Wakuu.
Google Maps kila mtu anaitumia. Mfano unaenda Kilosa, unataka ujue wapi utalala au utakunywa bia au ofisi flani ipo wapi bila kuuliza wenyeji, Google Maps anakusaidia.
View attachment 3480370
Pia kupitia Maps, unaona reviews mbalimbali katika iyo sehemu, ambazo zinatolewa na wateja au watu waliowahi kutembelea, kwa mfumo wa nyota (out of 5 stars) na maneno yakisuportiwa na picha na video.
Sasa mtu yoyote mwenye account ya Google na App ya Google Maps anaweza kutoa izo review. Na ukianza tu kutoa unakua Local Guide.
View attachment 3480369
Kua Local Guide hakuna faida yoyote. Zaidi ya kuwasaidia wengine. Local Guide ina level 1 hadi 10. Unapanda level kutokana na michango yako. Level za mwanzo 1 hadi 5 ni rahisi ila level 6 kwenda mbele zinahitaji points nyingi.
View attachment 3480366
Kwa upande wangu imekua addiction. Kila sehemu nikienda uwa naacha review. Najitahidi kua honest ili ije msaidia mwingine.
Nakumbuka kuna restaurant tulienda na mama mjengo ina jina kubwa. Tukaacha review negative. Walitupa huduma mbaya na msosi haukua mzuri. Waliangaika sana hadi walinipata kwa simu (kwa sababu nilipiga simu kuuliza chakula before sijafika, na jina kwenye review linafanana na niliosajiri namba). Waliomba niedit review watanipa free treatment next time nikasema poa. Niliogopa sana so nikaedit to ila sijaenda tena.
Next time na we ukienda bar, beach, restaurant, lodge, hotel, park au ofisi ya serikali au private, unaweza kuacha review. Ila jitahidi kua honest. Inaweza kumsaidia mtu anavyotafuta mahal pa kupata huduma.
Weekend post. No hard feelings.