Mwanzo mzuri, hongera sana. Ushauri wangu katika kuboresha zaidi:
1. Nakushauri kuwa uende mbali zaidi, iongezee "value" idea yako... How? Kwa mfano, ishu kubwa sana ya online business kwa Tanzania kwa sasa ni TRUST; Watu wengi sana wanapigwa (pande zote, wauzaji na wanunuaji), can your site solve this issue? If the answer is YES, you are a billionaire in the making. Fikiria kuhusu hilo, how will you solve the trust issue ya online business kwa bongo kwa kupitia site yako? That should be your VALUE. Na hiyo ndo inakua SELLING POINT ya site yako, hata kwenye matangazo, unakua unaongelea kuwa YOU BRING TRUST TO THE ONLINE BUSINESS.
2. Mpangilio wa rangi: Nashauri uangalie kwa makini mpangilio wa rangi kuu za site yako-Kwa sasa naona mpangilio huu bado unahitaji maboresho zaidi. Jaribu kujisomea zaidi na kutafiti zaidi juu ya combination za rangi kwa ajili ya kuongeza mvuto na kuipa utulivu website yako.
3. Jina-Jaribu kutafuta jina ambalo litakua ni rahisi, linalokumbukika kirahisi, na pia ambalo linaleta mtazamo chanya wa site yako. Hii inahitaji muda hata hivyo, kwa hiyo tulia, uendelee kuangalia namna ya kuboresha zaidi. Fikiria kwa mfano jamaa waliotengeneza sabuni ya OMO; Hivi walifikiria nini kuiita sabuni yao OMO?
Otherwise, hongera kwa udhubutu, kazi nzuri sana!
keneddelly