GPA zetu bongo kweli ni kizungumkuti

GPA zetu bongo kweli ni kizungumkuti

na bodi za wanazuoni kama nbaa, body ya procurement, body ya bank, body ya wakandarasi, chama cha wanasheria(tanganyika lawa society) watafanya nini?
Kumbuka hata kama una gpa ya 5.0 ili kutambulika na hizi body lazima ufanye mtihani wao.
Vyuo viendelee kutoa gpa hata kama mtu hajafanya mtihani, ila kuwe na body ktk kila fani ya kitaaluma ambayo itatoa mtihani wa jumla bila kujali chuo unachotoka(body zote nilizotaja zinafanya hivi)
ila pia kwa nacte vyuo vyote lazima vipeleke mitihani waliyoandaa ipimwe kama imekidhi viwango kabla haijafanywa, sina uhakika kama tcu wana hichi kitu.
Pia kulingana na kalenda ya vyuo huwezi kusema vyuo vyote vifanye mtihani mmoja, mfano kuna vyuo vimefanya UE may(tia, iaa etc) vingine june(udsm, duce,) na vingine ndo wanafanya nw (cbe, st John, ustawi)
unaset vip mtihani hapo?
Maadam kuna prof bodies acha waendelee ila watakapoletwa kwny body ndo tutajua gpa ya kupewa au kutafuta mwenyewe

Maoni yako naona yana afya maana hawa TCU wamejiweka zaidi kwenye kufanya selection wamesahau kusimamia ubora wa elimu ya vyuo vikuu kwani vyuo vingefanya yao katika kufanya selection kwani kwa sasa unakuta mtu angeweza kupata kozi anayoitaka let say Mwanza lakini kwa utaratibu huu wa TCU unakuta mtu anapelekwa Mtwara wakati siku hizi elimu ni ya uchangiaji na kama angepata chuo katika eneo analotaka hata namna ya kumudu gharama ingekuwa rahisi, otherwise nimependa mchango wako hasa hapo bolded
 
naona matangazo ya kuongeza elimu, kazi n.k eti gpa sijui above 3.8, wengine 4.0 n.k n.k
sasa swali langu je ni ya chuo gani? Kwasababu kuna vyuo unaanza mpaka unamaliza hakuna mtu aliwahi kupata gpa ya 4 mifano tunayo ,na kuna baadhi ya vyuo yaani watu wameishia gpa ya 4.0, ukiangalia gpa zao ni vichekesho eti 4.9, 4.8 siuji 4.7 ambayo mimi na u t.o wangu siwezi kwa hiki chuo nilichopo. Elimu ya chuo kikuu bongo ya kijinga kungekua na tcu examinations watu washindane gpa ila sio uhuni wengine wanapewa wengine wananyimwa.
Yaani ni sawa necta zisingekuwepo halafu unachagua watu kwenda form five kuangalia matokeo ya shule zao ya terminal unaweka cuuttpoint kabisa kuanzia 75,na wakati kila shule ilifanya mtihani wake .nazungumza hivi kwasababu kuna shule wastani utakuta wanaanzia 65 wengine 95 n.k
hakuna elimu mbovu kama ya chuo ,unfair.. Elimu form iv tu na six huku kwingine mbwembwe ,ngoja na mimi nianzishe chuo changu wanafunzi gpa zao hazitakua chini ya 4.5 wote wawe na vigezo muhimu .

tcu wasipokuwa makini vyuo vyetu vikuu vitakuwa na wahadhiri bomu, juzi juzi hapa imethibitika kati ya wahadhiri wenye hizo gpa za 3.8 kutoka kenya walikuwa wamechonga vyeti, achilia mbali wenye hizo gpa zaidi ya 3.8 na kuendelea kutoka vyuo uchwara. Kuna vyuo hapa nchini ukipata gpa ya 4.0 wewe ndiyo mjnga darasani, huku vyuo vikuu vikubwa kama sua, udsm gpa ya 4.0 jiandae kubakizwa kuwa t.a maana zitazofuata ni zile zetu za namba za viatu tena vya mtoto mdogo. Nasikia tcu wanatambua mhadhiri wa chuo kikuu aanzie na gpa ya 3.5 lakini hata hivyo utakuta wazawa wenye hizo gpa hawachukuliwi tena kutoka kwenye vyuo vyetu vya hapa nyumbani lakini wanapewa ajira raia wa nchi nyingine kisa gpa za kuchonga za 3.8 ambazo hata hatuwezi kudhibitisha kama ni za kweli! sijui tunalipeleka wapi taifa hili.
 
Hujaelewa mada mkuuu
ndo wewe una watoto au wadogo zako wanasoma shule tofauti wanakuletea matokeo ya terminal unaangalia mwenye wastani mkubwa unasema ndo kichwa ,inakuja necta ndo anakula zero....
Kama uwezo wangu ningependekeza TCU examinations kama cambridge vyuo vyote koz zinazofanana wanafanya mtihani mmoja ,hapo ndo utajua nani mkali sioo siasa hadi kwenye elimu

Haya mawazo tungeyaelekeza kutafuta hela na kubuni ubunifu wa kujiajiri na kufanya kazi kwa bidii taifa hili tungekuwa mbali sana.
Hivi wanajamvi mi kwa upeo wangu mdogo wa kufikiri nina swali!
1. Hivi Bakresa alikuwa T.O? Mzee Reginal Mengi? GPA ya Mohamedi Dewji ni ngapi?
2. Nimrod Mkono alipata sijui mnaita Gentlemen/Pass je nitajie hata Tanzania nani alipata first class ya sheria anamzidi hela huyu mzee! Mnafahami GPA ya Mzee Mwinyi? Mkapa je? Nani anajua GPA ya rais wetu wa sasa? Japo kuna watu wanambeza eti alipata pass pia ni kilaza lakini ndo head of state wa Tanzania.
Mnakumbuka Kikwete alishindana na nani urais 2005? Alikuwepo prof Mwandosya, Dr. Salm na wasomi wengine tena waliobobea kwenye fani zako, swali la msingi, je hao wasomi wakali walimshinda huyu mnaye mbeza kuwa ni kilaza?
Samahani kwa mawazo yangu yasiyo na tija kwasababu mi sijasoma kama nyie huko chuo kikuu, lakini tujiulize GPA kubwa ama ndogo zina mahusiano yeyote na ugumu wa maisha tuliyo nayo sasa? Ni kweli wenye GPA kubwa wana maisha bora kuliko wale wenye GPA ndogo? Ni kweli tukifanya tafiti masalani kwa graduates wa kuanzia 2002 na kuendelea kwa wastani wanafunzi wa UDSM wanaosemekana wana alili sana kulinganisha na wale wa vyuo vingine kama SAUT na Tumaini tukitaja kwa uchache, tutakuta wangapi na wa chou/vyuo vipi wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kimaisha?
Samahani ndugu zangu kwa upeo wangu mdogo wa kufikiri! Nawasilisha.
 
mmbona Muhimbiri university hamtusemi.....wote nyie vilaza
:A S-fire1:😛izza::A S kiss::kev::faint:🙂:ban::smile-big::embarrassed1::tongue::love::wave::frog::tape::A S-key::noidea::help::yield::disapointed:
 
Wasomi wa dot.com mnachekesha sana!! Mnashindana kupata GPA za juu wakati mko empty headed when it comes to skills & knowledge!! Shame on you!!

ndo maana ikawepo training n development makazini mkuu
 
Utakuta mtu ana GPA ya 5.5 lakini utendaji wake ni wa ovyo kupindukia, na hawajui kimombo! Sasa mtu utajiuliza, "hivi huyu alipataje GPA kubwa kiasi hiki ilhali anaonekana kilaza?". Na mtu mwenyewe labda mwanamume, ingekuwa mwanamke labda ungehisi 'kavua'! Du, majanga!

Duh..!! mjomba hiyo ya 5.5 ndo naiskia kwako leo hii pamoja na uzee wangu huu. Kumbe Tanzania tumefika huko..!!?
 
kuna tetesi kuwa SAUT watu huwa hawa disco hata kama ume surp masomo yote, wakat MU uki surp manne usha disco,

Kumbe kwa Bongo ili chuo kionekane kizuri lazima wakidisco wawepo. Vyuo vyenyewe wakufunzi kusifiana wakiwafelisha watu sometimes for their personal interest/gains. Shame on our education system.
 
GPA mbwe mbwe tu chamsingi maisha yako yanakunyookea, full stop, ukitaka mambo ya GPA nenda kwa wataalamu wa elimu tena wanofundisha kwenye hivi vyuo gumashi vyetu hap nchini na sio kitaa, wewe mgodini unaleta habari za GPA, badala ya kutuletea dhahabu safi, chezea kazi za kusaka nyoka wewe.
 
GPA co maisha,uliza jk ana GPA ya ngapi na leo ana nafasi gani katika hili taifa.
 
Maoni yako naona yana afya maana hawa TCU wamejiweka zaidi kwenye kufanya selection wamesahau kusimamia ubora wa elimu ya vyuo vikuu kwani vyuo vingefanya yao katika kufanya selection kwani kwa sasa unakuta mtu angeweza kupata kozi anayoitaka let say Mwanza lakini kwa utaratibu huu wa TCU unakuta mtu anapelekwa Mtwara wakati siku hizi elimu ni ya uchangiaji na kama angepata chuo katika eneo analotaka hata namna ya kumudu gharama ingekuwa rahisi, otherwise nimependa mchango wako hasa hapo bolded

asante mkuu, unajua kuna wakufunzi wanatunga mtihani kama wa kukomoa wanafunzi na kuna wengine wanatunga mtihani chini ya standard. Ni vyema tcu wakawa wanapelekewa mitihani ili kuifanyia aproval kabla wanafunzi hawajaifanya. Kile kitengo cha tcu kinachohusika na mitaala(sylubus) kihusike pia kuhakikisha kama mtihani uliotolewa unakidhi mtaala husika na ni kipimo sahihi cha kumpima mhusika.
Upande wa pili vyuo navyo viwe strick kwa habari ya uuzaji wa mitihani na paper leakege, maana tcu wanaweza kuwa wanatelekeza hayo ila walimu wanauza/wanavujisha mtihani.
Tukifanikiwa hapo hata kama mtu amepewa course work isiyo halali yake atajikuta akiambulia tech sup itakayompa gpa iliyo halali yake
 
watanzania ndo tulivyo eti GPA, GPA kwani GPA ndo inafanya kazi? michosho tu
 
Pamoja na 'kusongoka'kuna departments zinabana sana udsm,mwaka 2009 ktk kitivo cha SOCIAL SCIENCE wanafunzi takribani 1500,FIRST CLASS ilikuwa 1. Tena ya 4.4, mwaka uliofuata yaani 2010 niliomaliza mimi pia hapo hapo udsm,FIRST CLASS pia ilikuwa 1,ktk idadi kama hiyo 1500. Ambayo pia ilikuwa ya 4.4.kiukweli kwa chuo km udsm wengi wanamaliza na GPA za kawaida sana e.g 3.3 haimaanishi km hawasomi.cjui vyuo vingne!
 
Tatizo kubwa lnalowafelisha wengi (especially Form 6 leavers) ni kukosa mbinu sahihi za kusoma vyuoni(university) apart from being clever or T.O....
Mfano:Chuoni kuna kitu inaitwa module/course discription ambayo kila mwanafunzi inambidi awe nayo through out the semester kwa kila somo. Wengi wao huishia kukomaa wenyewe na kukesha usiku kucha wakimeza nakukariri materials ambayo mwsho wa siku kwny mtihani hayatoki mana naamini lecturer mwnyw hawz kutunga out of sylabus.

Ushauri:Tumieni course discription forms ktk kusoma chuo na si kufuata tu kilichofundishwa lecture room pekee na forsure bila hvyo mtazidi kudisco,kusup&kupata GPA kiduchu mpk unagraduate. THANKS ALL!
 
Pamoja na 'kusongoka'kuna departments zinabana sana udsm,mwaka 2009 ktk kitivo cha SOCIAL SCIENCE wanafunzi takribani 1500,FIRST CLASS ilikuwa 1. Tena ya 4.4, mwaka uliofuata yaani 2010 niliomaliza mimi pia hapo hapo udsm,FIRST CLASS pia ilikuwa 1,ktk idadi kama hiyo 1500. Ambayo pia ilikuwa ya 4.4.kiukweli kwa chuo km udsm wengi wanamaliza na GPA za kawaida sana e.g 3.3 haimaanishi km hawasomi.cjui vyuo vingne!

kuna watu watakuja kukujibu kwamba nyinyi ni vilaza.
 
Pamoja na 'kusongoka'kuna departments zinabana sana udsm,mwaka 2009 ktk kitivo cha SOCIAL SCIENCE wanafunzi takribani 1500,FIRST CLASS ilikuwa 1. Tena ya 4.4, mwaka uliofuata yaani 2010 niliomaliza mimi pia hapo hapo udsm,FIRST CLASS pia ilikuwa 1,ktk idadi kama hiyo 1500. Ambayo pia ilikuwa ya 4.4.kiukweli kwa chuo km udsm wengi wanamaliza na GPA za kawaida sana e.g 3.3 haimaanishi km hawasomi.cjui vyuo vingne!

Faculty of law (udsm) sijui ilitoka lini naskia ni zamani sana hata wenyewe haeakumbuki aisee..
 
Pamoja na 'kusongoka'kuna departments zinabana sana udsm,mwaka 2009 ktk kitivo cha SOCIAL SCIENCE wanafunzi takribani 1500,FIRST CLASS ilikuwa 1. Tena ya 4.4, mwaka uliofuata yaani 2010 niliomaliza mimi pia hapo hapo udsm,FIRST CLASS pia ilikuwa 1,ktk idadi kama hiyo 1500. Ambayo pia ilikuwa ya 4.4.kiukweli kwa chuo km udsm wengi wanamaliza na GPA za kawaida sana e.g 3.3 haimaanishi km hawasomi.cjui vyuo vingne!

hivi kumbe udsm firrt class ni chini ya 4.5!
 
Acheck kwanza prospectus ndio aseme ni 4.4 au 4.5 coz najua 1st class n above 4.5 so hyo ya 4.4 tunaitaji muongozo hapo
 
Back
Top Bottom