Kuumwa tumbo ni kusudi jema kwa hiyo being nzima, kuanzia mtu [kama consciousness ya mtu], mtu kama mwili wa mtu, na hizo seli za tumbo na hata seli zote za mwili wa huyo mtu......... in fact ni chema kwa mke/mme wa huyo mtu, familia ya huyo mtu, jamii na taifa na dunia kwa ujumla. WHY? Tumbo linapouma tunakuwa na taarifa wote kwamba kuna kitu hakiko sawa na juhudi zinafanyika tunarudisha AFYA kwa mtu husika ambaye uwepo wake ni faida kwa wote.
Sisi ni finite, I mean miili yetu ina mwisho na hata hilo jambo la miili yetu kuisha ina kusudi jema pia🤭. Purely materialist kuelewa hilo labda chukulia metamofosisi za kipepeo. Kutoka lifunza [caterpillar] kula majani, na kutembelea tumbo ardhini na mtini tu[kuelekea kushoto au kulia tu] kufa kuwekwa kwenye jeneza[buu] hadi kuwa kakipepeo kufyonza nekta tamu na kupaa angani[kuelekea kushoto, kulia, juu, chini, kujongea kushoto-chini, kushoto-juu, kulia-chini na kulia juu au ku hover palepale maybe!] kuvuka mito na kuishi popote na kuvinjari almost msitu wote. There is season and purpose thereof.
Tuna shida moja tu hapa: Mungu inafahamika ni hana mwisho[infinity] na vyote tulivyonavyo duniani vina mwisho [finite] hivyo hakuna mfano hata mmoja utakaoshibisha picha kamili ya Mungu. Hilo wote tunakubaliana. Mifano tunayotoa inajaribu kugusia sifa chache za ukuu wake, ni analojia zisizo kamili. Mfano wa mwili na seli zake umetumika kuonesha kuwa kuna kusudi jema katika maumivu yetu na umeelezea vizuri hilo, that is all.