Kuna kusudi kwa kila jambo, na sio kwamba linaletwa na Mungu peke yake. La.
Tunachangia wote kufanya mambo hayo yatokee. We make sh*t happen.
Mimi nitasema hata kama Mungu hapendi watoto wafe kwa utapiamlo, lakini jua pia Mungu hapendi kuingilia..... No. Nazirudia hizi sentensi kwa neno la kufaa zaidi.
Mimi nitasema hata kama Mungu anapenda watoto wapate lishe bora, pia jua kwamba anapenda sisi tufanye maamuzi yetu kama wanadamu, kama jamii bila kuingiliwa kwa mabavu. FREE-WILL
Watoto kufa njaa unaweza kusema ni matokeo ya shughuli za kibinadamu ikiwamo uchafuzi na hasa VITA. Tutajifunzaje ubaya wa vita kama hatutayaishi madhara ya kuchagua njia za kivita? Au ndo ulitaka tuzaliwe na ujuzi wote mojakwamoja tujue vita ni mbaya tu automatically na tukitaka tufanye vita tuzuiliwe kinguvu - Where is the purpose of will then?