Hello y’all..
NB: Naomba moderator mada hii msiihamishie jukwaa la dini maana huko itakosa wachangiaji na lengo langu la kutaka kujuzwa jambo hili halitatimia and that will leave me frustrated and bums me out, Natuamaini mtatii takwa langu hili. Ahsanteni.
Binafsi kiimani ni muumini wa kanisa Katoliki kwa kuzaliwa na kubatizwa, pia ninaamini na kuisadiki kanuni ya imani yangu katoliki isemayo “Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi muumba mbingu na dunia na kwa Yesu Kristu Bwana wetuu….” Self-schemas: katika sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.
Self-Concept ni i hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future self (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo). Toka nilipoanza kutambua Self Concept yangu Nimekua na swali ambalo kwakweli pamoja na kuisadiki imani yangu hii na kupokea ya Sakrament takatifu ya Communion swali hilo limekua mwiba mchungu na kikwazo kikubwa katika imani yangu hii na Mungu kwa ujumla.
Toka nilipoanza kujitambua nimejaribu kuwashirikisha watu wenye uelewa jambo hili ila bado sijapewa majibu thabiti….natumaini hapa JF nitapewa maelekezo vyema , mnivumilie kama maelezo yatakua marefu maana hua siwezi kuelezea kwa ufupi but it worth your time.
The One above all, In-Betweener and The One bellow all.
Monotheism ni imani ya kua kuna Mungu mmoja pekee ambae aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo. Watu wanao amini katika imani hii ni wafuasi wa dini zilizotokana na Ibrahim ambae anachukuliwa kama baba wa imani ambazo ni Judaism, Ukristo,uislam, mandaeism ,Rastafarian na Bahai. Mungu wa imani hii ndio huyu tunayemfahamu mimi na wewe ambae ana sifa kuu tatu ambazo ni yupo kila mahali, anajua kila kitu, na anaweza kila kitu. Omni ni neno la kilatini lenye maana ya yote au kila kitu na Sciens ni neno la kilatini likimaanisha kujua(conscious)……. Moja kati ya sifa kuu tatu za Mungu nilizotaja hapo juu ni Omniscience ikimaanisha kwamba Mungu anajua yote yaliyopita,yaliyopo na yajayo.
The Great Chain of Being ni mchoro au nadharia ambayo inaonyesha kwamba maisha ya mwanadamu yapo kwenye ngazi /mtiririko Fulani ambapo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,mimea halafu chini kabisa yupo shetani. Mungu ni the one above all, mwanadamu ni aliyekati /in-betweener na shetani ni the one below all. Unajua mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote walioumbwa na mungu kuzidi hata malaika ndio maana kuna malaika wanafanya kazi kwa wanadamu ya kutulind, Moja kati ya utajiri na kitu kikubwa alichonacho mwanadamu hakuna kiumbe kingine anacho ni uwezo wa kuchagua na kuamua Kuishi vile atakavyo yeye yaani Free Will….Katika Great chain of being mwanadamu amewekwa katikati (In-Betweener) maana yeye ameumbwa na roho isiyokufa (immortal) na mwili ambao unaokufa (mortal) hivyo inamuwezesha yeye kuishi duniani au mbinguni . Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi Uungu kwa kutenda mema maishani mwake au ushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Kwakua mwanadamu ana free will uamuzi ni wake ni kuchagua kwenda kwa The One above all au kwa the one bellow all.
Free Will is illusion (?)
Kuna mada Fulani niliwahi kusema kwamba tukio la kuumbwa Adam na eva hadi kufukuzwa eden linapinga uwepo wa Mungu kwa kupinga sifa tatu alizonazo Mungu kwamba anaweza yote,anajua kila kitu na yupo kila mahali… ndio maana mimi hua nalichukulia kama lugha ya picha tu na sio tukio halisi na kama kweli ni kweli lilitokea kama lilivyoelezewa kwenye kitabu cha mwanzo basi linaonyesha Mungu hafai kupokea sifa tunazompa. Kama anajua kila kitu je wakati anamuumba adamu bila Eva hakujua kwamba adamu hatapata uhitaji wa kua na mwenza? Yupo kila mahali jewakati adam na eva wamekula tunda hakuwepo pale walipojificha hadi aanze kuuliza wako wapi? Alikua hajajua juu ya tukio la adam kula tunda maana lilimuudhi kwelikweli like he didn’t know a thing from a first place.
Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni? Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo. Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?
Kuna phrase protestant wanapenda kusema kwamba sisi wakatoliki hatujui kusoma na kuielewa biblia, naamini name ni mmoja wapo nisiojua kusoma biblia. Hivyo basi napenda kuwaalika wale wote wenye uelewa juu ya jambo hili. Naombeni mnijuze kama Mungu anajua hatima yangu na hukumu yangu siki ya mwisho na kama anajua je naweza kubadirisha? Kama mchezo kautengeneza yeye na sharia za mchezo kazitengeneza yeye je wachezaji wanawezaje kua huru?
Vinjii…
Swali la Msingi katika mada hii ni Uhalisia wa uwepo wa Hiyari(free will) kwa Mtu.
Maswali yako yanaihoji zaidi imani yako Juu ya Mwenyezi Mungu Kama ipo sahihi au la!.
Ikiwa hupati Majibu katika Imani yako basi ujue tatizo lipo kwenye Imani yako na si Uhalisia wa Jambo ambalo unaliuliza.
Katika Bibilia na Quran vyote vimeandika Mungu baada ya kuumba vitu vyote na kabla ya kumuumba Mtu alionyesha azma ya juu ya alivyo viumba!
Kwenye Bibilia Mungu anaonyesha lengo la kumuumba Mtu ni kwa ajili ya kuwa msimamizi na mtunzaji wa vitu vyote katika nchi. Zingatia kwamba lengo limetangulia kabla ya kumuumba.
Katika Quran Mungu pia anaonyesha lengo la kumuumba Mtu kabla ya kumuumba pale alipo waambia Malaika" Mimi nitaweka katika Ardhi kiongozi(Khalifa) Msimamizi na mwangalizi wa vitu vyote.
Kabla ya kwenda kutafuta Majibu mbele ya tukio yakupasa utulie katika lengo hili na kutafakari ili kupata Majibu.
Unatakiwa kutafakari huyu kiongozi ,Msimamizi,Mwangalizi wa vitu vyote anatakiwa awe vipi ili aweze kuifanya kazi iliyo kusudiwa!.
USIMAMIZI JUU YA KITU: kitu mpaka kuwa na sifa ya kusimamiwa,au kutunzwa au kuongozwa, Ni kwamba kitu hicho kinakuwa na sifa kutoleta ufanisi kisipo simaniwa, kuharibika kisipo tunzwa,na kuto ongoka kisipo ongozwa.
MSIMAMIZI: Msimamizi ili aweze kutenda kazi kwa ufanisi ulio kusudiwa ni lazima awe na sifa zinazo weka kukidhi majukumu anayo pewa!
Kujua namna kusimia kitu ambacho kina sifa ya ulazima wa kusimamiwa, ikiwa na maana kisipo simamiwa hakitaleta faida na badala yake kitaleta madhara.
Msimamizi ni lazima ajue faida ya usimaimizi na ubaya wa Kuto simamia!
Kwa maana nyingine ni lazima aujue wema wa kitu na ubaya wa kitu ili aweze kukisimamia kibaki katika wema ambao anaujua na kisilete ubaya anao ujua,
Vile vile kutunza kitu, Ina maana ni lazima kile chenye kutunzwa kiwe kina sifa mbili sifa ya kubaki katika uzuri kikitunzwa au kuharibika kisipo tunzwa!
Ni lazima mtunzaji awe na sifa ya kujua uzuri ni upi katika anacho kitunza na ubaya ni upi asipo kitunza!
Hivyo kwa kuwa kaumbwa kwa ajili ya kutunza Basi ni lazima ajue wema na ubaya wa kile anacho kitunza ili akitunze kisiharibike.
Vile vile kuongoza ni lazima kiongozi ajue hii ndiyo njia sahihi na hii siyo njia sahihi( njia ya wema ni ipi na njia mbaya ni ipi).
Tafakari hii ni kabla Mtu hajaumbwa ,unatakiwa kujua sifa anazo takiwa kuwa nazo kwa kuangalia lengo analo letwa kwa ajili ya kulitimiza.
Tukija Ndani ya Edeni tunamkuta Adamu akiwa hajui kuchanganua lililo sawa na lisilo sawa hata hajui Kama yupo uchi au kavaa!
Ni sawa sawa na Mtoto ambaye bado hajaweza kuchanganua Mambo!.
Kwa kawaida Mtoto mdogo, au Mnyama hapewi Usimamizi wa vitu si kwa sababu wao si viumbe la!
Bali ni kwa sababu ya kukosa sifa ya uchanganuzi(hili sawa na hili si sawa).
Kwa hali ya Adamu aliyo kuwa nayo Edeni ya kukosa Elimu ya upambanuzi bado ilikuwa haimpi sifa ya kuwa msimamizi wa vitu vyote.
Si Jambo rahisi kusimamia kitu ambacho hukijui Wala hujawahi kukiona katika Maisha , Adamu alihitajia kupata semina elekezi ya namna gani ataweza kutimiza majukumu yake.
Mungu alimwambia Adamu "KULA KATIKA BUSTANI HII CHOCHOTE UPENDACHO" hapa Adamu anaongozwa na Mungu nini cha kufanya!
"USILE KATIKA MTI HUU" hili ni katazo!
Kwa hiyo tunapata KULA ni Muongozo sahihi wa Mungu!
USILE: Ni katazo la Mungu.
Adamu anafundishwa namna ya Kufuata Muongozo na kukatazika kwa Maonyo.
Mungu anamleta Ibilisi Edeni, huyu Ibilisi aoishafukuzwa katika rehema ya Mungu iweje awepo tena Eden?
Ukitafakari utagundua Mungu alimleta Makusudi kwa Adamu ili ajifunze ubaya wa Ibilisi.
Akamuacha Ibilisi amdanganye ili ale katika Mti alio katazwa!
Kitendo cha Adamu kula katika Mti ule ni kukiuka katazo la Mungu.
Mti ule ulikuwa ni kielelezo cha ile sifa ambayo Adamu alikuwa bado hajaipata sifa ya kujua wema na ubaya ambayo ilikuwa ni lazima awe nayo ili kutimiza lengo la kuumbwa kwake.
Kwa ushawishi wa Ibilisi Adamu anakula katika mti aliyo katazwa na Elimu ya Utambuzi wa wema na ubaya unambainikia!
Ili kutambua Madhara ya ubaya wa kitu na uzuri ni lazima uwe katika hali ya utimamu wa akili.
Ndiyo maana Mungu aliruhusu Utambuzi upatikane katika tukio hili.
Ili Adamu aweze kuona na kutambua kosa lake na aweze kumtambua Adui mwenye kumshawishi kuacha Makatazo ya Mungu.
Kwa Mujibu wa Quran baada ya Adamu kufanya kosa kwa kula Katika mti ule,Mungu aoimfundisha Adamu Jinsi ya kuomba msamaha,
Si rahisi kwa Kiumbe kipya kujua nini maana ya kosa na nini maana ya kuomba msamaha bila mafunzo ya vitendo!
Hivyo Mungu alimfundisha Jinsi ya kuomba msamaha anapo fanya makosa!
Baada ya Adamu kuomba Msamaha Mungu akamsamehe!
Ila alimfukuza asikae Eden(peponi Mahali pa Ahadi ya Maisha ya Milele) kwa sababu haikuwa lengo .
Lengo ilikuwa ni kuishi katika dunia hii tunayo Ishi akiwa na utambuzi na Elimu kamili ya Usimamizi .
Kwa hiyo katika tukiobla Edeni Adamu Alijifunza baada ya kutolewa kwenye neema!
Anajua kilicho msababisha kutoka katika neema ni kutifuata Muongozo wa Mungu na kuto katazika na katazo la Mungu!
Na kamuona Ibilisi kuwa ni adui kwa sababu huyo ndiyo aliye mshawishi kuacha Kufuata Muongozo na kufanya aliyo katazwa!
Kwa hivyo amejifunza!
Huku katika Maisha haya ya Dunia halisi adamu kapewa Muongozo yeye na kizazi chake ,atakuwa mwalimu mwema wa kuongoza kizazi katika Kufuata na kutii Muongozo.
Kapewa Makatazo atakuwa Mwalimu mwema kwa kizazi chake kutii Makatazo ya Mungu.
Kauona uadui wa Ibilisi,atakuwa Mwalimu kwa kizazi chake kuwafundisha wamuepuke Ibilisi na ushawishi wa kutotii Makatazo ya Mungu.
Aliishi Padiso, atawahadithia kizazi chake mahali pa ahadi ya Milele kwa kuwa yeye ameishi kwa Muda.
Sasa hizo hadithi za Mungu alikuwa anapunga upepo hazina maaana! au hajui nini Adamu atafanya ni hadithi za kupuuza!
Umesha ambiwa ndani ya konde Hilo kuna Magugu na ngano wewe kwa kuwa unaakili salama,inaweza kutambua hii ngano na hili gugu.
Kuhusu Adamu kuto kuwa na Mke kabla! haimaanishi kwamba Mungu alikuwa hajui kuwa Adamu atahitajia mke.
Kabla ya kujenga dhana hiyo hasi kwa Mungu kwanza tafakari umbile la Adamu mpaka yeye kuwa na umbile la namna ile ni maana kwamba Mungu alimuumba vile kuwa Mwanamume anaehitajia mke kwa hiyo ni suala la muda tu.
Kabla Mungu hajamuumba Mtu alisema atamuumba Mtu mume na Mtu mke wakaijaze dunia!.
Lazima aliweka mpango wa kjzaana ambao ndiyo unaupata katika umbile la Adamu.
Tazama wanyama ndege wote waliwekwa dume na Jike kwa ajili ya kuzaana ! Kwa hiyo Adamu kuwa dume kwa wakati huo Mungu alikuwa anajua kabla suala Hilo.
Kuhusu free will ni kwamba binaadamu wamepewa Jambo na lipo wazi hata kwako wewe!
Suala la kuamini au kuto kuamini ni swala la Hiyari Ila Mungu anakuta uitumie hiyari yako kwa kufuata Muongozo wake na kumuabudu yeye peke yake.
Jambo hilo ndilo litakalo kupa faida na ufanisi wewe!
Wakati hiyari ya kuchagua uovu ni maangamivu kwako.
Mungu anataka tutumie uhuru wa maamuzi utufikishe katika mafanikio yetu,
Adhabu anazo zitoa kwa wale wanao tumia hiyari zao vibaya kwenda katika njia ya maangamivu si kwa ajili ya kumpokonya mtu uhuru wa kuchagua bali ni adhabu za kutulea tukumbuke njia sahihi.
Ni Kama mwalimu anapotoa adhabu kwa wanafunzi lengo likiwa ni kuleta ufanisi kwa watu.
Lengo la Maisha ni wapatikane walio tumia hiari zao kwenda katika Njia ya wema!
Hawa wanao tumia hiayari zao nje ya lengo hawatokuwa na faida katika Maisha ya duniani Wala peponi.