RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 4,707
- 11,365
Mnahamisha tena magoli,Pep kawafata kwenye ligi yenu nakawabamiza nyie wote,halafu oooo pep hamna kitu wenye kitu ni Klop na Mourinho basii.Usiingize topics off subject sijui cha liverpool Ama Man U
Utampamba sana Pep wako
Lakini ukweli unabaki kuwa hajafanya lolote jipya likaitwa maajabu
Mnahamisha tena magoli,Pep kawafata kwenye ligi yenu nakawabamiza nyie wote,halafu oooo pep hamna kitu wenye kitu ni Klop na Mourinho basii.
Unaposema mashabiki wengi wa Chelsea hawajui soka kwa vile wameanza kuishabikia timu hiyo 2005 it doesn't make sense at all.
Kwani baada ya 2005 hakukuwa na soka?kulikuwa na nini? Klabu ngapi zimefanya makubwa katika ulimwengu wa soka from 2005 to date? Wachezaji wangapi wamefanya makubwa katika ulimwengu wa soka from 2005 to date? Makocha wangapi wamefanya makubwa katika ulimwengu wa soka from 2005 to date?
By the way kwa umri wangu ni sahihi kabisa kuishabikia Chelsea kwasababu tangu nianze kuishabikia Chelsea nimeshuhudia ikibeba EPL back to back and 5 times in total,4 FA cups,3 League Cups,UCL na Europa League that's 14 trophies in total so najivunia kuwa mshabiki wa hii timu na naweza kwenda mbali zaidi na kusema mimi ni mshabiki mzuri wa soka kuliko unavyofikiria na mambo mengi ya huko nyuma nimejaribu kufatilia baada ya kuanza kuutazama mchezo huu kwa mara ya kwanza 2002 World Cup.
Back to the point,Nadhani una tatizo la uelewa au unaongozwa na mihemko bila kujijua kwasababu hapo juu sijazungumza mafaniko ya Guardiola katika EPL na kwingineko nimezungumza rekodi zake alizofanikiwa kuweka katika Ligi tatu kubwa duniani so far.
Katika EPL kila kocha ana rekodi za peke yake na zinaheshimika,tukianza na SAF ana rekodi ya kuchukuwa ubingwa wa EPL mara tatu mfululizo(2006-2007,2007-2008 na 2008-2009).Arsene Wenger ana rekodi yake ya kuchukuwa ubingwa bila ya kupoteza mechi hata moja msimu wa 2003/2004.Mourinho ana rekodi yake ya kuchukuwa EPL kwa Points nyingi zaidi,95 points msimu wa 2004/2005.Conte ana rekodi yake ya kuchukuwa ubingwa wa EPL kwa kushinda mechi 30 kati ya 38.
Hizi zote ni rekodi na zinaheshimiwa maana ni CV tosha ya Kocha hivyo kama una criticize rekodi ya Guardiola hadi hapo atakapochukuwa ubingwa basi lets meet in May uje kumpa heshima yake kwa kuchukuwa ubingwa na kuweka rekodi yake ambayo wengine hawakuweza kuifikia hapo nyuma,18 games winning streak.
Plus Conte si kocha wa kwanza kubeba EPL katika msimu wake wa mwanzo hata Mourinho alifanya hivyo akiwa na Chelsea msimu wa 2004/2005 vile vile Carlo Ancelotti alifanya hivyo akiwa na Chelsea msimu wa 2009/2010.
Na unaposema ili tumpe credit achukue UCL back to back nazidi kuwa na wasiwasi na uwezo wako kuuelewa mchezo wa mpira.Hivi apart from Zinedine Zidane kuna kocha aliyewahi kuchukuwa UCL back to back tangu wewe uanze kutizama mpira? Kwahiyo hawa akina SAF,Mourinho,Ancelotti,Vicente Del Bosque,Frank Rijkaard,LVG,Juup Heynckes,Benitez,Di Matteo na wengineo hawa deserve credit kwa vile hawakuweza kuchukua UCL back to back?
Umeandika upupu mwingi nahakuna cha maana ulichoandika.
Nyie ndio mlisema Pep anashinda mechi nyingi kwenye ligi dhaifu,hawezi kufanya EPL.Sasa mnapouliza Pep hawezi kufanya hivyo EPL mnabaki mnaandika utumbo ambao hauna maana.
Mmeulizwa hawezi kuzifunga timu za EPL kama alivokuwa anafanya huko kwenye ligi dhaifu?.Jibuni acheni kuhororoja.
Ndio mkuu nilikimbia umande,niliishia darasa la nne,hongera wewe uliemaliza madarasa hata kuitwa Prof,lakini nikwambie kitu acha kuandika upupu ambao kila mtu anaufahamu,maana unaonekana ulivo na takataka nyingi kichwani.Hivi Wewe Unajadili Nini? Na Unajadiliana Na Nani?
Mbona Nakuona Unaandika vitu kama uliyekimbia umande!!
I'm not your level, Just find someone else may be you can gain some knowledge about aoccer
Acha kujitia upofu usiokuwa nao au tatizo lako la uelewa linazidi kujidhihirsha?Labda Nikuulize Back-to-Back ipi unayoikusudia Hata Ukasema Ni Zidane Pekee Ndiye Aliyebeba?
Coz Waliowahi Kubeba UCL B2B kuna REAL, BENFICA, INTERMILAN, AJAX, BAYERN, LIVERPOOL, NOTINGHAM FOREST na AC MILAN.
Au Unahisi UCL imeanzishwa 2005 kama ilivyoanzishwa timu yako?
"MPAKA HAPO NIMALIZIE TU SINA CHA KUKUSAIDI TENA"
View attachment 665289
Mnahamisha tena magoli,Pep kawafata kwenye ligi yenu nakawabamiza nyie wote,halafu oooo pep hamna kitu wenye kitu ni Klop na Mourinho basii.
NITAKUJA TENA KWENYE UZI HUU JANUARY 14
hapo sasa EPL watajipigia hutoaminiIla liverpool ni mwanaume jamani, bikra ya man cty imetoka leo
Nadhani watu wengi tunakumbuka ile Barcelona ya 2009-2012 ambayo kwa wengi ni timu bora kabisa katika kizazi hiki cha soka, kuanzia ugawaji wa vipigo,kandanda safi na uwezo binafsi wa wachezaji.
Wakati Guardiola akiiongoza Barcelona kugawa vichapo vya hatari hadi kumtetemesha mzee wetu Ferguson kwenye fainali ya Uefa 2011 wengi walikuwa wanammbeza kwa kusema anacheza ligi ya timu 2, ooh mara kabebwa na messi, wengine wakasema ana bahati.
Guardiola akaondoka zake kwenda Bundesliga, huko nako akagawa vichapo vya kutosha, ila wadau wa England wakaendelea kumponda kuwa anaiogopa England maana sio size yake [emoji23](wakajisahaulisha kilichokuwa kinazikumba timu za England zilipokutana na Barcelona).
Haya sasa , mara Guardiola akaja hapo England, ni kweli msimu wa kwanza hakufanya vizuri ila wadau wa England wakatamba sana eti alidhani yupo la liga au ligi nyingine nyepesi, hii ndio England bwana, timu zote kali!!!!
Msimu wake wa pili, akaanza kwa kasi ndogo, wakaongea sana,alipoanza kugawa vichapo wakasema ngoja tumuone, hawezi fika mbali hii ndio England, mara kashinda game 10 mfululizo, akashinda nyingine 5(still counting), humo kagawa vichapo na kuupiga mpira mwingi mno ikiwemo nyumbani kwa timu vigogo kama Man untd na chelsea.
Sasa hivi England ni ligi ya timu moja tuu, Man city imegeuka kama msalaba wa jumuiya ambao unapita kila nyumba, Guardiola hajawahi kuwa na timu iliyokusanya pointi nyingi hivi ndani ya mechi 16 za kwanza, cha kushangaza huku ambapo Guardiola anajipigia tuu watu ndio tunaambiwa ni ligi ngumu lakini kule ambapo alikuwa na timu ya Dunia alikuwa hashindi hivi tunaambiwa ile ligi ni mbovu/rahisi.!!
Kinachotokea sahizi si kingine bali ni E.P.L kuumbuka, tayari Pep amejipigia vigogo wote wa E.P.L wengine kwa aibu ya goli 5....,tungojee mwisho wa msimu tuone mambo yatakuwaje ila nina uhakika Man city watachukua ubingwa