Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Mnatakiwa mjue kuwa Kila aina ya binadamu yeyote yule anapatikana Marekani. Mchanganyiko huu ndiyo unaifanya Marekani iwe na maendeleo ya Hali juu zaidi. Kuchanganya akili za watu kutoka Kila pembe ya Dunia ndiyo faida yao
Sure, but you have to think globally then act locally. Yaani twendeni huko tukaibe maarifa na mitaji kisha turudi kwetu kutengeneza vya kwetu kwaajili yetu na watu wetu. Laana ni kuzamia na kuwatelekeza your own people. Wakati tunawafundisha watoto wa wazungu kwenye vyuo vyao tukumbuke watoto wetu nyumbani hawana walimu pia. Wakati tunapangauza wazee wa kizungu matakoni tukumbuke hata wazee wetu Wana shida hiyohiyo.
 
Huyu dogo ni kvma take an example ya Nigerian diaspora mwaka Jana wametuma remittances worth 20 USD billions kila mwaka ,kuanzia January yaani first half ya mwaka huu nigeria imeingiza 11billions of USD kama remittance za watu wake walioko nje ya nchi ,hiyo ni nusu ya mwaka tu . Tafuta ni economic sector ipi nigeria inacontribute kiasi hicho cha pesa kwenye GDP na economy ya nigeria Kwa mwaka .
Majirani zetu Kenya wao hutuma 4.9 bil kwa mwaka

Tanzania 500mil usd kwa mwaka.

Taifa letu ujinga mwingi sana
 
Naomba mawasilino yako ole wako nikute unakaa kwa dada ako au nyumbani
 
Hivi Kuvulata unasoma notes nini? Maana ni kama mtu aliyeko Marekani anaposoma notes za poverty ya Africa, nimesoma development economics, najua kutumia data ziseme nachotaka kusema!
Anyway kwa kukutarifu niliingia Marekani kwa Greencard, na nimechukua uraia wa Marekani kwa hiari yangu! Sikulazimishwa!
Siku ya kuapishwa kuwa raia, ofisi zilifunguliwa asubuhi na kufungwa jioni,kulikukuwa na makundi makubwa mno ya watu! Cha ajabu waafrika tulikuwa sana! Maybe 2% Mchanganyiko toka nchi mbali mbali,Brazil, China,Korea, India, Mexico...Ulaya nk! Nchi ambazo hawajawahi hata kuchukuliwa manamba! Hivi hao wote ni wapuuzi!
Na kwa taarifa tu,ukisikia illegal immigrants,Waafrika ni aslimia ndogo kabisa! Na hata number ya legal immigrants toka Africa, number yetu ni ndogo mno!
Watu wanatoka sehemu mbali mbali za dunia kuingia US! Wenye pesa kuja kuweka investments zao, na wengine kutafuta wanachokitafuta!
Kijana wangu marafiki zake chuoni walikua toka Italy, Korea na India, wako IBM,Google! Wote ni wahamiaji!
Walimaliza University hata hawakusubiri ajira!
Kama huo ndio umanamba,watched wawe manamba!

Tatizo wanajidanganya, USA wanaiona kwenye TV. Ile ni land of opportunity lazima mjue.
Everybody can be a winner.
Issue ni vibari tu
 
Huyu mdau humu nimegundua ni mtu ana akili timamu ila anatumiaga bangi.
Tusimtupe tumshauri vizuri atapata akili.
Mambo ya umanamba ni ulivyomezeshwa kwenye historia, ni sawa na mama ako akwambie baba ako mtu mbaya baada ya kugombana nae.
 
Mnatakiwa mjue kuwa Kila aina ya binadamu yeyote yule anapatikana Marekani. Mchanganyiko huu ndiyo unaifanya Marekani iwe na maendeleo ya Hali juu zaidi. Kuchanganya akili za watu kutoka Kila pembe ya Dunia ndiyo faida yao
kinachowafanya waendelee ni watu kufanyakazi kama punda bila kukwepa kulipa kodi. Watu wanajinunulia kila kitu kuanzia matibabu, elimu na haja kubwa. serikali haina kitu, vitu vyote ni mali ya mabepari wanaofanya watakavyo, unalipwa zaidi lakini wanazichukua zaidi tena wao wenyewe.
 
Ninawaangaliaaa kisha ninacheka sana namna vijana wetu wanavyoendelea kunasa kwenye mitego ya akina Karl peters mamboleo hadi Leo. Tunaonekana kubaki na akili zilezile za akina Mangungo hadi Leo, green card Haina tofauti na zile shanga, vioo, baruti, goroli, bunduki dhaifu za magobole walizokuwa wanatumia akina Karl peters kuwapa akina mfalme Mangungo ili kupewa ardhi, madini, watumwa, meno ya tembo na faru na kila kitu Cha thamani kuwapa wazungu. Marekani hakuna kitu Cha Bure hata kimoja na kila mtu ana deni analotakiwa kulilipa kila siku hadi anakufa. Hakuna anaefanikiwa kukwepa Kodi, na huwezi kuhamisha fedha zako kwenda nyumbani kwenu unakotoka, ukifanya hivyo utatandikwa pesa nyingi sana kama ushuru wa kutumia fedha hivyo. Yaani wanadiscourage kusyphone fedha kutoka Marekani.

Tofauti yetu waafrika na mataifa mengine kama wachina, wahindi, wajapan, wakorea ni kwamba wao wanafanya kazi nzuri na muhimu wakati watu wetu wengi wako mashuleni wanafundisha, mashambani wanalima na kuchunga, madukani wanauza na kubebea wateja mizigo, wanauza kwenye hardwares na glossary, kufanya usafi kwenye sekta ya nyumba na mazingira na hospitality.

Mataifa mengine kama wahindi, wachina, wakorea, wajapan, nk kazi Yao muhimu kule ni kuiba technology (electronics, automobile, civil, kijeshi, viwanda,nk) kwenye maeneo wanayofanyakazi za kuzirudisha kwao wakati watanzania kazi yaa muhimu kule ni kutafuta kila njia wawe raia watiifu kabisa, kupata wanawake na wanaume, kujenga vijumba hata kwa kutumia mbao TU, hopeless. Nyumbani anarudisha kidoooogo sana tena kwa taabu sana na shingo upande.

Kijana wangu aliambia baba nimejenga huku, nikasema waooow, nikaenda kumtembelea siku moja nikakuta amebandikabandika mbao kama Kuta na kuezeka mabati. Kimoyomoyo nikasema lahaulaaa!!!!
 
Wakoloni walitusafirisha kwa majahazi kama watumwa kwenda kwao kuwafanyia kazi bure (manamba) kwenye mashamba, viwanda na majumbani kwao, history mbaya sana hii kukumbukwa, maana sio tu kwenda kuwafanyia kazi wazungu bure lakini wengi wao walikufa njiani wakati wakisafirishwa kwa kutoswa majini, msongamano mkubwa, njaa na ugonjwa njiani.

LEO hii miaka 60 baada ya uhuru sababu zilezile za kusafirisha manamba kwenda Marekani, Ulaya na uarabuni ndio sababu hizihizi za watu kwenda huko kwa Green card lottery, Jamani hali hii ni mpaka lini? what are you looking for? Kilichobadilika tu leo ni kitu kimoja tu kutoka manamba walionunuliwa kwenye masoko ya watumwa hadi kwenda kwa green card na baadhi ya sifa za watu wanaohitajika kusafirishwa na aina ya usafiri. Wakati ule walihitaji watu vijana wenye nguvu za kufanya kazi za wakati ule na sasa hivi kwa kutumia green card wanahitaji watu vijana wenye afya wenye elimu na ujuzi maalum kwaajili ya kufanya kazi za wakati huu.

Hii ni kujitafutia balaa wewe mwenyewe na familia yako kwa matumaini feki kabisa huku ukijua kuwa utakwenda kule kufanyakazi kubwa na nyingi sana ili upate chochote kitu wakati nguvu, juhudi na akili hizo ungeweza hata kuziwekeza hapahapa nchini kwako na kupata mafanikio makubwa sana ya ajabu pamoja na kutoa mchango kwenye ujenzi wa taifa lako kwa njia za kodi, tozo na huduma kwa jamii yako.

Jaamaani, Si shauri uombe hiyo kitu, nyambafu!!!!
kati ya wengi wanaokwenda huko wachache sana (pengine chini ya 3%) wanarudi wakiwa wamefanikiwa wengine wengi hata kurudi nyumbani likizo wanaona aibu. Kitu pekee walichofanikiwa ni kujifanya wamesahau kuzungumza kiswahili
 
Majirani zetu Kenya wao hutuma 4.9 bil kwa mwaka

Tanzania 500mil usd kwa mwaka.

Taifa letu ujinga mwingi sana
Daah!! ni heri aliyefilisika mfukoni kuliko aliyefilisika fikra. Kenya Iko bankrupt hata mishahara kwa watumishi wake ni tabu kulipa ndio unaifananisha na tz. Yaaani kufirwa na umanamba ndio unasifia? Guys, tz zipo fursa nyingi sana kama una akili timamu.
 
kati ya wengi wanaokwenda huko wachache sana (pengine chini ya 3%) wanarudi wakiwa wamefanikiwa wengine wengi hata kurudi nyumbani likizo wanaona aibu. Kitu pekee walichofanikiwa ni kujifanya wamesahau kuzungumza kiswahili
Sasa nenda Marekani na ujifanye unawaaga kuwa unarudi tz mara moja, weeee!!! Kila mtu anataka akutume kwao, vijana wengi wanateseka sana huko ughaibuni wanafanya kazi yoyote hata ikibidi kufirwa ili wapate maisha.
 
Namshulu mungu nimechaguliwa kuendelea na mchakato, naomba msaada Kwa ambae anafaham zaidi aniekekeze.
 
Watu wakichoka na maisha hapo bongo, kuibia ukitoka kazi unavamiwa ukiwa kwako wanaiba vitu dirishani,
Ukicha gari umepaki nje kesho utakuta boshen tu.
Huku unavamiwa unachomwa visu,chupa etc.
Ukikaa bar majambazi yanakimbizana huko yamepora mnaambiwa wateja wote mlale chini mnaibiwa kila kitu.
Hayo maisha gani?
Mnaamua kuhama tu ili angalau muokoe uhai.
 
Back
Top Bottom