Gone Too Soon: RIP JF Member.....Chetuntu!!!

Mungu ailaze roho ya marehemu dada yetu mahala pema peponi. Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Duh!............ R.I.P Chetuntu. Nakumbuka nilimpokea jukwaa la utambulisho.
 
Duh!............ R.I.P Chetuntu. Nakumbuka nilimpokea jukwaa la utambulisho.

tena wewe ndiye uliyekuwa wa kwanza kabisa kumfungulia mlango alipobisha hodi hapa JF, its sooooo touching!!

raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanaga wa milele umuangazie apumzike kwa amani, Amina!

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe!
 
RIP Chetuntu! Bwana ametoa na Bwana ametwaa,na apumzike kwa Amani Bwana.
 
Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani. Aaaamen!
 


Yaani nimeshtuka utadhani namfahamu moja kwa moja.
 
Mungu ailaze roho y marehemu mahala pema peponi....Amen
dunia tunapita, kila mtu njia yake ni hiyo moja tu, poleni wafiwa
 
Ninaloweza kusema ni kuwa NIMESHTUKA!
Nikiiona avatar yake na picha ni kama namfahamu, sijui nilimwonaga wapi huyu mdada !
Dadaangu mpendwa, kapumzike kwa amani...Kazi uliyofanya yatosha!
Raha ya milele umpe eebwana na mwanga wa milele umwangazie!

Naomba nimuimbie Chetuntu(rip) wimbo huu:

Si mbali safari, siku nyingi
Kuaga dunia kutazama juu,
Vinanda vyalia kwa sauti tamu
Malaika waimba kumsifu Mungu.

Lango la dhahabu linafunguka.
Mwanga wa
milele unamulika.

etc etc...Asprin anaweza kuendeleza nimesahau mashairi mengineyo!
 
Nakuunga mkono mkuu, mkifanikiwa mtujuze hata kwa pm ili na sie tuchangie
 
Nakuunga mkono mkuu, mkifanikiwa mtujuze hata kwa pm ili na sie tuchangie

....Dadangu Moderators wameificha thread kule kwenye Msiba wa Zanzibar, sijui wamehusianisha vipi haya matukio mawili, so members wengi wameshindwa kuiona ile thread kwa sababu imefichwa kule.....pengine Moderators hawajapenda wazo lile? to me it was better wangeidelete tu kuliko kuipeleka kusikohusika......!
 
duh!
Poleni sana wafiwa.
Mungu aliyemjua tangu tumboni mwa mama yake, ampe heri kwa kadiri ya matakwa yake.
Upendo wake ukawe mwanga kwa waliobaki.
Mwanae akapate kukua katika uchaji wa Mungu.
 
Maisha mengi yanapotea mapema siku hizi ... Kazi ya Mola haina makosa... Pumzika kwa AMANI Chetuntu...
 

...inawezekana ni makosa ya kibinadamu tu, nashauri ui report thread hiyo ili ifanyiwe kazi/marekebisho.
tuwe wastahmilivu katika kipindi hiki kizito kwa misiba ya taifa hao wahanga wa ajali ya meli, na
mwenzetu chetentu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…