Niliwahi kusema hili katika uzi wangu fulani hivi, na leo nakazia, ni hivi: fikra zangu zinanituma kuwa dhana ya free will na Mungu muweza wa yote ni kama pande mbili za sarafu moja. Ili upande mmoja uonekane ni lazima upande mwingine usionekane.
Ili binadamu awe na free will basi inabidi Mungu asiwe muwezz wa yote, kwa maana ya kwamba kuna vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wa Mungu.
Na kama Mungu ni muweza wa yote basi binadamu hawezi kuwa na free will.
Hii ya kusema kwamba Mungu ni muweza wa yote lakini pia ametupa free will kuchagua mema na mabaya ni haiwezekani. Huwezi kuweka sarafu ya shilingi 100 mezani na ukaona Nyerere na swala kwa wakati mmoja. Hell no.