Hatujui.Tunachojua ni uelewa ambao bongo zetu zimeshindwa kuprocess either kwa sababu uwezo hatuna au Mungu huyohuyo katufunga.
4.Free- will ipo kwa kila mtu labda wanyama.
5.Utashi ni hatua moja kubwa ya kujustfy freewill.Hakuna binadamu asiyechakata taarifa na kufanya maamuzi basing na uchakataji wake wa taarifa...lazima kuna uchaguzi always.
6.Cha ajabu na muujiza ni kwamba despite ya kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi bila kuingiliwa as long as utalipia mwenyewe: Nguvu ya asili huwa muda wote inajaribu kutushauri pale ambapo free will zetu zinatupeleka kwenye hatari ya kufanya maovu.
7.Hofu ya wanadamu ni kifo and the strongest punishment au makosa ambayo binadamu anaweza kufanya ni kuua.
8.Tunaogopa kifo sababu hatujui kuna nini baada ya kifo. Pata pita tungejua kuna nini baada ya kifo..maisha hapa duniani yangekuwa ya hovyo sana, hofu ya kifo - kuuawa au kuua inatoa speed governor ya watu kutulia.
9.However Mungu hayuko kwenye ligi ya kifo : NDO MAANA hata mtu akifanya free- will inayoenda kusababisha kifo : Binadamu tutalaumu na kuumia sababu mtu kafa, hatutamuona tena etc..LKN Mungu usikute anashangaa why tunalaumu..sababu maybe kuna better life baada ya hicho kifo au kuna utaratibu mwingine kabisa unao-operate. THUS KWAKE IT IS NOT A BIG DEAL..
10.Hakuna kitu katika ulimwengu wowote wa kiroho au kikwili kinachoweza kuzuia free-will ya mtu.Hata shetani na uwezo wake hawezi kudetermine au kukupangia cha kufanya:
 
Adamu aliumbwa akiwa ni kiumbe cha milele. Mungu aliemuumba akampa utashi wa kupambanua na kufanya uchakuzi kwa kigezo cha yeye kumpa option ya kula au kutokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Adamu alipochagua kula tunda matokeo ikawa kukaribisha kifo. Siri ipo katika ulaji wa lile tunda. Maana lilisababisha mchafuko katika uzao wa binadamu. Kukawa na uzao wa mnyama nyoka chini ya roho ya shetani na uzao wa mwanamke ambao baba yao ni Adamu chini ya roho wa Mungu.
Zao hizi mbili moja inakomboleka na ya pili haikomboleki ila hilo ni siri kwetu sisi binadamu. Haturuhusiwi kutuoa hukumu ya kuua bali kuishi kwa amani.
Binadamu ana sehemu tatu yaani mwili, nafsi na roho, na hii ni kwa zao zote mbili.
Sasa roho ni tabia ya nafsi, kama roho ya Mungu itakaa kwenye moyo(nafsi) ya mtu, tabia yake itakuwa ni tabia ya Mungu. Na kaka roho ya shetani itakaa kwenye nafsi ya mtu, tabia yake itakua ni ya shetani.

Ila tusijidanganye kwa matendo kwa kuwa malango ya nafsi kama vile utashi, hoja, mapenzi, kumbukumbu nk vipo kwa wote. Wanapenda, wanajali, wanahurumia wa kwao wanalisha na kusomesha watoto nk.
Tofauti inayowarofautisha ni matunda ya roho kama ni ya Mungu wana Amani, furaha, upendo, utu wema, fadhili, kiasi, uaminifu sabari nk. Kwa upande wa pili ni tabia za kinyume na hayo matunda ya roho wa Mungu.
Adamu alipopoteza ule uzima wa milele kwa kuwa ni sehemu ya Mungu maana alipuliziwa nafsi akawa nafsi hai Mungu hakuridhia ampoteze kwani aliasisi pale pale mpango wa kumkomboa kwa njia ya Mungu mwenyewe kuja duniani kama jamaa wa karibu na Adamu kujipatanisha mwenyewe na kilichoanguka kwa kulipa fidia ya hukumu ya adhabu aliyoitoa mwenyewe aliposema "ukila hakika utakufa"
Yesu ndio utimilifu wa ahadi ya Mungu ya ukombozi kwa kurudisha roho wake kwa aaminie na hivyo huyo roho wa Kristo ndio ule uzima wa milele uliopotezwa na Adamu wa kwanza.
Bado hadi kwa sasa hivi suala hili lipo katika uchaguzi wa mtu binafsi kwamba achague kufa au kuishi.
Sisi hatujui ni nani ata amini na nani atakataa kuanini ila ili Mungu awe, omnipresent, omniscience,omnipotent nk anafahamu ni nani wata amini na ambao hawataamini kwa kuwa aliisha waona wakipewa hilo neno la wokovu na wakalikataa hata kabla hawajafanya hivyo.
 
Mkuu niulize tu Tunda gani alokula adam??
 
Freewill ni illusion tu wala haipo in reality

Nataka nianze na Mfano wako wa kusema malaika hawana freewill na kwamba wamekuwa programmed kutii kile ambacho Mungu anawaagiza

Kumbuka freewill ni dhana yenye kuambatana na selection ya mambo mawili "ubaya na uzuri"

Sasa kama malaika hawana freewill na kwamba hawawezi kufanya ubaya, unaelezeaje ishu ya malaika muovu lucifer ambaye alifanya ubaya kwa kumsaliti Mungu?

Alitumia njia gani kufanya ubaya huo bila kuhusisha freewill?

Vipi kuhusu robo tatu ya malaika walioshawishiwa na shetani na kuungana naye katika mkakati wa kumsaliti Mungu na kupelekea vita huko mbinguni?

Hayo yote yaliwezekanaje kufanyika kama malaika wako programmed na hawana freewill ya kuwawezesha kuchagua kufanya ubaya?

Mnaofikiria kwamba mateso na migogoro ipo duniani na kwmaba mbinguni ni raha tu, mnabidi mkumbuke kuwa vita ya kwanza ilianzia huko huko

Mpaka hapo tushajua mbinguni sio sehemu salama na kwamba kuepuka kwako vikwazo huku duniani unakumbushwa kuwa na mwendelezo huo huo wa kinidhamu hata ukiwa huko.
Mreno wa bumbuli, enzi hizo hujaanza ubishi
 
Back
Top Bottom