GSM anaachana na yanga kwasababu ya wajumbe hawa

GSM anaachana na yanga kwasababu ya wajumbe hawa

Yanga mbona mnakuwa wanyonge sana. Mi nawaunga mkono kina Gumbo. Yanga ni taasisi haiwezekani mtu anajifanyia utaratibu pembeni. Kama anania njema kwa nini asifuate utaratibu. Hili jambo litakuja kuwagharimu siku moja. Kwa mfano angejitoa mazima,wachezaji wake angewalipa nani.
Naunga mkono hoja.
 
Yanga inawadhamini wengi, SportPesa akiwa mdhamini mkuu. GSM udhamini wake ni kwenye jezi, ila alichoamua kufanya kama msaada nje ya mkataba ndio kilichohojiwa na kuleta mgogoro.

Kwa maoni yangu GSM wanatumia nguvu yao ya pesa kufanya yasiyo wajibu wao na wao kutamkwa zaidi kuliko wadhamini wengine.

Na hata ukimsikia Nugaz msemaji wa Yanga amekuwa kama msemaji wa GSM zaidi akisifia brand yao kuliko wadhamini wengine.

Pia kutoa pesa zao nje ya mfumo rasmi wa club kuna leta harufu ya utakatishaji pesa kwa njia hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nugaz anaipamba sana GSM nahisi analipwa kwa hilo, ndiyo maana anashindwa kubalance shobo
 
Back
Top Bottom