Katika eneo la Gongo la Mboto, kituo cha magari yanayoenda mjini kinachoitwa Maliasili, kuna yard ya magari ya mwendo kasi. Kumekuwa na tatizo la maji ya DAWASA kuvuja na kutiririka katika eneo hilo.
Maji hayo yameendelea kutiririka kwa takribani mwezi mmoja, huku yakielekea hadi eneo la makaburi. Cha kusikitisha, licha ya wahusika wa DAWASA kufika na kuliona tatizo hilo, hadi sasa hakuna hatua madhubuti iliyochukuliwa kulitatua.
Tunaomba DAWASA ichukue hatua za haraka kurekebisha uvujaji huo ili kuzuia uharibifu wa mazingira na usumbufu kwa wananchi.