Mtu mwenye akili zote kichwani hawezi kushabikia kuwa economic refugee, badala yake anatumia akili, kipaji, nguvu na maarifa yake kuyageuza mazingira yake ili yamfae yeye na wengine, kila mtu lazima aache legacy kabla hajaondoka duniani, kama utashindwa kabisa kuacha uridhi mzuri kwa taifa lako angalau basi panda hata miti 2 tu ya kivuli kwenu ili watu wakukumbuke wakati wakijinga na jua kali.
Greencard na scheme nyingine za aina hii ziko mataifa ya Marekani, canada, Uingereza, Ufaransa na na nchi za Nordic. Leo lao kuu ni kuchukua bure nguvukazi ya mataifa maskini iliyokuzwa na kusomeshwa kwa taabu sana kwa kodi za nchi na watu maskini bila kulipa hata shilingi moja wala bila mikataba ya aina yoyote. Nguvukazi ya mamilioni ya watu inasombwa kwenda marekani na nchi nyingine kwenda kufanyishwa kazi mbalimbali zinazojenga uchumi wao.
Watu wa nchi hizo wanakataa kuzaana kwa kuogopa maisha magumu. Ushoga ni sehemu ya mkakati huo wa kukataa kuzaana, yaani mume anamuoa mume, na mke anamuoa mke ili mimba isitokee. Lakini ukienda kule marekani, pamoja na watu kukakaa kuoa, lakini hata hao wachache waliopo wengi wao wako jeshini wamesambazwa kwenye vikosi vilivyoko nje ya marekani karibu dunia nzima ili kulinda maslahi ya Marekani duniani kote.
Ni mtu mjinga tu anaesherehekea kuikimbia nchi yake, eti ameukata, yaani uzuzu wa starehe za kitumwa.