God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Jambo kuwa binafsi ni swala lingine na jambo kuwa ukweli ni swala lingine

Usifanye ionekane kuwa jambo ambalo linadaiwa kuwa lakibinafsi haliwezekani kujua ni la kweli au lah

Au kufanya jambo hilo likubaliwe kwa dhana ya ukweli kwakua tu limedaiwa ni jambo binafsi

Uwongo wowote unaweza ukalindwa kwa mgongo huo
 
Aje kama hicho kiitwacho kuwa LOGIC ndio hichohicho kiitwacho kuwa MUNGU?

JE, BADO HAKITAKUWEPO?

Mungu ni Ukamilifu wa Hesabu wa Uwepo ama Kutokuwepo kwa jambo au kitu chochote. Nayo ndiyo Logic.
Tunaongelea Mungu specific, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Logic haina upendo.
 
Anhaa kumbe wewe unaposema ni LOGIC unataka kuiacha kama tu entity fulani hewani.
Mungu si Kitu, Bali ni Kila Kitu. Ndivyo ilivyo kwa Logic, nayo ni KILA KITU.

Ni Ukamilifu wa Kutokea ama Kutotokea kwa jambo iwe jema au bays, kesho au Leo, hapa au pale...Logic.

Kila kitu kipo vile kilivyo kwasababu ya Ukamilifu wa Kuwa vile kilivyo.
Hapana. Kumpersonalize Mungu ni jambo jema labda kumuanthropormorphize ndio haifai.
Ni kwa namna gani unaweza kupersonalize Mungu pasipo kufanya anthropomorphic?

Kilicho nje ya Hisia zote ndicho kiitwacho Mungu/Ukamilifu. Sasa unawezaje kuvika Hisia kwa kitu na bado kikabaki kuwa Kikamilifu?
Mungu ni personal katika uhusiano wake na uumbaji wake kabisa japo sio anthropormorphic.
Ndio maana ufafanuzi wake hukanganya wengi, Kosa linaanzia hapo.
 
Nakuuliza kwenye Euclidean planes, unajibu kwenye dimensions zaidi? Kwa nini?

Mungu wako kuwepo ni sawa na pembetatu duara kuwapo katika Euclidean planes.

Both have contradictions.
 
Thibitisha Mungu yupo, usiseme tu logic ni sifa ya Mungu.
 
Tunaongelea Mungu specific, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Ukishasema MWENYE.... Basi kwa Hakika HAJAWAHI KUWEPO.
Logic haina upendo.
Ni kweli, haina, maana yenyewe ndio huo Upendo Wenyewe, ndio hiyo Chuki Yenyewe, ndio hicho Kisasi Chenyewe, ndiyo hiyo Huruma yenyewe.... NI KILA KITU/Mungu.
 
Nakuuliza kwenye Euclidean planes, unajibu kwenye dimensions zaidi? Kwa nini?

Mungu wako kuwepo ni sawa na pembetatu duara kuwapo katika Euclidean planes.

Both have contradictions.
Nimejibu kwa sura zote mbona, kuna contradiction kwenye planes n kama huo ndio uhalisia pekee basi haiwezekni, lakini kama huo sio uhalisia pekee mbona ni kitu kipo kabisa.

So, Mungu kuwepo kwenye material pekee[plane] haiwezekani ila katika uhalisia wenye kujumuisha hadi spiritual Yupo kabisa na ili kumuona kwa sisi tutageuzageuza hayahaya material na kuziona kweli zote za material na spiritual. Hata kama kuna hizo ulizokazania kuwa 'evil' tutaziona na kuzielewa kama vizuri tu. There is no contradiction
 
Ukishasema MWENYE.... Basi kwa Hakika HAJAWAHI KUWEPO.

Ni kweli, haina, maana yenyewe ndio huo Upendo Wenyewe, ndio hiyo Chuki Yenyewe, ndio hicho Kisasi Chenyewe, ndiyo hiyo Huruma yenyewe.... NI KILA KITU/Mungu.
Unajuaje hilo ni kweli na si habari ulizojiaminisha tu?
 
Kwani nani kasema Mungu yupo kwenye material pekee?

Unaelewa hata analogy yangu?
 
Basi kasome relativity ili tuwe tunakubaliana na fact ndio tuendelee kubishana kwenye uhalisia.

Kaka upo uwezekano wa mimi kusema nimekaa dakika tano tangu ulipoondoka, na huyo aliyeondoka akasisitiza nimekaa miaka saba tangu tumeonana mara ya mwisho na wote wakawa wanasema kweli! Umri wao na kila kitu chao ni kweli kabisa na kila mmoja akauishi uhalisia wake
 
Ukishasema MWENYE.... Basi kwa Hakika HAJAWAHI KUWEPO.

Ni kweli, haina, maana yenyewe ndio huo Upendo Wenyewe, ndio hiyo Chuki Yenyewe, ndio hicho Kisasi Chenyewe, ndiyo hiyo Huruma yenyewe.... NI KILA KITU/Mungu.
Logic haina upendo wala si upendo.
 
Kwani nani kasema Mungu yupo kwenye material pekee?

Unaelewa hata analogy yangu?
Kwani nani kasema hivyo?

Analogi yako imeonesha contradictio ya logic ndani ya premise [mipaka] fulani, jibu langu limekubali hicho kitu kabisa kabisa na kuongezaa kuwa uhalisia ukiongozeka premise[mipaka] inatanuka na mabo yanawezekanika kiulaini kabisa. Na ndio UKWELI ulivyo. Bado unahisi sijaelewa?
 
Ni kwa namna gani unaweza kupersonalize Mungu pasipo kufanya anthropomorphic?

Kilicho nje ya Hisia zote ndicho kiitwacho Mungu/Ukamilifu. Sasa unawezaje kuvika Hisia kwa kitu na bado kikabaki kuwa Kikamilifu?
Ni swali tata kwa kweli majibu yake ni ya kutafuta karibu tu;

Kama unakubali kuwa Mungu ni Upendo huoni kama hiyo ni personal attribute.? au hili wewe hulikubali?

Ndiyo maana kurahisisha mimi hutumia maneno kama Mungu ana upendo na ndio UPENDO wenyewe, au Mungu anatumia Logic na ndio LOGIC yenyewe. So nakubali sifa zake za kuwa na sifa na kuwa sifa zenyewe maana ni kila kitu. Ameumba kila kitu na ndio kila kitu.

Sawa tu na mtu anayesema kuwa Mungu yupo mbinguni na pia Mungu yupo mahali pote. Hapo unatuambiaje?

Ukikataa sitakulazimisha ila endelea kujifunza maana ndio kazi yetu katika maisha yetu, hata mimi najifunza
 
Ni swali tata kwa kweli majibu yake ni ya kutafuta karibu tu;

Kama unakubali kuwa Mungu ni Upendo huoni kama hiyo ni personal attribute.? au hili wewe hulikubali?
Kwangu Mungu ni Ukamilifu wa Kuwepo ama Kutokuwepo. Huo Ukamilifu Si Kitu, Bali ni Kila Kitu na Kila hali. NI KILA KITU.
Ndiyo maana kurahisisha mimi hutumia maneno kama Mungu ana upendo na ndio UPENDO wenyewe, au Mungu anatumia Logic na ndio LOGIC yenyewe.
Hayo ni mazoea Yetu wengi, lakini kwa bahati mbaya yamekuwa hatarishi mno kwa walio wengi.
So nakubali sifa zake za kuwa na sifa na kuwa sifa zenyewe maana ni kila kitu. Ameumba kila kitu na ndio kila kitu.
Shida IPO kwa utakaowaambia hayo... Na ndio Upotoshaji na hoja ngumu zinapozinapozaliwa. Watu wengi hubeba hilo na kuchukulia Mungu sawa na Dubwana Fulani lenye sifa nzurinzuri za kibinadamu zilizokuwa exaggerated.
Sawa tu na mtu anayesema kuwa Mungu yupo mbinguni na pia Mungu yupo mahali pote. Hapo unatuambiaje?
Kwanini haYUpo? Aje kama tutasema haipo hapa wala pale maana ndio Uwepo wenyewe.
Ukikataa sitakulazimisha ila endelea kujifunza maana ndio kazi yetu katika maisha yetu, hata mimi najifunza
Ndicho tufanyacho hicho Mkuu. Tujifunze Tusichoke. Ila ni vema kutochagua upande kabla hujaondoa utata wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…