GPA ya 5 - Anazurura mtaani; we are not serious!

GPA ya 5 - Anazurura mtaani; we are not serious!

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kwa mtazamo wangu tumechelewa kuwatumia wanafunzi wenye ufaulu wa juu (outstanding) kulisaidia taifa. Hivi inakuwaje mwanafunzi kidato cha sita ana point tatu, Chuo kikuu amepata GPA ya 4.8 au kwa wenzetu wa Arts wanapata hadi GPA 5 naye yupo mtaani hana ajira?
Labda niunganishe na wale wataalam wabobezi waliosimamia reseach kubwa kama mbegu za Mikorosho zinazo tumia miaka 25 kupata matokeo; mihogo nk nao tuna waacha tu wapotee eti kwa kuwa wamefikisha umri wa miaka 60?
Prof mmoja tulimuachia pale Naliendele baada ya kufikisha miaka 60 akachukuliwa na Nchi nyingine kuwa Mshauri wa Wizara ya kilimo nk nk nk
 
Leo nilikua namwambia kijana wangu kwamba.

Shule itampa maarifa, lakini kusoma hakumpi guarantee ya kufanikiwa.

Lakini nilimwambia kwamba.

Akishaipata elimu, atakua namaarifa. Ili afanikiwe anapaswa kuwa mwenye bidii na nidhamu
 
kwa Nchi za wenzetu ukisoma Chuo chenje jina ukapata hizo pass, huenda mbali na hata kupewa Uraia mashart nafuu ukitaka
Wengi wa watu wa hizo pass wapo very serious kwa chochote atakachofanya.
 
Nafikiri tumechelewa sana kujua umuhimu wa pass za juu katika kupaisha Taifa kiuchumi nk
Hivi inakuwaje mwanafunzi amemaliza Chuo amepata GPA ya 4.8 au kwa wenzetu wa Arts wanapata hadi GPA 5 naye yupo mtaani hana ajira?
Hizo GPA ya 5 mnapataje Nyie vitoto vya sasa? Unajua maana ya GPA 5 Points.

Maskini Tanzania! Ni ya chuo gani hiyo GPA?
 
GPA na kuyamudu maisha kitaa ni vitu viwili tofauti,Std seven anayamudu maisha,anakula vizuri,analala pazuri na hana GPA,maisha hayana formula

GPA na kuwa na kazi yenye maslahi mazuri ni vitu viwili tofauti,

GPA na ufanisi wa kazi vinaweza visioane,GPA kubwa kwenye application F

Ukiendekeza kuwaza ulivyofaulu vizuri chuoni au sekondari utakawia sana kutoboa
 
Jinsia ina umuhimu hapo, kama mwenye hiyo GPA ni mwanamke ujue RUSHWA YA NGONO ilihusika ndio waajiri hawaiheshimu sana. Tupambane sio lazima tuajiriwe..maisha yanaenda kwa kazi yeyote...lialia haisaidii
 
mambo yamebadilika sana; good background, more digital, more resources, kuliko enzi zetu
na chuo kutoa maksi za chini haimaanishi kuwa ndio chuo Bora; Pengine kina kosa vitu vingi; supportive katika kusoma na wawezeshaji dedicated
Nafahamu!
But GPA ya 5! Yaani kwamba tangu anaanza mwaka wa Kwanza Hadi anamaliza chuo mwaka wa tatu au wa nne, alikuwa akipata [emoji817]% Kwa masomo yake yote?

Au ni wale ukipata "A" iwe ya 80 au 90 basi hiyo ni GPA ya Tano?

I wonder!
 
Mtu anayepata GPA ya 4.8 kwenye chio chenye reputation hata ukisema amekariri ni kwamba ubongo wake una uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa.

Ataachwa ajipambanie,akishinda aanze kusemwa.
😂😂😂umenikumbusha mbali kipindi na mimi nimemaliza chuo nahustle hakuna aliekua na time na mimi,wote wenye uwezo wananicheki tu waone nitaishia wapi,wengine wananisikitikia eti kasoma lakini hana kazi,anadhurura mtaani,elimu haijamsaidia

Nimekuja kulamba shavu kwa juhudi zangu,mambo safi sasa naanza ona simu simu,mara naitwa kijana wetu,mara kaka.

Walikua na vijigari vyao,wamejenga vijumba wanajidai dai,nimewalipa mara mbili.

Binadamu ni wanafiki,nimechinjia wote baharini,wanabaki wanasema tu.ooh eti ninadharau 😂

Ulikua huna time na mimi,na mimi sina time na wewe

Sitakagi ujinga
 
Creativity and innovation matter most ,Elon musk kafika hapo alipo kwa kujiongeza computer hakufundishwa darasani na ndio imemfikisha alipo mm naamini kama uko serious GPA ni upuuzi tu kikubwa get right materials angalia upepo unaelekea wapi jitose ulingoni...
 
Back
Top Bottom