Tatizo kubwa na huu ndio ukweli ni kwamba GPSA ilikuwa shamba la bibi huko zamani sasa hivi taasisi hii inafanya vizuri mno.
Tatizo watumishi wamekaa sehemu moja miaka na miaka kwa kuwa hakukuwa na uwezo kutoa stahiki za uhamisho, kwa sasa Wakala huu unavyopiga hatua kuongeza mapato inahamisha watumishi kwenda maeneo ya kukusanya mapato ya serikali ili kuchangia uchumi wetu, mbona wengine tumehamishwa na tumekubaliana kuwa ni kwa maslahi na hitaji la utumishi wa umma na hatulalamiki?
Wapo tuliohamishwa kwenda kwenye mikoa na sio kijijini ni makao makuu ya mikoa ya Tanzania bara kuongeza nguvu au kuongoza utamaduni huu haujakuwepo tangu GPSA imeanza na wapo waliohamishwa na idara kuu ya utumishi yani Wizara ya utumishi kwa kuwa ni kwa maslahi mapana ya umma nikiwepo mimi, watu waliokulia hapo hapo na ikaonekana tuhamishww kuleta maboresho kwa Wakala uliofikia hatua ya kufutwa kabisa kwa kuwa ulikuwa haujawahi kufikia lengo la kuanzishwa kwake, tumehama tulipewa stahiki zote kwa mujibu wa kanuni za utumishi!
Kwa mara ya kwanza bila kushurutishwa GPSA imetoa gawio serikalini ile awamu ya kwanza kabisa . Ni maendeleo makubwa mno na brand yake imekuwa kuliko miaka yote ya huo uongozi unaoonekana ulikuwa na afadhali! Na kama ni suala la watumishi posho, haijawahi kutokea hata siku moja miaka yote huko nyuma kuwa na posho hizo? Sasa hivi waliopo pale wanapewa! Sasa kwa nini tusione sasa hii ni mwanzo mzuri kwa uongozi uliopo? Mimi ambaye nimehamishwa ninaona maendeleo na haya hapa ni majungu ya baadhi yetu tuliohamishwa kwa maslahi mapana ya umma.
Pia uongozi wa serikali umeendelea kuboresha taasisi zake na baada ya muundo mpya wa GPSA wapo ambao ni viongozi nafasi zao hazikuwepo kwenye muundo huo mpya kwa sasa ndio wanataka kuongoza majungu haya. Ikumbukwe GPSA ina maslahi makubwa ya nchi.
Hiyo clearing inayotajwa tajwa inafanywa kwa kiwango kikubwa na hapa wengi wanaotaka kuhujumu serikali wana hasira kwa kuwa walikuwa na makampuni au wako nyuma ya makapuni ya watu binafsi tangu tukiwepo hapo. Sasa wanaumia kwa sababu biashara hiyo sasa inasimamiwa na GPSA yenyewe ujanja ujanja hakuna.
Ninashauri pia tuangalie zamani GPSA ilikuwa inatoa kiasi gani serikalini na sasa wanatoa nini? Na ni kwanini serikali ilifikia hatua ya kuifuta Wakala huo na kwanini leo hii serikali imewapa dhamana ya kugomboa mizigo yote ya serikali! Sio kwamba wameaminika?
Mimi niliekuwepo hapo GPSA ninaona kabisa baadhi yetu tumeanza kuhujumu umma na juhudi za serikali katika kuongeza mapato yake huu ndio ukweli. Tuache maslahi binafsi na taamaa zetu na badala yake tujikite kujenga nchi! Na tukumbuke kuwa sio lazima wote kuwa viongozi na tukiendelea hivi huku tulipo tutaonekana hatufai.