Juzi imepita Nissan Primera moja iko mafuta sana. Ghafla nikaona imerudi mpaka nilipokua. Jamaa akashusha kioo.
Jamaa: Oya niaje?
Mimi: Freshi chief, karibuu (Hapo
nimemtambua, niliskulinae)
Jamaa: Sikuhizi ndo uko hapa?
Mimi: Ndio chief, shuka nikupigie maji ndinga
hiyo, buku tano tuu.
Jamaa: Mwanangu acha kutusanif bwanaa, we
jamaa ulikua na maakili ulikua
unatukimbiza kwenye namba.
Mimi: Akili zangu kwasasa zimeishia hapa.
Jamaa: We si nilisikia ulikua unasoma
madegree huko. We ulitakiwa uwe
mabenki hukoo, maana yale mahesabu
nomaa
Kufupisha story:
Jamaa amenikuta car wash naosha gari za watu akakataa kukubali akirefer ufalme wa shule kua sikutakiwa kua pale.
Hiyo ndo jamii inayomzunguka graduate. Tunahitaji kujikana ili uishinde.