Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi

Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi

Unajua kuna msemo unasema ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu, ndio graduates wengi ambao hatuna kazi tunapitia hiyo hali yaani hatuna haki kabisa, now tumekuwa jalala la matusi sii la Saba, fm4 failure, waliobahatika kupata vijikazi, wanatuona kama wajinga, wazazi jamii inayotuzunguka wote wanatuona mafala hakuna wakututetea.

Yaani ukitaka kuiona dunia chungu, maliza masomo/degree halafu usipate sehemu ya kujishikiza au mchongo wowote asee utachekwa hadi na watoto wadogo, najua wengi hasa graduate mnanielewa ninacho zungumzia, just imagine interview ya jana TRA watu wanaitwa zaidi ya elfu sita kugombania nafasi mbili kwa kweli inasikitisha.

Now hata nafasi za kujitolea kwenye makampuni hazipo yaani ebu fikiria mtu anajitoa kufanya kazi bila malipo lakini bado unakataliwa, sio tu kwenye makampuni makubwa, hata kufanya kazi kama kibarua kwenye miradi ya ujenzi napo bilabila, viwanda vidogo vya kufyatua tofali unakuta kumejaa.

Yaani kwa sasa mambo yamebana hata nafasi ya kufanya field ukiwa bado unasoma napo unaweza kukosa kabisa, kuna zile kazi za kupakua mizigo inayotoka mikoani kama magunia ya mpunga, viazi huko kote bila connection hata kama una phd dalali hakupi kazi.

Kilicho nisukuma niandike haya yote leo kuna jamaa yangu ninapokaa ametimuliwa na mama mwenye nyumba kisa kushindwa kulipa kodi. Jamaa yeye ni graduate wa ba education toka 2018 anauza matunda kwa wanafunzi wa chuo kwao ni Kigoma kisa Corona mambo yameenda vibaya kodi yake iliisha toka tarehe moja leo mama mwenye nyumba ameleta dalali wakakagua nyumba na vitu viko ndani akafukuzwa.

Jambo ambalo nataka kuwaambia magraduate wenzangu usikomalie tu kukaa Dar es Salaam ukiona maisha hayaeleweki rudisha mpira kwa kipa sio kukomaa kwenye hakuna, mikoani kuna fursa nyingi kuliko Dar es Salaam kwanini nasema hivyo, Dar es Salaam imeshakamatwa na wafanyabiashara wakubwa.

Waliobaki wengi ni machinga kama unataka kuamini nenda kesho Kariakoo, Ilala, Makumbusho, Gongo la mboto ujionee mwenyewe machinga walivyojazana.

Kuingia kwenye system ya kujiajiri hasa biashara ni rahisi sana kwa mji unaokua mfano Dodoma kuliko sehemu kama Dar es salaam ambayo tayari mabeberu walishaishika toka kitambo, jaribu kuangalia gharama za ulipaji pango, umeme, usafiri ndio utaelewa.

Yaani kodi tu ya fremu Dar sehemu ya uchochoroni unaambiwa laki 4 na dalali anataka ya mwezi mmoja,

Najua kuna madogo wengi watasoma hapa, nakwambia kabisa jaribu kutafuta ujuzi binafsi huko chini, ukiona kitabu hakipandi nenda veta, kasomee electronics/ ufundi simu, gerage/umeme wa magari, pikipiki, ufundi bomba, umeme majumbani, kupaka rangi, kutengeneza furniture/sofa hawa watu wana uhakika wa kuishi mjini vizuri kuliko graduate wa kwenye makaratasi.

Kariakoo pale kuna mtu ana masters nilimkuta anafundishwa kutengeneza simu na fm4 B tena pale kwenye msururu wa vile vimeza vilivyopangana pale njee, maisha yamempiga hatari,

Nihitimishe tu kwa kusema Mungu atujaalie na atutangulie tuweze kutimiza ndoto zetu na atuwezeshe kuvuka salama katika hiki kipindi cha mpito.
Dah ukweli mtupu mimi na degree yangu nilisotea kibarua cha saidia fundi kwenye mradi wa tazara flyover na nikaukosa sikukata tamaa nikaenda na wa pale ubungo nao pia nikapigwa chini dah we acha tu yan hata huko nako unahitaji konection
 
Nakumbukaga nilicheke series fulani iliyokatishwaga kuoneshwa japo ilianza kubamba vibaya sana iliitwa "Travellers "

Kuna madogo wawili waliharibu kwao Mambo yakawa magumu hawajui waende wapi

Mmoja akamwambia mwezake" let's go new york"

Jamaa akaumuliza "why new york?"

Ajibiwa "there is no success like new York success" hao wakasepa .

New York Ni moja miji yenye ukwasi wa kutosha ma mzunguko mkubwa hela wall street iko new York big business zinatembea new York na gharama za maisha ya new Ni kubwa Ila ukitusua new umetusua kweli kweli

Dar ndio new York ya Tz ukitusua dar umetusua kweli kweli

Huko vijijini Ni kupoteza muda

Dar ndio bongo ,ukiwa dar tumia ubongo.

"There is no success like dar success"

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana kaka maana umetype kwa feeling until umeweza kuchanganya na lugha fulani. Ni ukweli usio pingika hio hali ipo katika jamii zetu na mitazamo ipo mingi sana, binafsi hio hali nimewahi kuipitia mwaka 2014-2015 na ilifikia wakati mpaka kutokua na maelewano mazuri na mzazi wa kiume kwa kipindi fulani ila kwa majukumu niliyonayo sasa naelewa kwanini hali ilikua vile kwa mzee. Kikubwa ambacho naweza shauri kwa Graduates

1. Jaribu kuangalia circle na network ya rafiki ama watu wa karibu na wewe? Je ni watu wa hustles au ni wenye mawazo ya kusubiri chakula kuiva nyumbani
2. Jitathmini wewe mwenyewe uwezo wako wa kutengeza mahusiano na watu mbali mbali
3. Jichanganye na watu tofauti na kuwa huru na wazi kujieleza kwa watu unao kutana nao
4. Usikubali kupoteza muda wako kulalamika sana bali kuwa mdadisi wa fursa zinazopatikana
5. Ruhusu akili yako kutembelea ndugu na jamaa kama upo mjini nenda hata kijijini na vice versa ukiwa na lengo la kuangalia nini unaweza kufanya mbadala
6. Ruhusu akili yako kukubaliana kufanya kazi ya halali ambayo haina athari kwa afya yako na weka kando qualifications zako; Niliwahi kusafisha vyoo vya SABASABA maonyenyesho na ndugu yangu na ilikua gateway ya kupata connection nyingine
7. Tumia muda mwingi kujiongezea maarifa kwa kujifunza soft skills mitandaoni zitaweza kusaidia kufika mahali fulani.

Hii hali ya kutokua na cha kufanya ni hali mbaya sana katika maisha ya mwanadamu na usikatishe wenzako tamaa au kudhihaki maana kila mmoja ameandikiwa rizki yake ila ni wakati au mahali huwa tofauti. tuombe sana na pia tukifanikiwa tuwe na akili za mbali sana ili tusiridhike na ujira au malipo bali tujiongeze kujitanua kiuchumi.

Nawatakia kila la kheri ndugu zangu In sha Allah mbarikiwe sana.
 
Kupanga ni kuchagua. Personally namshukuru mungu shughuli nnayofanya inaniingizia kipato na mimi najiona mtu mbele za watu. Hata kutuma maombi ya kazi nimeacha. Yani ofisi yangu ni simu yangu kila kitu nafanya online. I love this life hapa nafikiria jinsi ya kukuza hii biashara.

Asikwambie hakuna raha duniani kama kujiajiri, kwanza ukiwa mfanya biashara pesa unakua nayo kila siku sio kama waajiriwa wao pesa wanashika mwisho wa mwezi tu alafu baada ya wiki wanaanza msoto. Vijana acheni kufikiria kuajiriwa ndo njia pekee ya kutoka kimaisha. Think outside the box.
 
Kupanga ni kuchagua. Personally namshukuru mungu shughuli nnayofanya inaniingizia kipato na mimi najiona mtu mbele za watu. Hata kutuma maombi ya kazi nimeacha. Yani ofisi yangu ni simu yangu kila kitu nafanya online. I love this life hapa nafikiria jinsi ya kukuza hii biashara. Asikwambie hakuna raha duniani kama kujiajiri, kwanza ukiwa mfanya biashara pesa unakua nayo kila siku sio kama waajiriwa wao pesa wanashika mwisho wa mwezi tu alafu baada ya wiki wanaanza msoto. Vijana acheni kufikiria kuajiriwa ndo njia pekee ya kutoka kimaisha. Think outside the box.
Unafanya biashara gani.
 
Nguo, urembo, accessories za kina dada. Nina online store Instagram... no physical location.

Instagram kuna biashara sana yaani sio poa ni wewe tu kuwa creative na content zako graduates wengi insbid washtuke mapema pesa ipo mingi mtaani anyway tuwaache tu waendelee kusambaza cv huku mda ukienda ajira saiv ni kama kubeti tu
 
Dar ni nzuri kwa wale ambao wanajua nikiamka kesho naanzia hapa
Lakini tofauti na hivyo mpaka uje upate mwelekeo ushahenya sana.

Halafu vijana epukeni majukumu yasiyokuwa ya lazima mapema unalemaa kimaendeleo
 
Back
Top Bottom