Kwanza kabisa napenda niwatakie Sabbatical njema, pili leo ni Nyerere day, nitamuenzi baba wa Taifa kwa njia hii.
Kwanza naomba nikiri huyu Zari mimi namsikia jina tu sijawahi kujuwa hasa kwa hakika shughuri zake ni nini zaidi ya kujuwa ni hawara wa msanii Diamond that's it.
Huwa sina muda wa kudiscuss drama za watu wa aina hii lakini kwakuwa hili la zari lipo in economics grounds naomba nitowe maoni yangu.
Kwa maoni yangu ni dharau kwa Watanzania GSM kumleta Zari kuzinduwa hilo duka lao la Danube nadhani kwa maoni yangu mtu sahihi walipaswa wamuite Diamonds kufanya uzinduzi huo
Kwakuwa Watanzania sasa hivi ni mashabiki ushuzi wa Team ushuzi hawawezi kunielewa wala kukubali kitendo hiki ni dharau kubwa imefanywa na GSM dhidi ya models wetu, kumleta mganda halafu utegemee wateja Watanzania huu ni ufala uliopitiliza.
Binafsi yangu natangaza rasmi boycott bidhaa za duka hilo la Danube kwa kitendo hiki cha kutowapa support models wetu kufanya jukumu hilo.
Tunao kina Mbwana Samatta, Flavian Matata, yupo Joti yupo Masanja, yupo mzee Majuto why Zari? Zari ni Celeb wa nini jameni naomba kujuzwa.
Team ushuzi unaruhusiwa kujaza omo mdomoni ukaja na mapovu hapa.
Mazee.
Kwanza mimi sina team zaidi ya kuwa "team first principles".
Umeandika vizuri kwamba huna ushabiki na mtu, umeleta hili kwa sababu linaingia katika uchumi.
Tuongelee uchumi. Turudi kwa Adam Smith kuja mbele.
Hapa nakuja na darasa la uchumi, natumia kanuni za "free trade". Sipendi protectionism. Protectionism inaleta "trade wars". Ukizuia watu wa nje kufanya biashara Tanzania, na wao wakilipiza hivyo hivyo kwao, Watanzania tunaofanya biashara nje tutapata tabu sana.
Biashara ya soko huria inawaruhusu kumleta model wa popote.
Wamarekani wangeleta kijiba wa support models wao tu, Flaviana Matata asingekuwa model wa kimataifa Marekani.
Wabelgiji wangesema wa support wachezaji wao tu, Mbwana Samatta asingekuwa anacheza Genk.
Waache watumie uhuru wao wa soko huria.
Na wewe tumia uhuru wa wallet yako kuwasusia kama hupendi wanakichofanya.
Kama mpo wengi hampendi na mna protest, watapata ujumbe na kuwasikiliza. Mnayo haki hiyo kupitia kanuni za demand and supply.
Mimi nishapeleka biashara zangu Kabalagala Kampala. Nisingependa kuona Waganda wanawasusia Watanzania biashara eti kwa sababu ni Watanzania tu.
Hujui maelewano yao yakoje. Waache wafanye wanavyoruhusiwa kwa kanuni za soko huria na sheria.