GPA zetu bongo kweli ni kizungumkuti

GPA zetu bongo kweli ni kizungumkuti

yah... hiyo point.... kwenye chuo changu hata second upper class ni ndoto kwa lola mtu....
 
Eeeeh M/MUNGU nakushukuru kwakunijaalia kusoma kwa ajili ya kupanua mawazo na utambuzi wa mambo mengi na wala sikusoma kwaajili ya kupata GPA kubwa!!!! nachojua mimi gpa ni sehemu ya matokeo ya machache uliyojifunza na mengi ni pale graduate atakapokwenda kwenye implememntation ya hicho alichokisoma na sio kujigamba ooohh! mara UDSM hivi mara SAUT vile, mara st. joseph cjui nininini!!!!! someni na fanyeni tafiti za kina zenye tija mnapokuwa mnafanya thesis zenu za masomo, sio kulialia humu JF
 
Naona matangazo ya kuongeza elimu, kazi n.k eti GPA sijui above 3.8, wengine 4.0 n.k n.k
Sasa swali langu je ni ya chuo gani? kwasababu kuna vyuo unaanza mpaka unamaliza hakuna mtu aliwahi kupata GPA ya 4 mifano tunayo ,na kuna baadhi ya vyuo yaani watu wameishia GPA ya 4.0, ukiangalia GPA zao ni vichekesho eti 4.9, 4.8 siuji 4.7 ambayo mimi na U T.O wangu siwezi kwa hiki chuo nilichopo. Elimu ya chuo kikuu bongo ya kijinga kungekua na TCU examinations watu washindane GPA ila sio uhuni wengine wanapewa wengine wananyimwa.
Yaani ni sawa necta zisingekuwepo halafu unachagua watu kwenda Form Five kuangalia matokeo ya shule zao ya terminal unaweka cuuttpoint kabisa kuanzia 75,na wakati kila shule ilifanya mtihani wake .Nazungumza hivi kwasababu kuna shule wastani utakuta wanaanzia 65 wengine 95 n.k
Hakuna elimu mbovu kama ya chuo ,unfair.. elimu form IV tu na six huku kwingine mbwembwe ,ngoja na mimi nianzishe chuo changu wanafunzi GPA zao hazitakua chini ya 4.5 wote wawe na vigezo muhimu .

UDSM na matawi yake unapata GPA hata 4.9 but lazima usome sana tofauti na Vyuo vingine kama Tumaini au RUCO ambapo mwanafunzi akifeli tu mwalimu hana kazi na anaweza kuwa na SUPP lakini wakubwa wakamchomoa tofauti na UDSM na ndiyo maana chuo hiki ni BORA ni cha NNE AFrica.
LINK Top 100 Universities in Africa | 2013 World University Ranking
 
asante mkuu, unajua kuna wakufunzi wanatunga mtihani kama wa kukomoa wanafunzi na kuna wengine wanatunga mtihani chini ya standard. Ni vyema tcu wakawa wanapelekewa mitihani ili kuifanyia aproval kabla wanafunzi hawajaifanya. Kile kitengo cha tcu kinachohusika na mitaala(sylubus) kihusike pia kuhakikisha kama mtihani uliotolewa unakidhi mtaala husika na ni kipimo sahihi cha kumpima mhusika.
Upande wa pili vyuo navyo viwe strick kwa habari ya uuzaji wa mitihani na paper leakege, maana tcu wanaweza kuwa wanatelekeza hayo ila walimu wanauza/wanavujisha mtihani.
Tukifanikiwa hapo hata kama mtu amepewa course work isiyo halali yake atajikuta akiambulia tech sup itakayompa gpa iliyo halali yake
Ninachokijua mimi binafsi ni kwamba mitihan yote ya final (UE) inakaguliwa na external examinors lakin baada ya mtihan kufanyika!, labda sasa TCU waanzishe utaratibu wa kufanya hivo before,ili kuondoa hizi superiority complex na kubezana eti kwasababu huyu kakosa gpa ya 5.0 kwaajil ubora wa chuo chake na yule kapata 5.0 kwaajili ya ubovu wa chuo chake. NOTE: MJADALA HUU NI MPANA SANA NDUGU ZANGU!
 
ahaaaaa!!! bongo bana eti bado mnawaza kuhusu gpa! mbona nchi hi unaweza kua hata gpa ya 4.9 ukasugua bench kijiweni wakat walopata 2 wakula nchi! jitume achana na gpa za bongo!
 
Ninachokijua mimi binafsi ni kwamba mitihan yote ya final (UE) inakaguliwa na external examinors lakin baada ya mtihan kufanyika!, labda sasa TCU waanzishe utaratibu wa kufanya hivo before,"
Mkuu umeona ee! Lazima tcu wakague mitihani ili waiaprove kuwa imekidhi mahitaji kulingana na sylubus husika na ni kipimo sahihi.
Tambua kuwa wanafunzi karibu nusu ya wanaofeli si kwamba ni vilaza ila walimu wanahusika pia ktk kutunga mitihani isiyokuwa kipimo sahihi kwa wahusika
 
Wewe ni hoi katika hoja. Kwa hiyo sifa ya MU ni kuwa na watu wa kudisco. Poleni!
 
Sasa wajumbe hivi hicho chuo ha ST.JOSEPHY ndo kinapatikana wapi na SURP ndio nini wajumbe? Hata abbreviations tu zinawashinda sasa ndo mpewe first class kwel? kuweni serous bwana hakuna Elimu rahisi. Piga shule utatoka
 
Umeongea ukweli UDSM gpa wanatubania, nenda SAUT , ST.JOSEPHY gpa wanapewa tu

Msomi huwa anaongea na facts, unadhani elimu ya UDSM ya zamani ndo ya sasa, ratio ya 1:30? Kuna tcha mmoja alikuja Field ya Econ, kutoka Udsm, japo tulikuwa tumekaa mwaka bila mwl wa Econ watu walimkacha heri wakariri notes, ni weupe kichwani (By Hon. Machemli MP Ukerewe).
 
UDSM na matawi yake unapata GPA hata 4.9 but lazima usome sana tofauti na Vyuo vingine kama Tumaini au RUCO ambapo mwanafunzi akifeli tu mwalimu hana kazi na anaweza kuwa na SUPP lakini wakubwa wakamchomoa tofauti na UDSM na ndiyo maana chuo hiki ni BORA ni cha NNE AFrica.
LINK Top 100 Universities in Africa | 2013 World University Ranking

Kuwa ranked no 4 kuna vitu vingi wanaangalia kama Idadi ya Ma profesa, Dr, resources, ratio ya wanafunzi na walimu, afu hivi vyuo vya gvt huwa vinapendelewa sn, nk. Hivyo basi hawa wanafunzi watokao vyuoni sasa, wenye tabia ya kuongezewa wastani wa 9(maksi 81) ili ufaulu uongezeke 4m 2 kufurahisha wakubwa, na kuongezewa div 1 mbele mtihani wa 4m na 4m 6; jina la chuo halitakubeba ktk utendaji wako wa kazi. Cha mhimu ni kusoma ww mwenyewe kwa bidii uwapo chuoni na c vinginevyo. Kwani huyu mkuu wa nchi kasoma wapi? Na matokeo yake yakoje na utendaji wake wa kazi ukoje?

Bwana Yesu Asifiwe.
 
Ninachokijua mimi binafsi ni kwamba mitihan yote ya final (UE) inakaguliwa na external examinors lakin baada ya mtihan kufanyika!, labda sasa TCU waanzishe utaratibu wa kufanya hivo before,ili kuondoa hizi superiority complex na kubezana eti kwasababu huyu kakosa gpa ya 5.0 kwaajil ubora wa chuo chake na yule kapata 5.0 kwaajili ya ubovu wa chuo chake. NOTE: MJADALA HUU NI MPANA SANA NDUGU ZANGU!

Je hawa TCU watakuwa reliable kwa kiasi kipi? Kama NECTA tu mtihani wa darasa la 7 wanavujisha? C WABUNGE WOTE WA CCM watakuja na degree tena first class 2015!! Kama Mr. MSEMA KWELI aliwandika wachukuliwe hatua hadi leo bado na wengine wakadiliki kulangua vitabu visipatikane hapa Tz!! Hawa NECTA + TCU wakipewa hiii kazi basi elimu mfukoni mwa mafisadi.
Bwana Yesu Asifiwe
 
The highest form of ignorance is when you reject something you dont know about it..... ha ha ha ha ha.



“Katiba ijayo lazima sasa iondoe kinga kwa marais ili mtu yeyote aweze kumshtaki Rais na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa,” Mateo Qaresi.
 
Back
Top Bottom