Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Ethiopians wameaza kubadilisha gia anganj, taratibu wanajisogeza kwa mchina. Mchina akileta dili Ethiopia anafungua milango yote, kampuni kubwa ya super market ya Marekani Walmart, walitaka kujingiza Ethiopia wakawakatalia. Tatizo waafrika hatujuwi nia ya wachina kukimbilia Afrika, wengine wanasema mchina anatafuta masoko ya baadae. Wengine wanasema mchina anawatafutia watu wake shehemu ya kuishi kwasababu huko China hawatoshi (1.3bn ppl). Wengine wanasema mchina anataka kujimilikisha rasilimali zote za duniani maana hata South America amesha jijaza huko. Wananunua mali nyingi za Europe na Canada mpaka Australia. So, hiyo ndio siri inabidi watu waitengue, kasi ya wamarekani inapungua sana. Wamarekani wamefikia mahali pale waingereza walikuwepo 1900's (fail of world kingdom), maybe the world needs another leadership, but inabidi waafrika tuanze kujitawala wenyewe, na hatuwezi kufanya hivyo tukiwa bado tunashindwa hata kuvumbuwa dawa zetu, silaha zetu au hata kuzalisha chakula cha kutosha sisi wenyewe.Hakuna siri yeyote mataifa ya Afrika.
Tungalikua na uwezo mkubwa wa kitekinolojia labda kungekuweko ahueni.
Leo hii tunaambiwa Mrusi amedukua siri za uchaguzi Marekani,haijulikani kulikoni lakini hawa wababe tu ndio wenye uwezo wa kuweka siri japo pia yaweza dukuliwa(HACKING).
Mhabeshi anatumia miundo mbinu zote na tekinolojia ya hawa wenzetu,ikiwa ni tarakilishi,simu ya mawasiliano,mashine ,mitambo ya kielektroniki,ndege na kadhalika kwahivyo hamna kitu kama siri hapo......kwa sisi bado sana mwenzangu.