Kwenye suala la kulipwa kidogo watumishi wa mikoani kulinganisha na makao makuu hapa naungana na mwandishi wafanya maamuzi hawakufikiria zaidi huku mikoani kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi, watu tunafanya kazi kubwa usipokuwepo hata kama unaumwa kazi hazifanyiki kiukweli hili inabidi liangaliwe, Hili la mfuko tunalokatwa kwenye mishahara kuchangia hawakutushirikisha ipasavyo tungeweza kutoa maoni tofauti maana hii mishahara ndio tegemeo letu kwenye kuchukulia mikopo kwenye taasisi za fedha japokuwa wafanyakazi wengi ni waoga ila hawaafiki haya makato ya kwenye mishahara, ni bora ingekatwa sehemu nyingine lakini pia linapokuja suala la usimamizi wa huu mfuko hapa wengi tunapata mashaka, Sisi tulio kwenye taasisi tangu zamani tulishawishiwa kujiunga na mfuko wa GPSA HOUSING na GPSA SACOSS kwa ahadi nyingi sana za kupata viwanja na kujengewa nyumba, kinachoendelea huko kwa sasa kinasikitisha, ukiomba mkopo mwanachama wa kawaida utafikiri unaomba msaada mfuko umebaki kuwa mali ya kikundi cha watu flani, kibaya zaidi mwanachama akifa, akihama,kuacha au kuachishwa kazi hakuna utakachoambulia japo kila mwezi unakatwa kwenye mshahara. wasiwasi wetu ni kuwa huu mfuko mpya ukishakuwa na pesa nyingi hayawezi kutokea kama yale yanayotokea kwenye mifuko mingine maana hii mifuko haifanyiwi ukaguzi. sioni tatizo la mtendaji mkuu lakini kuna watu wanamzunguka na hawa ndio wanaomharibia, kuhusu DBSS huyu hata mimi hapana na nafikiri ndio chimbuko la yote haya
NASHAURI utaratibu wa mwanzo uliokuwa unatumika kwenye kuchangiana kwenye matatizo uendelee huu wa mfuko hapana tunaweza kuwafaidisha watu hapa