Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Upo vizuri sana, hivyo ndivyo ilivyoMuda ni kiumbe cha Mungu...Mungu ameumba muda/nyakati. Yeye hawi governed na Muda yaani hana jana, hana leo wala hana kesho ila ametuumbia usiku na mchana ziwe kama ishara za kutambua uwepo wake na pia zitusaidie kujua hesabu za siku, miezi na miaka. Hivyo ukimuwaza Mungu usimtazame ktk muda.
Ametuumba akiwa anajua jana yetu, leo yetu na kesho yetu...ameipa nafsi uhuru imuabudu au imkatae. Hana sifa ya kuwadhulumu waja wake kabisa, infact amejiharamishia dhulma. Anajua nafsi nn zitachagua na ameweka reward /malipo kwa kila chaguzi litakalofanywa na nafsi iwe ni baya au zuri.
Imani ingekuwa uhalisia basi leo kungekuwa na imani mojaImani kwa ilivyotumika ni muunganiko wa uhalisia kuhusu ukweli wa jambo/mambo ulivyo kama mtu binafsi anavyoona mwenyewe. Imani ni binafsi unaijua mwenyewe imani yako.
Kama ndicho unachokitaka basi amini kwamba ulimwengu huu uliopo ndio huo unaoutamani, ni suala la muda tu.
Ulimwengu tulionao unayo mazuri yote yanayompendeza kila mtu kwa namna yake katika dunia/[uhalisia] wake, hakuna uwezekano wa watu kukosoa chochote katika uhalisia wao. Bali watakosoa vitu vingine tu katika uhalisia wa wenzao walio katika dunia nyingine.
Natumai sasa nimejibu tena, najua nishajibu zaidi ya mara moja.
Kuumwa tumbo ni jambo jema kwa nani?Kuumwa tumbo ni kusudi jema kwa hiyo being nzima, kuanzia mtu [kama consciousness ya mtu], mtu kama mwili wa mtu, na hizo seli za tumbo na hata seli zote za mwili wa huyo mtu......... in fact ni chema kwa mke/mme wa huyo mtu, familia ya huyo mtu, jamii na taifa na dunia kwa ujumla. WHY? Tumbo linapouma tunakuwa na taarifa wote kwamba kuna kitu hakiko sawa na juhudi zinafanyika tunarudisha AFYA kwa mtu husika ambaye uwepo wake ni faida kwa wote.
Sisi ni finite, I mean miili yetu ina mwisho na hata hilo jambo la miili yetu kuisha ina kusudi jema pia🤭. Purely materialist kuelewa hilo labda chukulia metamofosisi za kipepeo. Kutoka lifunza [caterpillar] kula majani, na kutembelea tumbo ardhini na mtini tu[kuelekea kushoto au kulia tu] kufa kuwekwa kwenye jeneza[buu] hadi kuwa kakipepeo kufyonza nekta tamu na kupaa angani[kuelekea kushoto, kulia, juu, chini, kujongea kushoto-chini, kushoto-juu, kulia-chini na kulia juu au ku hover palepale maybe!] kuvuka mito na kuishi popote na kuvinjari almost msitu wote. There is season and purpose thereof.
Tuna shida moja tu hapa: Mungu inafahamika ni hana mwisho[infinity] na vyote tulivyonavyo duniani vina mwisho [finite] hivyo hakuna mfano hata mmoja utakaoshibisha picha kamili ya Mungu. Hilo wote tunakubaliana. Mifano tunayotoa inajaribu kugusia sifa chache za ukuu wake, ni analojia zisizo kamili. Mfano wa mwili na seli zake umetumika kuonesha kuwa kuna kusudi jema katika maumivu yetu na umeelezea vizuri hilo, that is all.
Imani ni kitu binafsi hatuwezi kuwa na imani moja kwa sababu ni watu tofauti.Imani ingekuwa uhalisia basi leo kungekuwa na imani moja
Since kuna buch la imani tena zinazopingana huo ni uthibitisho imani ni ujinga tu
Hata wewe hukubaliani na imani nyingi, kwanini usikubaliane nazo kama imani ni uhalisia?
Tuna record nyingi za watu kuamini uwongo na mwisho wa siku imani hizo leo hii zinatambulika kama ni ujinga baada ya kuwa debunked
Jema kwa wahusika woooote waliotajwa kwenye aya ya kwanza hapo post #689Kuumwa tumbo ni jambo jema kwa nani?
Watu wengi hawaelewi kuhusu haya mambo, katika nguzo sita za imani ya kiislam, kuna nguzo ya mwisho inaitwa kuamini Qadar (makadirio ya ALLAH) kuwa heri na shari vyote vinatokana na Qadar yake ALLAH (Mungu).Upo vizuri sana, hivyo ndivyo ilivyo
Mkuu nikusahihishe tu kuwa hakuna kinachofichikana kwa MUNGU.Iwe ni mdudu mdogo aliye ndani ya udongo au hata ndege aliyepo angani ..vyote ana viona. Moja ya jina ktk majina yake Mwenyezi Mungu linaitwa "MWENYE KUONA" anaona kila kitu kiwe kikubwa ama kidogo hakuna kinachofichikana kwake.We live in the universe of 'duality'
Good|bad, juu|chini, kulia|kushoto, ukweli|uongo
MUNGU | SHETANI
Ili ulimwengu uwe balanced ilibidi MUNGU amuumbe shetani
Kosa kubwa watu hufanya kwenye majadiliano yahusuyo Imani ni kuuliza swali la MUNGU ni Nani badala ya MUNGU ni nini? Na ndicho kinachojadiliwa hapa
Kwanza kabisa tujiulize MUNGU ni nini?
Nikupe mfano huu,
MUNGU katika kusudi lake la milele kabla hajamuumba binadamu aliuliza HAKI,KWELI NA HURUMA endapo ni vema wamuumbe binadamu au lah
Haki akajibu "usimuumbe binadamu Kwa kuwa atazivunja Sheria na kanuni zako zote"
Kweli akajibu "usimuumbe Kwa kuwa binadamu atakuwa mbaya na daima atatafuta uwongo na hila( udanganyifu)
Huruma akajibu "ninajua mwanadamu atakuwa mbaya Sana lakini Mimi nitamuhifandhi na kutembea naye katika njia zake za Giza mpaka mwishowe nitamrejesha kwako"
Umejifunza nini hapa mkuu kuhusu free will mkuu?
Kuna tofauti Kati ya dhambi na nakosa.Ukifanya dhambi MUNGU hawezi kukuona maana ni mtakatikfu ,ndy maana Adam alipokula tunda, MUNGU hakumuona Adam ndy maana akauliza "Adam uko wapi"
Naamini sasa utakuwa umenielewa kwa nini nilijiuliza lile swali lililokuvunja mbavuSynonym alishalimaliza hili suala, alisema kuna matendo ambayo mtu atahukumiwa nayo na mengine hatahukumiwa nayo. Nakubali uwepo wa hizo 'ajali' mda mwingine lakini siwezi kuuweka mustakabali wa maisha yote chini ya mambo tusiyoyaendesha sisi kama sisi. Zipo chaguzi nyingi tu za kuitikia hizo unazoziita 'ajali' na zipo chini ya utashihuru wako -FREEWILL
Kaka zipo hatua za kun'gamua na kubeba majukumu na kadri unavyokuwa na majukumu zaidi ndio unazidi kuwa na uwezo zaidi. Na uwezo ni simply uamrishaji wa will yako, hivyo ni uhuru zaidi:View attachment 2252383
Ewaaaah! kumbe sasa umenielewesha vizuri zaidi. Inaonesha kuwa walio kinyume na free-will in essence hawataki tu kuyakabili majukumu ya kiutu, au ya kiutu-uzima.Naamini sasa utakuwa umenielewa kwa nini nilijiuliza lile swali lililokuvunja mbavu
Nakazia: Watu eidha hawajui tofauti au wanashindwa kuoanisha kwa usahihi au wanachanganya;
1. Prescience 'Foreknowledge'
2. Devine will and decree 'Mipango/Matakwa na Makadirio'' na
3. Free will
Ndo maana unaona mtu anauliza kwa nini hakupewa nafasi ya kuchagua kuwepo au kutokuwepo duniani hata kabla hajaumbwa?
"And your Lord creates whatsoever/whomsoever He wills and chooses" Al-Qasas, verse no. 68
Au mtu ahoji nafasi ya kijusi katika kuchagua kuzaliwa au kutokuzaliwa? [emoji23]
Hivi kijusi kina akili tambuzi? Hivi kijusi kinaweza kutofautisha kati ya jema na zuri? Hivi kijusi kinaweza kutenda kwa kutaka kwa mfano: kula au kutokula? Kwa minajili hiyo kijusi kina utashi huru? Kwa werevu mtakuwa mmeshang'amua
"It is He who shapes/forms you in the wombs of your mothers however/as He wills" Al-Imraan, verse no. 6
Hivyo, asome na ajifunze kutofautisha kati ya hivi
1. Vitendo vya mja na vitendo vya Mungu
2. Vitendo vya hiari au kutaka na vitendo visivyo vya hiari au kutokutaka
Nijazie nyama kidogo ndugu yangu ni kuwa kila unaemuona ni binadamu awe alishaishi ktk dunia hii,anaishi ktk dunia hii au atakuja kuishi ktk dunia hii jua kuwa alikubali kuumbwa kuwa binadamu na alikubali kuibeba amana ya Mola wake.Naamini sasa utakuwa umenielewa kwa nini nilijiuliza lile swali lililokuvunja mbavu
Nakazia: Watu eidha hawajui tofauti au wanashindwa kuoanisha kwa usahihi au wanachanganya;
1. Prescience 'Foreknowledge'
2. Devine will and decree 'Mipango/Matakwa na Makadirio'' na
3. Free will
Ndo maana unaona mtu anauliza kwa nini hakupewa nafasi ya kuchagua kuwepo au kutokuwepo duniani hata kabla hajaumbwa?
"And your Lord creates whatsoever/whomsoever He wills and chooses" Al-Qasas, verse no. 68
Au mtu ahoji nafasi ya kijusi katika kuchagua kuzaliwa au kutokuzaliwa? [emoji23]
Hivi kijusi kina akili tambuzi? Hivi kijusi kinaweza kutofautisha kati ya jema na zuri? Hivi kijusi kinaweza kutenda kwa kutaka kwa mfano: kula au kutokula? Kwa minajili hiyo kijusi kina utashi huru? Kwa werevu mtakuwa mmeshang'amua
"It is He who shapes/forms you in the wombs of your mothers however/as He wills" Al-Imraan, verse no. 6
Hivyo, asome na ajifunze kutofautisha kati ya hivi
1. Vitendo vya mja na vitendo vya Mungu
2. Vitendo vya hiari au kutaka na vitendo visivyo vya hiari au kutokutaka
Tatizo wanaadamu tunajisahaulisha kwa makusudi kuwa hatukukubali kuibeba amanah ya MUNGU. Wanaadamu tulikubali wenyewe kuwa tutafata maamrisho ya Mungu hapa duniani na kuyaacha makatazo yake na tulikubali kuwa atakayefata aliyoyaamrisha Mungu atapewa malipo mazuri na atakayeyaacha ataadhibiwa vikali. Haya tuliyakubali kwa mikono yetu miwili kuyabeba licha ya sisi kuwa ni dhaifu na ni wenye kujidhulumu nafsi zetu.Ewaaaah! kumbe sasa umenielewesha vizuri zaidi. Inaonesha kuwa walio kinyume na free-will in essence hawataki tu kuyakabili majukumu ya kiutu, au ya kiutu-uzima.
Kwa nini wajifananishe na katoto ambako bado hakana utashi huru? Helpless
Ndio maana wanataka hadi wapewe maarifa yote bila kuyatafuta, watatuliwe matatizo yao yote na Mungu bila wao kufanya chochote. Eti ndio wamuamini
Wanajiona watoto wasio na maamuzi wala majukumu badala ya kujiona ni wana wenye majukumu na maamuzi pia.
Unapostulate mambo bila ushahidi wala kuonesha mambo logically, kwa wishful thinking tu.Kuhusu suala la fact vs imani unajidanganya. Hata fact tunavyoiona inatofautiana kutokana na 'imani' ya anayeitazama hiyo fact.
Fact inaweza kuwa ni homa au maumivu lakini kwenye kusema ni kitu kiovu au ni kitu chema itategemea na imani zetu. Mimi nikipata homa labda naamini ni mwili wangu unanisaidia kupambana na virusi hivyo ninaishi - Purpose is good.
Hapa nimetumia neno imani kama namna tunavyochukulia kuwa ukweli wa mambo ndivyo ulivyo yaani uhalisia. Kwa kusema hivyo the problem of evil ni sababu moja zaidi ya kumuondoa Mungu mwenye upendo katika dunia yako, wakati ni sababu moja zaidi ya kumuona Mungu mwenye upendo katika dunia yangu. Inatokana na imani/uhalisia wetu binafsi.
Katika dunia isiyo na kusudi everything can be evil, lakini katika dunia yenye kusudi EVERYTHING IS GOOD. We are surrounded with overabundance of goodness which we will keep realizing over time. Chooing to be the side of evil or good is your choice to make. FREEWILL
Nilishalitolea analojia ya mwili hili. #637
Mungu wako, dhana ya kuwapo kwake na kuwapo kwa ulimwengu huu ina logical inconsistency.Kwangu mimi nitatumia yote ninayoyajua hadi hivi sasa na nitaamini katika yale ambayo bado sijayathibitisha nitatumia trust na faith kukamilisha ambacho knowledge imebakiza. Kama nikipata data ikathibitisha kinyume labda ntaacha, ila siachi nisikudanganye kwa ninachokijua hadi sasa hivi sisi ni wa Mungu tu bro hamna namna🤦♂️. Ndo maana walokole wanasemaga NIMEOKOKAA
Kwa suala la ukatibu mkuu wa UN siwezi kuendelea nalo maana hakuna knowledge inayosapoti hivyo, na kuna vitu tayari vinaniprovia kwamba hicho kitu ni wrong. Mfano:sijawahi hata kupanda ndege[labda hii chukulia ni prerequiste]
Kwa nini hutamini?Hapana sitaamini
Anaviona.... Kuona ni tendo lenye mchakato/hatua, JE, KWANINI MUNGU ALAZIMIKE KUCHAKATA KATIKA NYENDO ZAKE?Mkuu nikusahihishe tu kuwa hakuna kinachofichikana kwa MUNGU.Iwe ni mdudu mdogo aliye ndani ya udongo au hata ndege aliyepo angani ..vyote ana viona.
Kwanini isiwe CHENYE/PENYE/LENYE/YENYE nk.... Kwanini Dhana Mungu iko personalised? Je, hamuoni kuwa hilo ndilo linalokaribisha Udhaifu na mapungufu mengi juu ya Mungu?Moja ya jina ktk majina yake Mwenyezi Mungu linaitwa "MWENYE KUONA" anaona kila kitu kiwe kikubwa ama kidogo hakuna kinachofichikana kwake.
Hivyo kuwaonya alikuwa anajua kuwa nibkupoteza muda tu, na bado akafanya?Kitendo cha Adam na Mkewe ,bi Hawa kula tunda la mti waliokatazwa ,tayari Mungu alishajua na infact alishajua kabla hawajala kuwa watakuja tu kula.
Hata Leo hii, huwezi kutoa vitisho vya kinyago kinachotisha kwa mtoto kipofu, ilikuwaje atishie watu ambao alikuwa anajua 100% hawatamsikiliza?Alilitambua hili na aliwaonya mapema kuwa wasile maana wakila watavuna matokeo yake.
Unapaswa usemee hiyo maana sasa, Kwanini atumie Tashititi, ili iwe nini?Kitendo cha Mungu kusema upo wapi ewe Adam hakikuwa na maana kuwa hakujua Adam alipojificha laa hasha . Ni sawa na pale alipomuuliza Musa umeshika nini mkononi mwako ewe Musa .Musa akamjibu kuwa nimeshika fimbo. Sio kwamba alikuwa hajui au hamuoni Musa kuwa ameshika fimbo. Kilugha tunaita ni rhetoric question! Ni swali unauliza ukiwa huna lengo la kupata jibu lake, kwani tayari wewe muulizaji unajua jibu lake.
Tulikubalije? Hiyo amanah nini hasa? Na kwanini tuwajibike kumbebea Mungu, kwanini asibebe mwenyewe?Tatizo wanaadamu tunajisahaulisha kwa makusudi kuwa hatukukubali kuibeba amanah ya MUNGU.
Makubaliano hayo yalifanyikaje?Wanaadamu tulikubali wenyewe kuwa tutafata maamrisho ya Mungu hapa duniani na kuyaacha makatazo yake na tulikubali kuwa atakayefata aliyoyaamrisha Mungu atapewa malipo mazuri na atakayeyaacha ataadhibiwa vikali. Haya tuliyakubali kwa mikono yetu miwili kuyabeba licha ya sisi kuwa ni dhaifu na ni wenye kujidhulumu nafsi zetu.
Usibebe kila dhana uzisikiazo kwenye Hekaya na Masimulizi ya Kiimani.Mbingu, Ardhi na milima, wanyama ,wadudu ,ndege wote walikataa kuibeba hiyo amanah ila sisi na majini tulikubali kuibeba!!!
FreeWill ni Kiini Macho, hakijawahi kuwepo kokote.Na ndio hapo tukapewa FREE WILL (to do or not to do). Ila hivyo viumbe vingine vyote havikupewa huu upendeleo wa free will.
Aje kama hicho kiitwacho kuwa LOGIC ndio hichohicho kiitwacho kuwa MUNGU?Mungu wako umemtengeneza mwenyewe kichwani halafu umemrusha vikwazo vyote in "a priori" way.
Ama unakubali logic, ama hukubali.
Ukikubali logic, Mungu wako hayupo, kwa sababu dhana ya kuwapo kwake ina logical inconsistency.
Ukikataa logic, Mungu wako hayupo, kwa sababu ulimwengu usiofuata logic haumuhitaji Mungu.
Popote utakapokwenda, unakuta Mungu hayupo.
Kwa sababu, Mungu huyo hayupo.
Knowledge, mambo ninayofahamu na sheria za kuaminika zimeonesha hicho kitu hakipo pembetatu ni pembetatu na duara ni duara sijaonaga hata hint ya kuwepo pembetatuduara katika ujuzi wangu ninaoufahamu kwa maumbo bapa hadi sasa. Na sina haja ya kutegemea maajabu maana naamini hiyo eucledian geometry unayoisema ina mipaka ya bapa tu.Kwa nini hutamini?
Safi sana kwa kukazia hili, hata mimi nilionelea labda tujaribu kutumia kile kitu anakikubali zaidi. LOGIC, LOGOS, NENO.Aje kama hicho kiitwacho kuwa LOGIC ndio hichohicho kiitwacho kuwa MUNGU?
JE, BADO HAKITAKUWEPO?
Mungu ni Ukamilifu wa Hesabu wa Uwepo ama Kutokuwepo kwa jambo au kitu chochote. Nayo ndiyo Logic.
Anhaa kumbe wewe unaposema ni LOGIC unataka kuiacha kama tu entity fulani hewani.Kosa ni kupersonalize Mungu.