Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,559
- 11,180
na bodi za wanazuoni kama nbaa, body ya procurement, body ya bank, body ya wakandarasi, chama cha wanasheria(tanganyika lawa society) watafanya nini?
Kumbuka hata kama una gpa ya 5.0 ili kutambulika na hizi body lazima ufanye mtihani wao.
Vyuo viendelee kutoa gpa hata kama mtu hajafanya mtihani, ila kuwe na body ktk kila fani ya kitaaluma ambayo itatoa mtihani wa jumla bila kujali chuo unachotoka(body zote nilizotaja zinafanya hivi)
ila pia kwa nacte vyuo vyote lazima vipeleke mitihani waliyoandaa ipimwe kama imekidhi viwango kabla haijafanywa, sina uhakika kama tcu wana hichi kitu.
Pia kulingana na kalenda ya vyuo huwezi kusema vyuo vyote vifanye mtihani mmoja, mfano kuna vyuo vimefanya UE may(tia, iaa etc) vingine june(udsm, duce,) na vingine ndo wanafanya nw (cbe, st John, ustawi)
unaset vip mtihani hapo?
Maadam kuna prof bodies acha waendelee ila watakapoletwa kwny body ndo tutajua gpa ya kupewa au kutafuta mwenyewe
Maoni yako naona yana afya maana hawa TCU wamejiweka zaidi kwenye kufanya selection wamesahau kusimamia ubora wa elimu ya vyuo vikuu kwani vyuo vingefanya yao katika kufanya selection kwani kwa sasa unakuta mtu angeweza kupata kozi anayoitaka let say Mwanza lakini kwa utaratibu huu wa TCU unakuta mtu anapelekwa Mtwara wakati siku hizi elimu ni ya uchangiaji na kama angepata chuo katika eneo analotaka hata namna ya kumudu gharama ingekuwa rahisi, otherwise nimependa mchango wako hasa hapo bolded