Hello y’all..
NB: Naomba moderator mada hii msiihamishie jukwaa la dini maana huko itakosa wachangiaji na lengo langu la kutaka kujuzwa jambo hili halitatimia and that will leave me frustrated and bums me out, Natuamaini mtatii takwa langu hili. Ahsanteni.
Binafsi kiimani ni muumini wa kanisa Katoliki kwa kuzaliwa na kubatizwa, pia ninaamini na kuisadiki kanuni ya imani yangu katoliki isemayo “Nasadiki kwa Mungu baba mwenyezi muumba mbingu na dunia na kwa Yesu Kristu Bwana wetuu….” Self-schemas: katika sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.
Self-Concept ni i hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future self (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo). Toka nilipoanza kutambua Self Concept yangu Nimekua na swali ambalo kwakweli pamoja na kuisadiki imani yangu hii na kupokea ya Sakrament takatifu ya Communion swali hilo limekua mwiba mchungu na kikwazo kikubwa katika imani yangu hii na Mungu kwa ujumla.
Toka nilipoanza kujitambua nimejaribu kuwashirikisha watu wenye uelewa jambo hili ila bado sijapewa majibu thabiti….natumaini hapa JF nitapewa maelekezo vyema , mnivumilie kama maelezo yatakua marefu maana hua siwezi kuelezea kwa ufupi but it worth your time.
The One above all, In-Betweener and The One bellow all.
Monotheism ni imani ya kua kuna Mungu mmoja pekee ambae aliumba ulimwengu na vyote vilivyomo. Watu wanao amini katika imani hii ni wafuasi wa dini zilizotokana na Ibrahim ambae anachukuliwa kama baba wa imani ambazo ni Judaism, Ukristo,uislam, mandaeism ,Rastafarian na Bahai. Mungu wa imani hii ndio huyu tunayemfahamu mimi na wewe ambae ana sifa kuu tatu ambazo ni yupo kila mahali, anajua kila kitu, na anaweza kila kitu. Omni ni neno la kilatini lenye maana ya yote au kila kitu na Sciens ni neno la kilatini likimaanisha kujua(conscious)……. Moja kati ya sifa kuu tatu za Mungu nilizotaja hapo juu ni Omniscience ikimaanisha kwamba Mungu anajua yote yaliyopita,yaliyopo na yajayo.
The Great Chain of Being ni mchoro au nadharia ambayo inaonyesha kwamba maisha ya mwanadamu yapo kwenye ngazi /mtiririko Fulani ambapo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,mimea halafu chini kabisa yupo shetani. Mungu ni the one above all, mwanadamu ni aliyekati /in-betweener na shetani ni the one below all. Unajua mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote walioumbwa na mungu kuzidi hata malaika ndio maana kuna malaika wanafanya kazi kwa wanadamu ya kutulind, Moja kati ya utajiri na kitu kikubwa alichonacho mwanadamu hakuna kiumbe kingine anacho ni uwezo wa kuchagua na kuamua Kuishi vile atakavyo yeye yaani Free Will….Katika Great chain of being mwanadamu amewekwa katikati (In-Betweener) maana yeye ameumbwa na roho isiyokufa (immortal) na mwili ambao unaokufa (mortal) hivyo inamuwezesha yeye kuishi duniani au mbinguni . Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi Uungu kwa kutenda mema maishani mwake au ushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Kwakua mwanadamu ana free will uamuzi ni wake ni kuchagua kwenda kwa The One above all au kwa the one bellow all.
Free Will is illusion (?)
Kuna mada Fulani niliwahi kusema kwamba tukio la kuumbwa Adam na eva hadi kufukuzwa eden linapinga uwepo wa Mungu kwa kupinga sifa tatu alizonazo Mungu kwamba anaweza yote,anajua kila kitu na yupo kila mahali… ndio maana mimi hua nalichukulia kama lugha ya picha tu na sio tukio halisi na kama kweli ni kweli lilitokea kama lilivyoelezewa kwenye kitabu cha mwanzo basi linaonyesha Mungu hafai kupokea sifa tunazompa. Kama anajua kila kitu je wakati anamuumba adamu bila Eva hakujua kwamba adamu hatapata uhitaji wa kua na mwenza? Yupo kila mahali jewakati adam na eva wamekula tunda hakuwepo pale walipojificha hadi aanze kuuliza wako wapi? Alikua hajajua juu ya tukio la adam kula tunda maana lilimuudhi kwelikweli like he didn’t know a thing from a first place.
Mungu anajua kila kitu kutuhusu sisi wanadamu, anajua kesho nitakua wapi,nitakula nini na nitakufa lini...pia ametupa uwezo wa kuchagua kuishi ville tupendavyo bila yeye kutuingilia(free will) sasa hapa ndio kuna msingi mkuu wa mada yangu ambapo imekua ikinitatiza sana jambo hili. Je kwakua Mungu anajua kila kitu, Je anajua kama mimi nitakua mbaya au mwema? Je anajua kwamba mimi nikifa nitakua wa mbinguni au wa motoni? Na kama anajua nikifa nitafikia motoni je mimi naweza kubadirisha nisiende motoni? Kumbuka kwamba kama nitaweza kubadirisha nikaenda mbinguni badala ya motoni basi Mungu anakua hajui kila kitu kuhusu mimi…Pia kama anajua moja kwa moja nitaenda motoni basi wanadamu hatuna uhuru wa kuchagua kufanya yale tupendayo. Mungu kama anajua tutachagua kufanya kitu Fulani kwa uhuru basi huo sio uhuru tena bali tunapangiwa yale ya kuchagua hivyo free will hatuna its illusion na kama Mungu hajui kama nitachagua jambo Fulani kwa uhuru basi anapoteza sifa ya kujua kila kitu toka kwangu.?
Kuna phrase protestant wanapenda kusema kwamba sisi wakatoliki hatujui kusoma na kuielewa biblia, naamini name ni mmoja wapo nisiojua kusoma biblia. Hivyo basi napenda kuwaalika wale wote wenye uelewa juu ya jambo hili. Naombeni mnijuze kama Mungu anajua hatima yangu na hukumu yangu siki ya mwisho na kama anajua je naweza kubadirisha? Kama mchezo kautengeneza yeye na sharia za mchezo kazitengeneza yeye je wachezaji wanawezaje kua huru?
Vinjii…
Mambo vipi,Mimi ni MTU wa mungu,ninajibu kulingana na Dini zetu na utafiti wangu WA kumjua mungu.nabase kwenye Dini zote za ibrahimu
,HAKIKA MUNGU YUPO NA KWAKE TUTAREJEA.
Kizazi cha ibrahimu
Ismail-waislamu
Isaka-wakristo
Etc
wewe umebezi kwenye biblia inasemaje na sio VITABU vya Dini vinasemaje.
BILA KUPOTEZA MUDA TUANZE
FREE WILL IS ULLUSION
MUNGU AMEKUUMBA NA AMEKUFANYA WEWE NI BORA SANA KUSHINDA VIUMBE VINGINE VYOTE,NDIO MAANA SHETANI NA WIVU WAKE JUU YAKO AMETENGENEZA VITA KUBWA NA BATO KUBWA SANA NA MUNGU KWA SABABU YAKO.NA AMEMUAHIDI MUNGU KWENDA NA WEWE MOTONI MANA MOTO UMETENGENEZWA KWA SABABU YA SHETANI SIO WEWE MWANADAMU,ILA UKIWA UFWASI WA SHETANI HAKIKA MOTO UTAKUUSU.
SIFA ULIZOTAJA HIZO NI CHACHE MNO KWA MUNGU,
ALIKUWA ANAUWEZO WA KUMFINYANGA ADAMU NA KUFUTILIA MBALI PROJECT YENYEWE.
1.ANAWEZA YOTE:
ALIMJUA ADAMU KAMA ATAKUWA MPWEKE NDIO MAANA AKAMUUMBIA HAWA KUTOKA KWENYE UBAVU WAKE ALIIANGALIA FUTURE YA ADAM.HAKUWA AMEKAMILISHA MISSION YAKE BADO KWA ADAMU.
Biblia imeandikwa na wanadanu na imeelezewa short Sana coz imebeba story ya dunia.story ya dunia haiwezi tosha kwenye kitabu KILE.
2.MUNGU YUPO KILA SEHEMU
Adamu aliambiwa usile MTi wa mema na mabaya HAKIKA madhara yake NI makubwa.
Mungu alitaka kuona utii wa mwanadamu juu yake,mungu alimuamini Sana mwanadamu,mungu anampenda Sana mwanadamu.
Madhara ya Ule mti NI
Kufa,
Kuhukumu mema na mabaya
Kipawa cha mungu kupungua
Hofu
Dhambi
Swawabu
Etc
Mungu Hakumtafuta adamu Ila alipotembelea bustanini alipo adamu na hawa.kutokana na madhara ya lile tunda,adamu na mkewe walisikia sauti hasilia ya mungu,iliyowafanya wapagawe na kukimbizana wakati mungu ameenda kuwatembelea,na mungu alishajua Kila kitu na alimuuliza adamu Kwa kumtega Tu ili aone adamu atafanya nini.
FREE WILL
Hapa kunakitu hujakijua mkuu na NI mada ndefu.ila inshort,mungu anajua unawaza nini.na mwanadamu awezi kujiongoza pekeake.yani Sawa Sawa umwache mtoto nyumbani ukidhani ANAUWEZO WA kujiudumia Bila kumprovidia Kila kitu.
Huna free will ya kuzidi mipaka ya mungu,Sana Sana uwe SHETANI.
-Kujua utakufanye mungu hajui Ila anaangalia umekufaje.
-utakula nini,utakula chochote alichokuumbia na anavyokupa rizki Kwa kadri ya uwezo wake
-unauwezo wa kwenda peponi au MOTONI machaguo NI yako sio ya mungu juu yako
Bado hujamjua mungu VIZURI na matendo yake,soma Sana dig research.