Graduates wengi mkiweka aibu na uoga pembeni, basi mtaani mnaishi

Nilikutana na kimbunga cha uchumi kuyumba 2016 mishe zote zikafa. Nikafungua mgahawa mwananyamala biashara ikagoma ,ikabidi nitengeneze toroli ili iwe mobile kitchen.

Nikawa napika chapati ,nilianzia posta pale kituo kinapakana na usalama wa taifa,tra na mamlaka ya bandari. Baishara ilikua nzuri kweli ila usalama wa taifa wakanitimua. Nikahamia na toroli langu kigamboni nako biashara inawa ngumu Sana,kimara,mbezi kote hola.

Nikaamua kubeba toroli langu mkoani mbeya,nimepambana soweto kama miezi 6 hola. Huku nasikia maneno tu huyu amechanganyikia make amesoma ulaya saizi ilitakiwa awe na kazi nzuri tu.

Baada ya mapambano ya muda mrefu gizani sasa jua limewaka. Waliokua wanasema mbovu wanajificha huku wengine wakijisogeza karibu ili waonje keki ya mafanikio. Maisha ya kutafuta hela inatakiwa kujikana nafsi tu ,usione aibu kwani njaa ni yako na familia yako. Unaemuonea aibu ndiye awe mteja wako wa kwanza.
 
Daaaaah,maisha ya kujiajiri yana changamoto kubwa sana

Waliokuzunguka wana kushangaa kusoma nje na kufanya hizo kazi au wana shangaa kutokana na elimu uliyo nayo?
 
😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣
 
Yaaan mimi ndo siwezi kujilipua nina maaibu na mauwoga kama yote[emoji16][emoji1787][emoji1787]
Jitahidi anza hata na kimgahawa kisha uendee catering deals. Utasogea mamii!

Yani inatubidi tufanye mambo wanayofanya hata wasioenda shule ili tusogee tu. Chukulia kama wewe ni inferior tu hujawahi zama class. Chukulia corrola kama landcruiser upite kwenye dimwbi hilo hilo la aibu usogee mbele kwenye mafanikio.
 
Nilikuwa na mentality ya kuwa eti nimesoma mpaka level fulani basi nikawa nachagua kazi na kufungua biashara ndogo nikawa naona aibu

Nilichofanya ni kuhama mtaa na kuanza biashara ndogo baadae nimekuja kupata kazi wakati naendelea na biashara ndogo na ikazaa nyingine.

Kikubwa kama mtaa unaoishi wanakujua vizuri inabidi uhame ufanye kazi zako kwa uhuru na jitahidi kufanya mambo yako kisiri usimwambie kila mtu
Ulianzaje mkuu,nipe somo mkuu.
 
Sikuhizi unahitaji bundle tu hata ukiwa Kibondo au Ndungu mradi upate internet connection unawafikia walioko hata marekani.

Sasa connection ipi unayozungumzia kijana au ile ya kukaa bar kunywa bia za bure kila jioni.🤣🤣🤣
 
Hahah sawa kabisa, na hio ndio mbinu ya kijasusi.
 
Ila kwa kweli Leo umeahusha nondo itamsaidi sana waha madogo
 
Hii safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…