Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Naona hata nikikujibu napoteza muda bure , hoja za maana huna ni attacks tu.

Endelea kukaa huko hujalazimishwa kuja US na hivyo usiwalazimishe tuliopo na wanaotaka kuja waamini uongo wako.

Yaani kwa uandishi wa kuiita grocery kuwa ni glossary halafu ndio unataka tuendelee kujadiliana?
[emoji16][emoji16]
 
Hapo kwenye watoto kukaa chini darasani ndo umekuja kupoteza points zote. Umeonyesha ni kama unajaribu kufanya paonekane namna fulani tu na sio kwamba unaelezea hali halisi
Ndugu wewe hata huiijui Marekani kabisa. Wakati wa kampeni za Obama awamu ya kwanza Mimi hapa nilijaribu kuzunguuka nae huko vijijini kabisa kutaka kuifahamu Marekani vizuri, Kijiji kimoja alikuta shule ya serikali ambayo paa lake limeezuliwa na upeoo muda mrefu uliopita na madawati ni machache kuliko Idadi ya wanafunzi, hivyo wengine wakawa wamekaa chini. Jambo hili lilimsikitisha sana Obama akasema akiupata urais atatumia muda na hela nyingi kwaajili ya Marekani badala ya vita. Hii ndio iliyosababisha Obama akasitisha vita nyingi, akaanza kuchimba mafuta Yao badala ya kuagiza nje na kuanzishha Obama care, kukarabati shule za umma, na kuhangaika kukarabati miji ambayo ilitangazwa kuwa bankrupt Marekani. Usifikiri Obama care ilikuja kiboyaboya kama unavyodhani. Wewe nyamaza huijui Marekani.
 
Nimezoea kuishi nje! Kupapaswa ni wasio na elimu!
Wamarerani wengi hapa hawapendi kazi hizi tunazoiita regular Fox jobs kama zile za kwenye accomodations, restaurants na hospitality ambazo ndio nyingi sana Marekani. Wengi wako radhi waishi kwa Ile posho ya unemployment benefits kuliko kufanya hizo kazi za kimanamba, wengi pia wanaacha kazi mapema ili kupokea retirement benefits zao na kuondoka kuja kuishi Tanzania ambako hiyo hela ya pension inamtosha sana kuishi Africa na Asia, ndio maana kazi zinakuwa nyingi huko Marekani, hazioni watu sio kwamba watu hawapo ila hawazipendi, hawapendi kuwa manamba, hawapendi kuishi kwenye vision na missions za watu wengine kuanzia Jumatatu hadi jumapili, January hadi December kama kwamba wao hawana vision zao. Wewe njoo TU Marekani lakini utapishana njiani na wamarekani kunakuja Tanzania kuishi. Wanakuona bwege.
 
Wamerani wengi hapa hawapendi kazi hizi tunazoiita regular Fox jobs kama zile za kwenye accomodations, restaurants na hospitality ambazo ndio nyingi sana Marekani. Wengi wako radhi waishi kwa Ile posho ya unemployment benefits kuliko kufanya hizo kazi za kimanamba, wengi pia wanaacha kazi mapema ili kupokea retirement benefits zao na kuondoka kuja kuishi Tanzania ambako hiyo hela ya pension inamtosha sana kuishi Africa na Asia, ndio maana kazi zinakuwa nyingi huko Marekani, hazioni watu sio kwamba watu hawapo ila hawazipendi, hawapendi kuwa manamba, hawapendi kuishi kwenye vision na missions za watu wengine kuanzia Jumatatu hadi jumapili, January hadi December kama kwamba wao hawana vision zao. Wewe njoo TU Marekani lakini utapishana njiani na wamarekani kunakuja Tanzania kuishi. Wanakuona bwege.
Nasubiri majibu May 2023
Lengo langu wanangu wasiishie kupata elimu yetu ya Kanumba. I seek for their bright future!
 
Narudia tena kwangu hutapata airtime, maana huwa sifanyi illogical arguments na WAJINGA, ngoja nilale.
Wewe ndiye mjinga, umenaswa kwenye mtego wa manamba mamboleo una ujanja gani hapo tena. Wote tunafahamu kuwa Marekani ziko kazi nyingi kwenye ujenzi, estate, restaurants, hospitality, mashambani, udereva wa malori, uwalimu na Sasa IT, hii inajulikana tangu enzi hizooo hata mama yako hajazaliwa. Kuna kazi zilikuwa zinafanywa na wahamiaji wa kizungu TU, wamexico TU wakati ule wa Bracero program hadi mwaka ule 1965 walipokuja na sheria ya wahamiaji ya Immigration and nationality Act. iliyokuwa na lengo la kuchukua kila mtu duniani wa rangi yoyote mwenye ujuzi maalumu na mwenye elmu ya juu sana kote duniani (brain drain). Wewe unadhani kuwa ni bahati na sibu lakini ukweli hiyo sio bahati na sibu kwao. Wao tayari wameshakuwa takwimu kuhusu aina ya kazi zilizopo na idadi ya watu wanaohitajika kulingana na kazi zilizopo. Wewe zuzu ndiye unaedanganywa kuwa hiyo ni bahati na sibu. Kazi hizi haziwezi kukutajirisha wewe hata siku moja ili uendelee ku fanyakazi milele. Pesa yote inakuwezesha TU kulipa Kodi, kulipa madeni yako, nyumba na manunuzi ya chini kabisa. Hakuna anaekukataza wewe kufanya kazi huko lakini usidanye watu kuwa huko ni kuzuri kuliko Huku.
 
Bora huko mana hata mgao wa maji hakuna wala wa umeme!
Na hata ikitokea ajali ya ndege unajua uwezekano wa kuokolewa haraka ni mkubwa na sio usubiri kamba ikuvute!
Una uhakika?
 
Infact always I have an American dream.

There is no success like American success.

Nimejipanga nijaribu bahati yangu mwakani nicheze lottery ya Green Card natafuta nyezo tu muhimu mwakani must be.

Nina kazi but I ain't satisfied with my current position. And if kama nitaaendelea kubaki hapa I will die poor all red lights nimeshaziona.

So am seeking new challenges and new environment.

U never know may be something good will happen there.
Idadi ya Wamarekani wako 335 m hivi, Yaani ukiona Mmarekani 1 mwenye success ujue Kuna wamarekani 3m wameshindwa kuwa successful kwenye hilo eneo. Ukiona Kuna mwanamuzic mmoja anaimba vizuri ujue Kuna underdogs 10 m. Tz Ina miaka 61 TU tangu tupate Uhuru wakati Marekani Ina zaidi ya miaka 240 tangu ipate Uhuru, tuna tofauti ya miaka zaidi ya 180. Sasa fikiri miaka 180 iliyopita Marekani ilikuwaje.
 
Wakoloni walitusafirisha kwa majahazi kama watumwa kwenda kwao kuwafanyia kazi bure (manamba) kwenye mashamba, viwanda na majumbani kwao, history mbaya sana hii kukumbukwa, maana sio tu kwenda kuwafanyia kazi wazungu bure lakini wengi wao walikufa njiani wakati wakisafirishwa kwa kutoswa majini, msongamano mkubwa, njaa na ugonjwa njiani.

LEO hii miaka 60 baada ya uhuru sababu zilezile za kusafirisha manamba kwenda Marekani, Ulaya na uarabuni ndio sababu hizihizi za watu kwenda huko kwa Green card lottery, Jamani hali hii ni mpaka lini? what are you looking for? Kilichobadilika tu leo ni kitu kimoja tu kutoka manamba walionunuliwa kwenye masoko ya watumwa hadi kwenda kwa green card na baadhi ya sifa za watu wanaohitajika kusafirishwa na aina ya usafiri. Wakati ule walihitaji watu vijana wenye nguvu za kufanya kazi za wakati ule na sasa hivi kwa kutumia green card wanahitaji watu vijana wenye afya wenye elimu na ujuzi maalum kwaajili ya kufanya kazi za wakati huu.

Hii ni kujitafutia balaa wewe mwenyewe na familia yako kwa matumaini feki kabisa huku ukijua kuwa utakwenda kule kufanyakazi kubwa na nyingi sana ili upate chochote kitu wakati nguvu, juhudi na akili hizo ungeweza hata kuziwekeza hapahapa nchini kwako na kupata mafanikio makubwa sana ya ajabu pamoja na kutoa mchango kwenye ujenzi wa taifa lako kwa njia za kodi, tozo na huduma kwa jamii yako.

Jaamaani, Si shauri uombe hiyo kitu, nyambafu!!!!
Wew ni kiazi kama viazi wengine, jobless apate hiyo green card aache kwenda kufanya kazi ili abaki bongo kupiga story za Simba na Yanga wakati hana uhakika wa maisha
 
Ukinipa nafasi hata kesho ya kwenda states nakwenda Wala sijiulizi mara 2

Huyo kavulata ni kavulana Fulani labda ni silver spoon.

Hapa Tanzania labda uwe mwanga tu.

Na hivi waafrika hatupendana ndio kabisa
 
Narudia tena kwangu hutapata airtime, maana huwa sifanyi illogical arguments na WAJINGA, ngoja nilale.
huwezi kuukimbia unyonyaji kwa kumbilia kwenda kunyonywa tena. Umepoteza hadhi ya kuongea na wenye akili na maono juu ya taifa lao.
 
unakuta yeye mwenyewe mtoa post amecheza hiyo bahati nasibu
Niende wapi mimi? Hata wazungu wanapambana ndani ya nchi zao kupata hali bora, mbona hawaendi US kama hawa maboya wetu? ona hapa


 
Wewe usiombe ili ubaki bongo upige pesa mingi.
Wakati mataifa mengine yakiruhusu wananchi wao kwenda kuishi, kuchukua uraia na kufanya kazi kama manamba Marekani kama njia ya kusoma, kupata ujuzi, uzoefu na wizi wa technology za Marekani kwenye mambo tofauti sisi watu wetu wanakwenda kuwa manamba Marekani kama ya kukimbia ukosefu wa umeme, maji na hela mifukoni, kifupi wanakwenda kula bagger Mexican Pizza na hot dogs na kukaa kwenye mataa.

Marekani Leo inajuta kuwapa uraia watu wa Asia, China Sasa Iko juu sana kwenye kila nyanja.
 
Kavulata: Unajua unachokisema au umekaririshwa? Niko Marekani, sikuja kwa kufungwa mnyororo,na hata nikitaka kuondoka hakuna kamba iliyonifunga.
Ushauri kila siku kwa vijana wa kitanzania, kama unaona opportunities zimebana Tanzania jaribu popote, nina mifano mingi mno, na nimeona kwa watu toka mataifa mbali mbali niliokutana nao US!
Ukiwa na focus, na documents halali na yote unayoyasikia kuhusu Marekani, ni mahali unaweza kufikisha ndoto zako, sisemi ni rahisi, lakini kuna nyenzo ambazo hupati katika nchi nyingi za Kiafrica.
Sijahonga au kumuona yoyote watoto wangu kupata mikopo ya vyuo vyao, sikuwa na connection zozote zile watoto wangu kupata white color jobs! In short mtoto wangu alikuwa recruited akiwa bado chuoni, na leo akiwa na miaka24 is making almost $ 85,000/ Wenzake aliowaacha bongo waliomaliza chuo wanasaka ajira!
Sasa sijui ni utumwa wa aina gani huo!
Ni kweli Marekani/ Canada zinataka nguvu kazi, lakini ukiingia huku ni juhudi zako na akili yako! Wengine wataenda juu, na wengine chini, sawasawa na wazawa! Anayenifyekea majani nyumbani kwangu ni mzungu! Maana sina muda! Na kila baada ya wiki mbili au tatu ananipigia simu kama yameota aje kufyeka! Na ameniambia ni fundi katika serikali yetu ya mtaa anatafuta pesa ya ziada! Hii ndio Marekani, simdharau najua anachotafuta!
Hivyo usikaririshwe na akina Lumumba.
Hulazimishwi ni akili yako tu! Wengine wanatumia hapo bongo wanatoka! Wengine mambo yanakataa! Maisha popote pale!
Sijakaririshwa kaka yangu, umeamua mwenyewe kuwa manamba kwa hiari yako shida iko wapi hapo? nakataa vijana usiwaingize kwenye mtego bila kuwa na habari za kutosha. Angalia hawa hapa walikuwa wanapelekwa kwa nguvu walikuwa hawapendi, lakini nyie mnaenda wenyewe, what is the problem?
 
Dunia kijiji na mtu yyte mwenye fikra huru anaweza ishi nchi yyte anayotaka. Kwa kuzingatia sheria za nchi husika.. usipagawishwe na mipaka ya wakoloni!
 
Inaonekana unaijua US, Labda kwa stori za per Diem au ulikuwa mwanafunzi na visa ikaisha ukaogopa maisha ya kikunguru ukaamua kurudisha majeshi mavumbini, sasa kimewaka unaamua kuyananga maisha ya US kwa kuwa ulishindwa kupambana......
Haya karibu home, huku kuna ajira za uchawa, ni bora kuliko umanamba, lakini kama huna konekneshi utaendelea kujutia umanamba ulioukosa US kwa uwoga wa maisha.........
 
Dunia kijiji na mtu yyte mwenye fikra huru anaweza ishi nchi yyte anayotaka. Kwa kuzingatia sheria za nchi husika.. usipagawishwe na mipaka ya wakoloni!
Kubadili uraia kabisa Haina tofauti na "the door of no return"
 
Inaonekana unaijua US, Labda kwa stori za per Diem au ulikuwa mwanafunzi na visa ikaisha ukaogopa maisha ya kikunguru ukaamua kurudisha majeshi mavumbini, sasa kimewaka unaamua kuyananga maisha ya US kwa kuwa ulishindwa kupambana......
Haya karibu home, huku kuna ajira za uchawa, ni bora kuliko umanamba, lakini kama huna konekneshi utaendelea kujutia umanamba ulioukosa US kwa uwoga wa maisha.........
Si nimekwambia mm kule huwa ninaingia na kutoka nipendavyo, nafahamu uzuri na ubaya wa kuishi kule. Ninafahamu kuwa lengo la green card ni zuri zaidi kwa Marekani kuliko kwa anaepata hiyo green card, hakuna win-win bali win-lose. Watakulipa sana halafu wanazichukua sana vilevile wenyewe na kukuacha wewe ukiishi maisha ya kubana matumizi kupita kiasi. Hakuna working class anaetanua kule, hayupo, na hatakuwepo. Lengo ni moja kuwa ulazimike kwenda kufanyakazi utake usitake hata kama umechoka au unaumwa. Ukiumwa unakatwa posho.

Kuna wetu wengi sana wamepitia kwangu kwenda US kwa sababu mbalimbali na waliozamia huko wapo pia. Nina Ndugu wanaishi huko pia na ujumbe wangu ni huuhuu wa umanamba, wakatuma hela Huku najua inawauma sana maana nafahamu walivyoipata..

Kuna mzazi mmoja nilimkemea sana kupita kiasi. Alikuwa anatumiwa hela na mwanawe kujenga nyumba kigamboni lakini alikuwa anazila badala ya kujenga. Nikamuonya kuwa usishangae mwanao akaja kukupiga risasi, maana hella hiyo anaipata kwa shida sana.
 
Una akili nyingi sana wewe kuwaza kama hivi, hiyo ndiyo inayoitwa critical thinking. Yaani Marekani wanafaidika na nani kwa kuingiza majitu kwao, (motive behind). Jibu la swali hili ni njia nyingine ya kupata misukule ya kuwafanyia kazi zao kwa dezo.
Mnatakiwa mjue kuwa Kila aina ya binadamu yeyote yule anapatikana Marekani. Mchanganyiko huu ndiyo unaifanya Marekani iwe na maendeleo ya Hali juu zaidi. Kuchanganya akili za watu kutoka Kila pembe ya Dunia ndiyo faida yao
 
Mnatakiwa mjue kuwa Kila aina ya binadamu yeyote yule anapatikana Marekani. Mchanganyiko huu ndiyo unaifanya Marekani iwe na maendeleo ya Hali juu zaidi. Kuchanganya akili za watu kutoka Kila pembe ya Dunia ndiyo faida yao
Na ndionmaan halisi ya "Diversity" visa program
 
Back
Top Bottom