Muazisha uzi nakuunga mkono kwa baadhi ya hoja/maovu uliyoibua katika taasisi ya GPSA,Government Procurement Service Agency (GPSA) tatizo ni management kama yule DBSS hafai kabisa kuwa ofisini ni fisadi halafu mbinafsi na mbaya Zaidi anawahonga wakaguzi wanapokuja kumkagua na mambo yanaisha, na ili kulinda ugali wake anawala (anawagegeda) wafanyakazi wa kike walio wepesi kutongozeka ili wawe wanampelekea umbeya ambapo wengi wao anazawadia kwa kuwapa kipaumbele cha visafari na semina pale inapotokea yaani kama una mke wako anafanya GPSA humu jamaa hajali yeye anachovya tu,..na wa kiume nao anaselect wa kuwa wanampelekea umbeya kuhusu wafanyakazi wengine..
Ukiwa hujipendekezi GPSA maisha yako yanakuwa magumu, na CEO naye amemezwa na DBSS na mpenda sifa na maJungu Zaidi ya ufanisi wa kazi anatumia pesa nyingi kuhamisha watumishi kwa sababu ya umbeya tu anaopelekewa, kiufupi hana weledi wa kuongoza taasisi, na hawezi kuifikisha mbali na mara mia angepewa Liliani aliyekuwa ana - kaimu.
GPSA inatakiwa iwe juu ya MSD kimapato na kimaslahi kwa watumishi wake,tuna vyanzo vingi vya mapato lakini viongozi wanawaza ufisadi tu, sasa eti wafanyakazi wa mikoani tunalipwa posho kidogo kulinganisha na makao makuu kisa tuko mikoani tunatakiwa kulipwa tofauti na wa makao makuu, sasa kama hatuna umuhimu kisa tuko mikoani si bora tuhamishiwe wote makao makuu na mikoani kusiwe na wafanyakazi kama hawaoni umuhimu wetu na posho sio ya uhakika mpaka viongozi waanze kupiga majungu na kuchagua watu wa kuwapa…
KINACHOTOKEA SASA watu majembe wote wanaondoka, asilimia 90 ya wafanyakazi wa GPSA hawana moyo wa kufanya kazi kwenye ofisi hiyo wapo wakisubiri wapate nafasi waondoke sehemu zingine
.
serikali ingetakiwa ipangue management ya GPSA YOTE, wengine wangetakiwa wawe magerezani kabisa kama DBSS..
Wanaidhinisha makato ya mshahara ya watumishi bila idhini yetu, eti mfuko wa faraja GPSA. Yaani unashangaa mshahara unatoka unakutana na makato usiyoyaelewa, sawa ni jambo jema.. why wasingekata hata kwenye nauli..mishahara yenyewe ni midogo na ndio tunategemea kuikopea, wanaongeza makato kitu ambacho kinatupunguzia kiwango cha mkopo bank wakati walikuwa na option ya kukata hiyo pesa ya mfuko kwenye posho zingine.
Hii tasisi watu hawaipendi kiasi kwamba ni vigumu kukuta watu wamevaa fulana ya GPSA maofisini, zaidi tukipewa huwa tunawapa wafanyakazi wetu wa ndani wavae au wpigie deki, ama tunawapa mama ntilie
Mimi nikazia/ibua ufisadi, fitna majungu na matumizi mabaya ya madaraka unaofanywa na meneja GPSA Clearling somebody Mr. Jimi, naomba ieleweke haya yanayoandikwa sio majungu ni ukweli mtupu na inafanyika hivi katika kumsadia bosi wa GPSA anaefanya jitihada kubwa kuiboresha GPSA.
1. Ufisadi mkubwa unaofanywa na meneja clearling ni kutumia baadhi wasafirishaji ( transporters wasiotambulika na GPSA wala PPRA na mara nyngi anapowatumia hupata kamisheni kubwa ambayo hupitia kwa stafu
anaitwa Jafeth ili ampelekee bosi wake. matransporters hao anaonufaika hulipwa pasi kuwasilisha EFD risiti wala hawakatwi witholding tax wakati invoisi zao
zimeonyesha VAT ( bosi GPSA, TRA kodi za ndani, PPRA na TAKUKURU) fuatilieni hili kodi (VAT) ya serikali inapotea sana Wakaguzi wa ndani na nje fuatilieni hili mjue ukweli na mumsaidie CEEO wa GPSA
huenda hajui hili.
2. Kwa ukaribu alionao na bosi wa GPSA CEEO meneja Jimmi amekua akifanya kazi kwa fitna, majungu na upendeleo kwa baadhi ya mabinti aliyo kwenye mahusiano nao kimapenzi. mara kadhaa amekua akipitisha malipo makubwa kwa kaz ndogo kwa hao mabinti, na hili lilishapata
kulalamikiwa na stafu wa kiume katika vikao vyao vya ndani. (bosi GPSA fuatilia hili ujue ukweli).
3.Meneja huyu wa GPSA anatumia madaraka vibaya kuna stafu wa kike-
Interni kwa jina kama sikosei alikua anaitwa Aulah aliondolewa kwa
fitna na majungu kisa tu alikataliwa kua na mahusiano ya kimapenzi, binti huyu
aliondolewa pasi hata kulipwa stahiki yake ambayo haizidi hata laki tatu. GPSA stafu wote wanalijua hili ( Bosi wa GPSA fuatilia hili kupitia informa wako upate kujua ukweli).
4. Meneja GPSA clearling amekua ni mtu mwenye majivuno, kibru, jeuri na mwenye dharau kwa wateja, makandarasi wa miradi mbalimbali ya serikali wanao clear mzgo yao kupitia GPSA wanaweza kua mashuhuda
wazuri juu ya meneja huyu.
5. Matumizi mabaya ya gari la serikali na mateso makubwa kwa dereva wake. Meneja GPSA clearling amekua akikaa bar/night club hadi usiku wa manane ( mpaka sa8 usiku) huku dereva akiwa anamsubiri nje pasi kumnunulia chakula wa maji na hii haijalishi ni wiki days ama wikiend, hili sio jungu ni ukweli mtupu, madereva wa GPSA wanaweza kua mashuhuda wazuri ( bosi GPSA CEEO fuatilia hili, Jimmi anatumia vibaya rasilimali za umma ambapo ni kinyume cha sheria utumishi na anawapa
mateso makubwa madereva wake). kuna dereva anaitwa Haule hakua tayari kuvumilia mateso hayo, mwishowe Jimmi akamtengenezea zengwe ili afukuzwe kazi lakini akagonga mwamba, na dereva huyo akahamishwa. (Mamlaka husika fuatilieeni hili).
6. Kwa kua meneja Jimmi anabebwa sana na bosi kubwa wa GPSA, amekua akimpelekea CEEO majungu juu ya baadhi ya wafanyakazi wa GPSA Clearling na CEEO bila kufanyia uchunguzi kupitia informa wake (naamini anao wengi) amekua akiwahamisha bila sababu za msingi ( hapa
bosi GPSA awe anafanya uchunguzi kujiridhisha ndipo achukue hatua),
katika kisichozidi miez 9 amewapiga majungu stafu zaid ya 7 wakahamishwa bila sababu za msingi.
7. Meneja Jimmi ni incompent person yaani ni kilaza sijui alipataje hio nafasi nyeti na kubwa, nadhani alibebwa. Kupitia GPSA Clearling amekua akiisababishia serikali na taasisi zake gharama kubwa za kutunza mizigo bandarini ( storegi charges ) hili sio jungu mashuhuda wazuri hapa ni taasisi/mashirika/wizara zinazohudumiwa na GPSA kama Muhimbili chuo, Muhimbili hospital, MSD, nakadhalika.
Hitimisho, kwa kutoa rai kwa bosi wa GPSA CEEO, anavyoendelea kuiboresha GPSA atume wakaguzi wa ndani na nje ndipo atakapobaini ukweli haya yote yaliyosemwa;
- Baadhi ya wasafirishaji (transporters) wasiosajiliwa na GPSA wala
PPRA nyingi ni briefcase kampani hawana ofisi wala roli hata moja.
-Baadhi Wazabuni/transporters kulipwa pesa kamili pasi kuwasilisha
receipt za EFD wala kukatwa witholding tax wakati invoice za zimejumisha VAT.
-Majungu waliotengenezwa kwa stafu zaidi 7 mpaka ikapelekea huhamishwa
bila sababu za msingi.
-Gharama kubwa za utunzaji (storage chargi) zinazolipwa taasisi za
uma ikiwemo mzigo inayoaagizwa na GPSA wenyewe.