Naona hapa uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora kwenye hii mechi ya Kmc na Simba, hamna bango hata moja Au ndo mmeona msihangaike kwenye mechi za Simba kuyaweka? Kwa jinsi Mashabiki wa Simba walivyo jaa, wangeweza hata kuyachana, Bora mmejiongeza!
Kwenye mechi yoyote ya ligi kuu, kwa uchache kunatakiwa kuwa na mabango kadhaa kuwekwa uwanjani.
1. Bango la shirikisho.
2. Bango la logo ya ligi
3. Bango la wadhamini wa ligi (mdhamini mkuu, mdhamini mwenza, mdhamini anayeonyesha ligi kwa TV na mtangazaji kwa njia ya redio).
4. Bango la mdhamini binafsi wa klabu mwenyeji.
Katika hayo yote hapo juu, sio kazi ya mdhamini kwenda uwanjani "kusimika mabango".
Hiyo ni kazi ya timu mwenyeji wa mechi husika.
Mdhamini anazikabidhi timu zote kupitia bodi ya ligi, kitu kinachoitwa "vifaa" yakiwemo mabango, nembo n.k.
Kazi ya mdhamini inaishia hapo.
Kama uko serious kwenye huo uzi wako, nadhani unatakiwa kulifahamu hili.
Vinginevyo uwe ulikua unatania tu.