Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Nadhani hata suala la kutafuta maisha nchi za nje nalo limepitwa na wakati. Teknolojia imewezesha kupata vitu vingi sana by proxy
 
Elimu yetu tuliyopewa haitoshi. Tumefundishwa kulikimbia tatizo badala ya kulitatua tatizo kwenye mazingira yetu. Kama tatizo ni uongozi haufai wewe utachangiaje katika kutatua changamoto ya uongozi nchini kwako? Kama shida ni neo colonialism wewe ulifanya nini kama kijana. Vijana wetu ukiwemo ww mnaona suluhisho ni kukimbilia kule ambako vijana wenzenu wa mataifa hayo walipambana na mifumo Yao kwa jasho na damu zao kurekebisha mambo.

Vijana kama Ibrahim Traore kule Burkina Faso wanatafuta majibu ya shida zao wakati you cowards majisalimisha kwa watesi wetu kuwa manamba (cheaper labors) kuyajenga mataifa Yao. Narudia tena elimu yetu inawafanya vijana wetu iwe rahisi hata ikibidi kuf*rwa (short cut) ili kutoboa.
 
Kwenye jedwali hawa jamaa wapiga mabomu toka kote wanataka kwenda huko wakaimbe habeeb na wanazaa km mchwa.
Ngoja tunywe supu nyama ziko chini
 
Nipe statistics za Waafrika ambao walipelekwa Marekani kama watumwa kutoka west Africa kupitia the Atlantic ocean. Watumwa wanahitajika hadi Leo ila tofauti ni namna wanavyowapata.
 
Nipe statistics za Waafrika ambao walipelekwa Marekani kama watumwa kutoka west Africa kupitia the Atlantic ocean. Watumwa wanahitajika hadi Leo ila tofauti ni namna wanavyowapata.

According to Statistics nazokupa...Warusi ndio wanaongoza kuingia kama Manamba.....!Au Huangalii...
 
According to Statistics nazokupa...Warusi ndio wanaongoza kuingia kama Manamba.....!Au Huangalii...

Na kinachochekesha si Waafrica tu......Tanzania ni 165 tu......Urusi ni 5,505 2023........Nakumbuka Mwaka juzi fundi wa simu aliyekuja ku fix Modem yangu toka kampuni ya simu alikuwa Mrussia......
 

Upo Africa wewe......nipe Idadi ya Mapinduzi ambayo imeleta matokea chanya Africa...maybe 2%......Je mpaka leo changamoto ngapi zimetatulia.....Kuchimbiwa vyoo....Vyandalua kujikinga na Malaria.......Au Hujui Bajeti zetu zinategemea kiasi gani kutoka Nje.......Sijui uko upande upi wa Bandari....Wengine wanasema imeuzwa.....Wengine wanasema tunawapa Dubai kuzuia wezi....Kwe;i tunajua kupambana na changamoto....!
 

Kavulata......unasema " Elimu yetu tuliyopewa haitoshi" Hiyo mitala ya elimu inatengenezwa na nani......Si na watu kama wewe....Kila tatizo Beberu.....Beberu.....Beberu.....Miaka nenda tunaletewa vyandalua kujikinga na Malaria.....tunaleta wawekezaji toka China kuuza maua karikooo.......Unataka Nani amwelimishe nani.....na elimu kama ipi....? Maana Vijana wana elimu hawana kazi......!The only way ni kuingia siasa....short cut ya kufanikiwa Tanzania!

Tuliimba na kufundishwa Ujamaa......Waliousoma huo Ujamaa vyuo vikuu miaka ya 60-70.....Walipokuja kushika viwanda miaka ya 80 wakavimaliza.....! Au hauko Tanzania....
 
Nadhani hata suala la kutafuta maisha nchi za nje nalo limepitwa na wakati. Teknolojia imewezesha kupata vitu vingi sana by proxy

Extra Miles.....Nakubaliana na wewe Mkuu, hilo halipingiki.....Lakini kuhama Nchi ni zaidi ya kupata vitu......kuna sababu nyingi mno.......sometimes ni pure adventure.....aina ya maisha unayotaka.....ambapo ulipo huwezi kupata kwa urahisi huko uliko...Ndio maana kama umesoma mada huko nyuma. mara nyingi nawauliza watu wanaotaka kuja US, ni kuwa unakuja kufanya nini! Je umeshindwa kupata unachokitaka Tanzania?
 
Binafsi nadhani kama ni suala la adventure linafanyika kwa njia ya utalii, ila suala la kutafuta maisha linaanza na mtu binafsi kufanikiwa nchini kwake na kisha kwenda nje kama anahitaji kufanya hivyo.
 
Nipe statistics za Waafrika ambao walipelekwa Marekani kama watumwa kutoka west Africa kupitia the Atlantic ocean. Watumwa wanahitajika hadi Leo ila tofauti ni namna wanavyowapata.

Kavulata Statistics za nini...mbona ni mamilioni.....kinachoumiza zaidi ni babu yangu na babu yako walishindwa kabisa kuwazuia wazungu/waaarabu waliposhuka pwani zetu na majahazi yao.....kisha kudanganywa na gololi.....

Na unajua umbali toka Kigoma hadi Dar es Salaam ( Bagamoyo) ni kama Kilometer 1374 Hebu fikiria kundi la Waafrika kama mia mbili limefungishwa mnyororo na waarabu watatu au wanne tu, linatatembea kwa kwa mguu usiku mchana, maybe kwa miezi miwili hadi kufika Bagamoyo......kuingizwa jahazini kama makondoo......There is something wrong with our ancestors laana hii sijui imetoka wapi....! Leo hii tunawapa Bandari kwa kisingio tumeshindwa kuzuia wezi...!

Huwezi kumlaumu mzungu au mwarabu.....unaanza na mababu zetu.....to be specific babu yangu na babu yako.....
 

Una uhakika gani Ibrahim Traore hatakua kama Sargent Samwel Doe....Mohammed Siad Barre......Mengistu Haile Mariam....Sani Abacha.....Omar AL Bashir........Valentine Strasser..... Mobutu Sesse Seko.....Orodha ni ndefu mno....Hawa wote walitafuta majibu ya shida zao.....unafahamu matokeo.....!1
 
umeshaamua kwa hiari yako kuwa utakuwa mzalishaji cheap wa wazungu na mjenga nchi ya kizungu, lakini unaweza kusema idadi ya wafungwa gerezani inalingana na idadi ya askari gerezani? Idadi y mahabushi kwenye karandinga ni sawa na idadi ya askari kwenye karandika hilo? Babu zetu walikuwa mashujaa sana kuliko wewe ila walizidiwa tu na watu wachache wenye bunduki mikononi, kamba za kunyongea hadharani na kufungwa nyororo miguuni na shingoni, hata ungekuwa wewe ungefanya nini.

Na bahati mbaya sana watu hawa walikuwa wanauzwa na viongozi wao ndani ya jamii, hivyo hata kama ukitoroka msafara na kurudi nyumbani utakutana na kifo kutoka kwa machifu ambao walikuuza utumwani na utakamatwa tena na kusalimishwa kwa tajiri. Nilitembea kituo kimoja cha kumbukumbu ya watumwa pale Detroit, nilikosa usingizi kwa siku 5. Babu zetu walikataa fedheha ya kutumikia whites lakini vijana wao wa sasa wanahamasishana kwenda kuwafanyia kazi whites. Kizazi kimerudi nyuma kwa hatua nyingi sana, aibu ya karne hii. What are you looking for, money?!!!
 
Hawa wote unaowasema walisaidiwa na ex wakoloni wetu kupindua kwa faida ya wakoloni, Traore is a deferent case, wananchi wako nyuma yake na wako tayari yawafike mabaya pamoja na traore.
 
We Baki Tanzania unapotafuta fursa, acha wengine pia wakatafute fursa nje ya Nchi.
 

Malizia kabisa.....na Viongozi wetu wanauza Bandari...
 
Malizia kabisa.....na Viongozi wetu wanauza Bandari...
Kama vijana wenye kesho nyngi wameamua kuzikimbia bandari zao na kwenda kuwa manamba ng'ambo kwanini wazee wasiziuze? wacha ziuzwe ili sote twende marekani na ubelgiji tukatafute maisha, kaeni kimya subiri maombi yenu ya Greencard yajibiwe. Isiwe huku mwataka na kule mwataka.
 
Hawa wote unaowasema walisaidiwa na ex wakoloni wetu kupindua kwa faida ya wakoloni, Traore is a deferent case, wananchi wako nyuma yake na wako tayari yawafike mabaya pamoja na traore.

Hata Mwezi haujafika unasema Traore ni different case.....ndugu yangu Kavulata sasa umeakuwa mnajimu? .....Kuna mapinduzi ambayo wananchi wamewahi kuwa kinyume na Wapinduaji.....?Hata Uganda kipindi cha Idi Amin wananchi walitoka na kushangilia...... Kumbuka watu walivyofurahia ujio wa Samueli Doe.....! Mengitsu Haile Mariam....au umesahau historia? Tafadhali tunza maneno yako......tena inawezekana kabisa hao hao wenzake ndio watakao mgeuka.....!Hao wanamapinduzi huwa wanakuja na maneno ya Kimapinduzi.....wape mwaka tu......! Nigeria wamepinduana mpaka wenyewe wakachoka.....
 

Tutakula kote kote.......! Hujasikia uraia pacha...au vibali maalumu viko jikoni........
 

Kavulata, si heri kula jasho langu ughaibuni, kuliko kuwaibia Watanzania.....Jamaa zangu niliowaacha nyumbani, ambao wengi wako kwenye nyazifa za DED/RAS....Wakurugezi mawizarani nk.....wana pesa kufuru.....unajua wamezipata wapi? Wengine pesa za aina hiyo zilitushinda, dhamira zetu ziko hai..... na kama uzalendo ndio huo......basi siuwezi....! Tumewaachia watu kama wewe wenye Uzalendo......!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…