Mimi siko hapa kubishana wala kumwaminisha mtu cho chote lakini ninachokisema mwenyewe nimekishuhudia. Kama kuna mtu yupo * au aje hata kesho nimpeleke kwa bibi mmoja anaitwa **. Aje na sarafu moja nyeupe, kioo kidogo na kipande cha mnyaa basi. Malipo ni baadaye sana! Na akibahatisha mara nyingi masharti yake wala siyo magumu kivile na hayahusishi makafara wala nini.
Mfano huyu dogo niliyemtaja kwenye post hapo juu alipewa sharti moja tu la kutosema alichokiona. Aliambiwa aende sehemu kilimani usiku wa manane kuna jiwe kubwa. Pembeni yake kuna kama pango hivi. Aingie humo akiwa uchi. Humo pangoni atakutana na watu watatu na watampa kitu fulani. Halafu hao watu watammwagia kimiminika fulani kichwani. Yeye akipokee hicho atakachopewa na kimya kimya aondoke humo pangoni bila kugeuka nyuma. Sharti lilikuwa moja tu: Kamwe asije akamwambia mtu ye yote alichokiona wala kukisikia humo pangoni mpaka siku anakufa. Dogo akajiripua akatimiza masharti yote. Katoka chuoni na Bachelor of Law wala hana ajira akaja hapa machimboni kumbe anazuga tu. Dhahabu tayari alikuwa nazo. Kumbe ndicho alikuwa amepewa kule pangoni. Aliuza akapiga kama 2.8 bilioni hivi na hakuuza zote. Range Rover. Kahoteli kamoja kakali. Na akaingia rasmi kwenye buashara ya kununua na kuuza dhahabu. Akawa digala. Akaanza na kukopesha pesa. Zile za moto. Watu wa kwenye machimbo wanajua!
Bibi kumbe alimwambia asinywe pombe ili kulinda siri yake. Aaaa wapi. Pesa zinawasha. Pombe tena zile kali. Pisi za kila aina...kumbe siku moja akajisahau, pengine sababu ya pombe, akatoa siri. Hata hajui alimweleza nani. Na sasa tayari kimeumana vibaya sana. Kifupi ameuza kila kitu: magari, nyumba zote.... Kumbe anatakiwa kurudisha kila kitu - tena kule kule pangoni alikochukulia. Sijui kuna vitu gani vimepungua maana mpaka ndugu zake wanachangishana. Akisharudisha kila kitu inabidi arudi tena kwa yule bibi ili mwili ukasafishwe upya. Pengine ndiyo aanze tena harakati upya. Akishindwa kurudisha mali za watu kule pangoni basi watapita naye. Na deadline ameshapewa!
Ukiambiwa haya mambo utafikiri ni muvi kumbe yapo na yanatokea. Kwenye madini huku mh!!!