Chalii alipata utajiri wa ghafla sana alafu alikuja kijana tu miaka 40
Aisee kama ndo vile tuishi maisha ya uhalisia
Tutafute vya halali
Kwasababu hata historia yake kuna sehemu wanaruka yaani pale ambapo ameanza kua bilionea wanaruka yaani wanasema hatimaye amekua tajiri😂😂😂hapo katikati wanaruka maana kuna mambo mengi sana hawayajui wachambuzi
Jamaa ana magari ya kifahari ya gharama sana karibia 10 ya aina moja yaani hzo hela zake unatumia kwa vizazi laki 1 vyako
Niliona sehemu jamaa alikua anaelezea kwa mafumbo ila ilikua inamuhusu mwana huyo
Pia anasema yeye ni "self-made millionaire", yaani milionea aliyejijengea utajiri wake mwenyewe.Ni myth tu, kama huo utajiri upo kweli, nafikiri vijana wengi Africa kuanzia East Africa na mahala pengine kungekuwa na mabilionea wa hatari...
Maana kuna vijana wana roho ngumu balaa na wapo tayari kufanya lolote kwa ajili ya pesa...
Hii Tanzania yote ukiacha watoto wa viongozi sidhani kama kuna kijana ana miliki private jet...
Alikua anafanya biashara gani kwaniJamaa alikuwa anajiita self made millionaire
Umemjua lini Chivayo?Lakini fedha zilikuwa zinatoka wapi kufadhili biashara zake?
Hili ndilo swali ambalo Chivayo alikuwa akikabiliwa nalo mara kwa mara.
Yeye si mtu anayependa sana mahojiano na waandishi wa habari. Ameeleza pia hapo awali kwamba hapendi waandishi wa habari.
Lakini katika mahojiano machache aliyofanya kwenye kipindi cha redio cha asubuhi mwaka 2024, aliulizwa swali hilo moja kwa moja.
Jibu lake lilikuwa kwamba biashara yake kubwa inahusu zabuni za serikali anazopata kwa kushirikiana na washirika wa kigeni.
Alitaja sekta za nishati jadidifu, uhandisi, ununuzi na ujenzi pamoja na miradi ya umeme.
Pia alisema ana biashara nchini Kenya, Afrika Kusini na Tanzania.
Kwenye Instagram, Chivayo amekuwa akizungumza kwa kujiamini zaidi kuhusu mafanikio yake.
Anajiita "hustler" - mtu anayepambana na kufanya kazi kwa bidii.
Pia anasema yeye ni "self-made millionaire", yaani milionea aliyejijengea utajiri wake mwenyewe.
Anarejea maisha yake ya utotoni huko Chitungwiza, mji ulio karibu na Harare, ambako anasema familia yake ilipitia kipindi kigumu baada ya baba yake kufariki alipokuwa na umri wa miaka 10.
We wakishuaHakuna utajiri wa kishirikina.
ungekuwepo kila mtu angeenda kuutafuta hakuna mtu anaependa kuwa maskini.