Unachoamini huenda ni uwongo, zamani kanisa liliamini jua ndilo linazunguka Dunia, waliopinga waliuwawa. Mpaka wakati wa Copernicus revolution. Basi huenda hoja zako za kuamini uwepo wa Mungu si kweli. Duniani hakuna maabara ya kuhakikisha uwepo wa Mungu. Tuamini tu kwa umbaaaaali! Kuwa kuna "first cause" Hiyo utaijua wakati roho itakapotengana na mwili.
Kwanza Mimi si katika hiyo imani ya kanisa!.
Pia Kuna kitu ambacho hukielewi au hukutumia neema ya akili kutafakari na kufanamu.
Tunapo sema Ujumbe wa Mungu umekuja kwa watu wanao ishi katika dunia!
Maekezo yoyote yatakayo tumika kuelezea Jambo ni lazima yachukue uoni wa mahali husika!.
Nakupa Mfano Chukua Mpira wa Miguu,
Fanya upande wa kitundu cha kujazia upepo kiwe kimeelekea Juu na upande huo upe Jina la Mashariki,
Ule upande ulio elekea chini upe Jina la Magharibi,
Upande wa ubavu wa kulia upe Jina kaskazini na Upande wa kushoto wa mpira upe Jina la kusini.
Jenga taswira kwamba Kuna viumbe wanao ishi Kuzunguka Mpira ambao upeo wao wa uoni hauvuki mpira.
Bila shaka ile Mashariki ya Mpira haitokuwa ni Mashariki ya Dunia!
Ule Mpira hata ukiupindua juu chini ule upande wa kitundu upepo utakuwa ni Mashariki.
Ujumbe utakao wapelekea viumbe wanao ishi katika huo mpira ni kwa Mujibu wa uoni wao! Sio kwa uoni wa wanao utazama mpira!
Utatoa maelekezo viumbe wale Mashariki itakuwa ni Mashariki yao sio Mashariki ya walio nje ya Mpira!.
Bahati nzuri Maandiko matakatifu yamezingatia hali ya uoni wa watu na uhalisia wa kitu!.
Maandiko yanapo waambia watu watazame Jinsi Jua linavyo toka Mashariki kuelekea Magharibi yanazingatia kile wanacho kiona wakusudiwa ujumbe siyo walio nje yake.
Hakuna Mtu anae weza kuona Mwendo wa Mzunguko akiwa katika ardhi hii bali anaona jua likitoka Mashariki kuelekea Magharibi kwa macho safi.
Ujumbe unapo kuja kumwambia atazame unamaanisha kwa mtazamo wa aliyepo hapo si kwa mtazamo wa nje yake!
Kwa sababu ujumbe haukuletwa kwa alie nje!.
Huyo MwanaSayansi mpaka kugundua kuwa Dunia ndiyo inajizungusha katika muhimili wake kutengeneza usiku na Mchana alitoka nje ya eneo!
Ukitoka nje ya eneo husika ule ujumbe sio wako tena kwa sababu utakuwa na mtazamo tofauti haukusu na haukuletwa kwa sababu ya mtu aliye nje!
Mfano wa pili: Nakupa maelekezo kulingana na Mahali ulipo!
Kuna mti wewe unautazama Kuna chupa nimeiweka upande wa pili wa Mti Kisha nakutumia ujumbe kwa kuzingatia uoni wako na mahali ulipo kaa kwamba chupa ipo nyuma ya Mti,
Ujumbe huu kwako ni sahihi kulingana na hapo ulipo!
Lakini utakuwa ni ujumbe wa uongo ikiwa utausomea upande wa pili kwa sababu itaonekana kwako ipo mbele ya mti na si nyuma ya Mti.,
Hakuna anaweza kuona Mzunguko wa dunia akiwa anaishi katika mgongo huu wa ardhi, Hata Mwana sayansi hawezi kuthibitisha Mzunguko wa dunia ikiwa katika ardhi!
Akitaka kuthibitisha kuwa Dunia ni tufe ni lazima ushahidi wake aulete kwa mtazamo wa nje ya ardhi hii.
Sasa ujumbe wa dunia tambarare ulikuja kwa wale wanao ishi katika ardhi kwa kuzingatia uoni wao si kwa uoni wa mtu aliyetoka nje yake kwa sababu hata mtu akitembea kutaka bara moja kwenda jingine hato experience Mzunguko wa dunia.
Kwa hivyo ujumbe sahihi wa maelekezo mtu aliyoka katika mgongo wa ardhi ni dunia iliyo tambarare!.
Kwa Bahati nzuri Mungua alijua kuwa Kuna watu watakao toka nje ya Dunia na kuiona katika umbo tufe au Duara akatoa Maelezo yanayo ashiria umbile hilo katika baadhi ya aya.
Pia alitoa Maelezo ya jinsi usiku na Mchana unavyo patikana na katika maelezo hayo unapatikana ushahidi unao kubaliana na tafiti za kisayansi!
Kuwa Dunia inaumbo la Mzunguko inafanya mwendo na kujizungusha .
Hivyo Maandiko yamezingatia uoni wa Aina mbili!
Ule ujumbe unaonzungumzia Maisha na wanachomipitia watu katika Maisha unazingatia uoni wao!
Ujimbe unao onyesha kwa mtazamo wa pili ni ule unao toa dalili ya Uwepo wa Mungu kwa wafafiti.
Sasa wewe Kama hujajitosheleza kwa utafiti wako ni suala lako binafsi.