Google pixel zina tatizo la kujizima ghafla?

Google pixel zina tatizo la kujizima ghafla?

Wakuu habari zenu,

Nimekuja kwenye hili jukwaa lengo ni kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na watu wenye uzoefu na hizi simu za Google pixel.

Nimejichanga nimepata hela kidogo, nataka ninunue google pixel 5a kutokana na specs zake
Ila kuna jamaa yangu Kariakoo anaziuza hizi simu ila kanipa tahadhari kuwa hizi simu siku za karibuni kapokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja wake, simu kujizima tuu ghafla, kitu kinachopelekea kuanza kupoteza soko.

Sasa narudi kwenu wanajukwaa hilo tatizo ni common kwa hizi simu? Na linasababishwa na nini?

Nimeanza kupata wasiwasi nafikiria nichukue brand nyingine.
Kumbe ni ishu sugu, nilidhani kwangu tu....ntajarbu kukuwekea ushahidi hapa uone, hizi simu sio. Bora samsung au iphone tu, picha ndio kali ila hazdumu sjui ndio hvo kisa second hand au vipi
 
Simu zote za Android ni majanga Mzee , huwa zina mauza uza kibao ndani ya safari...!! Ads nyingi , mara izime , mara istack , mara ichemke yaan full disturbing
Simu yoyote inaweza kuwa na mauzauza...iphone 15 ina mauzauza ya heating problems...poor backglass durability...achana na mawazo ya ki-isheep.
 
Me Pixel yangu 5a ilizima ghafla tuu ...nlikua nimeitumia miezi mitatu tuu.... 450k ikawa ndo imepotea hivo

Refurbished phones ni majanga
 
Kwa ushauri wangu kanunue INFINIX, Dereva wetu anayo tangu 2020 na bado inadunda sema Kuna wakati Ina stuck.
Halafu Bei yake Ni pocket friendly, hakikisha tu unanunua kwenye duka lao upate original.
Very durable.
 
Ndgu sina hoja za kitaalam juu ya simu hizi ila nilichoona kwa dogo wangu alinunua zaidi ya tatu na zikamfia mkononi maana mwanzo alichukua used akasema labda tatizo nimechukua simu ya kutumika ikabidi azame shop kwa maelezo yake ila naona kwa hizi zote tatu zilizima gafla na haikuwezekanika kutengeneza amepeleka sehemu mbali mbali hola
Problem confirmed and discussion closed.
 
Back
Top Bottom