GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo

mwanzoni mwa huu uzi nilijua yawezekana kuna watu wanaunda majungu, baada ya kusoma vizuri michango ya wadau naona kabisa kuna shida kwenye hii taasisi, nimejaribu kuongea na wafanyakazi baadhi wa GPSA ili kupata ukweli maana kuna rafiki zangu wako halmashauri na walikuwa hatua za mwisho kuhamia hapo, wanavozungumza kuhusu taasisi yao unaona kabisa kuna shida, jamaa wameamua kucancel uhamisho.
 
Kwa ukweli hii taasisi ina aminika kuwa na shetani watatu wanaofahamika mkubwa wao ni huyo DBSS. Kazi yao kubwa ni kuiba na kutesa wenzao. Katika kuficha ili wasionekane wala kujulikana kwa wakubwa, wamekuwa wakishindana kusafiri kutafuta kinga kwa Sangoma. Wanaoteswa ni wale wasiopenda kuiba na kutesa wenzao kama shetani hao.

Kiwango cha utendaji wao kina mashaka makubwa kwa kuwa kila kitu kinachakachuliwa ili zipatikane pesa za kupeleka kwa sangoma ili kujilinda dhidi ya anayeweza kuona au kushtukia hali hiyo.

Hapa ndipo tulipofika na hi ndio hali halisi, kila kitu ni sangoma. Kwa takribani wiki moja sasa nasikia DBSS hayupo na hakuaga kuwa amekwenda wapi. imebaki ikiaminika kaenda kuweka mambo yake sawa kwa Sangoma kuzima hili skendo
 
πŸ™‚πŸ™‚nafurahi sana kuona jipu limepata mtumbuzi, GPSA nina marafiki wengi niliowaacha pale nitaenda wiki ijayo kuwatembelea. Mimi ni mvivu wa kuandika ila siku nikiandika humu kutalipuka, naona nyie mnagusia juu juu tu,nashauri hata Werema afuatwe huko TASAC aulizwe nini kilifanya wakashindwana na uongozi wa GPSA, watajua mengi huyu jamaa alikuwa kichwa sana
 


Suala la Jimmy .,...Siku Zote Ukisimamia Ukweli Lazima Uwe na Maadui ...Kitengo Cha Ugomboaji ...Ukiwa Mgumu,mchapakazi lazima Upigwe mawe ...Manager Government Clearing,Bwana Jimmy Anapambana Sana na Hizo Kashfa zote anazopewa Hapo Ni Njia ya Kumuondoa Yeye Kwenye Mapambano Kwa Mwaka Huu wa 2020 .... Ugomboaji Wamevuka Malengo ya 5% Kwenda Juu ya Idadi ya Mizigo Yote ya Mwaka 2019 na Mizigo Yote iliyotoka Mwaka Huu 2020 ..kwa sisi clearing Agents Ambao Tunafanya Kazi na GPSA kupitia Kwa Government Project Nyingi Tunafurahi Kwa Kazi Nzuri ya Hiki Kitengo Cha Ugomboaji ...Vijana Pamoja na Meneja wao Hawalali Kwenye Entry zote Kuanzia Aiport (Swissport,DHL,African flight),Bandari(Ticts,TPA,ICD's) na Road Consignment Wanafanya Kazi Kubwa Sana Kwa 24/7 Kwa Siku Zote za Kazi Kiserikali na Nje ya Kazi
 
Tunafurahi Mizigo Yetu Inatoka Kwa Wakati na Uhakika Kupitia Ugomboaji
 
Usiquote Mimi kuhusu Jimmy, huyo mtu Mimi simjui kabisa siwezi kusema uongo juu yake na Wala sijazungumzia, nilicho na uhakika nacho nitakisema kwa vile tu ni mvivu wa kuandika ila iko siku nitaandika, pale Kuna upumbavu mwingi sana hasa huyo mkurungenzi wenu wa fedha na utawala ni mshenzi mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbna umekwepa tuhuma zilizoelezewa, wewe unachozungumza ni kitu tofauti ingawaje ni ukweli kwa taarifa za uhakika japo sijafika mda mrefu huko ofisini kwenu, Kwa hali ilivo Sasa Kitengo kimeimarika sana na watu wanapiga kazi. Lakini vipi kuhusu tuhuma za upigaji zilizotajwa hapo juu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M2wawa2 ningejuaje kama wewe mi wa aina hiyo kama hukujionyesha?
 
Tunapiga kazi sana huku mikoani halafu hata hawatuthamini na huu mfuko hata mimi naona kabisa umekaa kiwiziwizi kwa huko baadae mimi barua yangu tayari wanayo wanitoe tu kwa kweli
 
mkuu upo TANESCO Nini
 
Da inasikitisha sana. Pole sana kwa wafanyakazi mnaopitia madhila hayo. Nimesikitishwa na huyo mama aliyekuwa na tatizo la kansa na pia kufariki japo taasisi siyo iliyosababisha kifo ile tu kunyimwa uhamisho mapema uenda angeishi miaka mbele zaidi.Nimesikitishwa pia na huyo mfanyakazi pia aliyeacha kazi baada ya kuhamishiwa Songwe na Ruvuma. Jambo moja nalofahamu mimi ni vizuri ukishindwa kutendewa haki ya kiutumishi uende ngazi za juu nje ya taasisi yako naamini msaada upo. Taasisi siyo mwajiri wa mwisho wa mtumishi. Ukikosa msaada kabisa huko ndo sasa waweza kuamua vinginevyo. Nampongeza aliachishwa kazi alichukua hatua na haki yake ikapatikana. Vyema sana serikali kufuatilia kwa karibu taasisi hii. Hizi ni tuhuma nzito sana na siyo kuacha zipite tu. Waliotoa taarifa hizi ni whatchdog/ whistle blowers wasipuuzwee
 
Basi wewe ni mzalendo, hii taasisi nasikia inanyanyasa sana wafanyakazi wake ni kweli?Kuna jamaa zangu wako halmashauri walikuwa kwenye process za kuhamia huko Baada ya kuona huu uzi wameona isiwe tabu naona kila mmoja amegeuza gia angani
Mkuu, Kuna rafiki yangu nae alikuwa kwenye process Kama hao jamaa. Yeye barua yake imeshafka Hadi Utumishi maana alishapata nafasi huko. Kwasasa Anasema amefwatilia Utumishi akakuta barua ipo hatua za mwisho kukamilika uhamisho. Sasa nayy baada ya kuona huu uzi, anataka ku cancel, je afanye hatua zipi ili a cancel uhamisho huko.
 
πŸ˜ŽπŸ˜ŽπŸ˜ΆπŸ˜ΆπŸ€¨πŸ€¨πŸ˜‘
 
Yametimia, Kisiki kimeng'olewa GPSA. Huu ni mwanzo tu

Serikali huwa hailali kwa tuhuma za kweli. Ma-infomer mliopo GPSA mmefanya kazi nzuri sana
Kuna nini kwani huko? Weka japo press release
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…