Kavulata: Unajua unachokisema au umekaririshwa? Niko Marekani, sikuja kwa kufungwa mnyororo,na hata nikitaka kuondoka hakuna kamba iliyonifunga.
Ushauri kila siku kwa vijana wa kitanzania, kama unaona opportunities zimebana Tanzania jaribu popote, nina mifano mingi mno, na nimeona kwa watu toka mataifa mbali mbali niliokutana nao US!
Ukiwa na focus, na documents halali na yote unayoyasikia kuhusu Marekani, ni mahali unaweza kufikisha ndoto zako, sisemi ni rahisi, lakini kuna nyenzo ambazo hupati katika nchi nyingi za Kiafrica.
Sijahonga au kumuona yoyote watoto wangu kupata mikopo ya vyuo vyao, sikuwa na connection zozote zile watoto wangu kupata white color jobs! In short mtoto wangu alikuwa recruited akiwa bado chuoni, na leo akiwa na miaka24 is making almost $ 85,000/ Wenzake aliowaacha bongo waliomaliza chuo wanasaka ajira!
Sasa sijui ni utumwa wa aina gani huo!
Ni kweli Marekani/ Canada zinataka nguvu kazi, lakini ukiingia huku ni juhudi zako na akili yako! Wengine wataenda juu, na wengine chini, sawasawa na wazawa! Anayenifyekea majani nyumbani kwangu ni mzungu! Maana sina muda! Na kila baada ya wiki mbili au tatu ananipigia simu kama yameota aje kufyeka! Na ameniambia ni fundi katika serikali yetu ya mtaa anatafuta pesa ya ziada! Hii ndio Marekani, simdharau najua anachotafuta!
Hivyo usikaririshwe na akina Lumumba.
Hulazimishwi ni akili yako tu! Wengine wanatumia hapo bongo wanatoka! Wengine mambo yanakataa! Maisha popote pale!