Naturalizations among immigrants from almost every country have rebounded since the pandemic started.
By
Alejandra O’Connell-Domenech | Dec. 02, 2022
Kavulata:
Mishahara yapaa tena
Viwango vya mshahara
Katika viwango hivyo vipya, mfanyakazi anayefanya kazi katika migahawa, nyumba za kulala wageni na baa atalipwa kima cha chini cha Sh150,000 kwa mwezi, hoteli za kati Sh180,000 na hoteli za kitalii atalipwa Sh300,000.
Mfanyakazi wa kazi za ndani ambaye haishi katika kaya ya mwajiri atalipwa chini ya Sh120,000, huku wale wasio katika kundi hilo watalipwa Sh60,000 kwa mwezi, huku wafanyakazi wa kazi za ndani walioajiriwa na Wanadiplomasia na wafanyabiashara wakubwa wakilipwa kima cha chini cha Sh250,000.
Wafanyakazi wanaofanya kazi katika huduma za mawasiliano watalipwa kima cha chini cha Sh500,000, wakati wafanyakazi wa huduma za utangazaji na vyombo vya habari, posta na usafirishaji vifurushi watalipwa kima cha chini Sh225,000.
Katika hoteli kubwa za kitalii, mfanyakazi atalipwa kima cha chini Sh300,000, hoteli za kati Sh180,000, huku katika makampuni makubwa na kimataifa huduma ya ulinzi wakilipwa Sh222,000 huku makampuni madogo wakilipwa Sh148,000.
Hali ikiwa hivyo katika sekta hiyo, katika sekta ya Nishati makampuni ya kimataifa watalipwa Sh592,000 na makampuni madogo Sh225,000, wakati katika sekta ya usafirishaji, wanaofanya katika huduma za usafiri wa anga watalipwa Sh390,000.
Katika sekta hiyo, wafanyakazi wanaofanya kazi za kutoa huduma za utoaji mizigo na usambazaji watalipwa kima cha chini cha mshahara Sh360,000, ilhali wale wanaofanya kazi katika huduma za usafiri nchi kavu ni Sh300,000.
Tangazo hilo halijawaacha nyuma makandarasi ambapo makandarasi wa daraja la pili hadi la nne watalipwa kima cha chini Sh360,000, huku wale wa daraja la tano hadi la saba wakilipwa kima cha chini ya mshahara cha Sh320,000 kwa mwezi.
Katika sekta ya madini, wenye leseni za uchimbaji na utafutaji madini wao kima cha chini cha mshahara kitakuwa Sh500,000, huku wenye leseni za wachimbaji wadogo kikiwa Sh300,000 na wenye leseni za wafanyabiashara kikiwa Sh450,000.
Huduma za shule binafsi kuanzia shule za awali, msingi na sekondari watalipwa kima cha chini Sh207,000, huku katika sekta ya biashara na viwanda wakilipwa Sh150,000 na Taasisi za fedha wakilipwa Sh592,000 kwa mwezi.
Sekta ya uvuvi na huduma za baharini wamepangiwa kima cha chini cha Sh238,000 kwa mwezi na sekta nyingine zote ambazo hazijaainishwa katika tangazo hilo la Serikali, wao watalipwa mshahara wa Sh150,000 kwa mwezi.
Sasa ndugu Kavulata, bila hata hata ya kujibu hoja zako, tangazo hilo la serikali limeniumiza mno! Sielewi kabisa kabisa watu namna hiyo wana mudu namna gani maisha!
Sina haja kabisa kufanya utafiti unaousema!
Nimekuletea huko nyuma kima cha chini kabisa Marekani! Na kwa sisi tuilokuja huku kama HUTATAKA kuishi maisha ya Kimarekani njia ambavyo pesa hiyo ni kubwa mno!
Na kwa taarifa yako sisi watu wa kuja huwa kazi za chini ni za kuingilia tu Marekani, hatuishi kwa kima cha chini! Hiyo ni ya wamarekani wenyewe! Sisi tumekuja kutafuta.
Nimeangalia kwa kima hicho, nimeona wazi maisha ya mtu ambavyo mbele ni giza kubwa kabisa! Na ili ufanikiwe Tanzania lazima uwe na tabia ya wizi, au kila njia isiyo halali ili uishi!
Kwa kifupi kabisa hebu nieleze Tsh 300,000 ni karibia $ 120! Hii ni pesa ndogo mno Marekani! Kwa kazi ya kawaida kiwandani ni pesa ya siku moja! Sasa utamkataza mtu kama huyo kujaribu kuja Marekani?
Wewe ndio unatakakiwa ufanye utafiti!