Gone Too Soon: RIP JF Member.....Chetuntu!!!

Gone Too Soon: RIP JF Member.....Chetuntu!!!

Hili linaumiza sana...Kwetu ambao umri umeshaenda...Ni bora Mungu kama akiamua basi tutangulie sie kama tulivyokuja mapema....

Hii biashara ya kutanguliza wajukuu na watoto ni ngumu sana kuibeba katika akili na feelings za kibinadamu!

Tuzidi kuomba tena sana!
Mzee mwenzangu uliyosema ni sahihi kabisa. Inasikitisha na kufedhehesha kuona nguvu kazi ya taifa inapotea mapema namna hii.

Hivi anayechukua uhai wa binadamu katika umri mdogo namna hii, Ni Mungu?
 
Pole zangu kwa ndugu, jamaa, marafiki na hususani mwanae alie muacha bado mdogo na mhitaji wa upendo, matunzo na malezi ya mama yake.... RIP Chetuntu........
 
Apumzike kwa Amani dada yetu...

Mungu awape nguvu ya kukubaliana na hali halisi ili maisha yaendelee, hasa kwa Mwanao wa pekee.
 
Ng'ang'ana sana kwenye maombi na BWANA atakuokoa kwani KIFO si mpango wake ni mpango wa yule mwovu, Shetani.
Mkuu unataka kutuambia kuwa Shetani ndo hupanga vifo na wala si Mungu?............. Na kwanini Mungu amuache shetani apange kuteketeza viumbe vyake? Si amwangamize?...This is unfair!
 
Msiba mkubwa JF na zaidi kwa familia ya marehemu hasa mtoto,Aspirin tufikishie pole zetu kwa wafiwa waambie tulimpenda na tutam-miss sana.
 
bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
 
Poleni sana wana JF na salamu zangu ziwafikie wanafamilia wote. Hivi hatuwezi pata jinsi ya kutuma rambi rambi say kwa VODA/TIGO pesa.

R.I.P Chetuntu
 
umeijuaje ID yake?? au mnaukaribu?? maana wana JF wengi tunapishana mtaani lakini hatujuani....RIP chatuntu
 
Mkuu unataka kutuambia kuwa Shetani ndo hupanga vifo na wala si Mungu?............. Na kwanini Mungu amuache shetani apange kuteketeza viumbe vyake? Si amwangamize?...This is unfair!
shetani ndo ana run dunia
 
Ng'ang'ana sana kwenye maombi na BWANA atakuokoa kwani KIFO si mpango wake ni mpango wa yule mwovu, Shetani.
Wewe wa wapi ? hebu usichafue hali ya hewa hapa. Afadhali hata ungesema baada ya kifo kuna maisha mengine huko mbinguni,Shetani hana mamlaka kwenye mambo ya kifo,kazi yake ni kujaribu kukupoteza njia ukiwa hai.
 
Babu....anyway will call you again later.....! lakini hii kitu imenigusa mnooooooo! siku ya leo haiendi kabisa! Sasa what the least we can do for her to show our sympathy babu? Bangolize her...TBC? She got a young boy, tunajua hatima ya huyo dogo? kama hatima yake iko mashakani can we do something for this boy in memory of our loved one....something small but memorable....open a junior account...put in some money for her future?

Takukupigia tena on this mkuu.....!
 
Mungu aipe familia na wote walio karibu nguvu kipindi hiki kigumu

am so sorry kwa dogo, maisha bila mama kwa umri wake very bad
 
Back
Top Bottom