Gwajima: Kutakuwa na Ugeni wa mzee kutoka kijiji cha KOROMIJE

Gwajima: Kutakuwa na Ugeni wa mzee kutoka kijiji cha KOROMIJE

Najua Mchungaji Josephat Gwajima upo hapa JF
Tumepata taarifa jumapili ijayo kuna wageni watatoka Kolomije village kuja kuongea na familiya ya wana Ufufuo,tumesikia wengine ni waalimu waliomfundisha Mh makonda na wengine ni wanakijiji.

Naomba nikuombe neno moja,samehe na kusahau kwa kuwa ndio tulioitiwa,waendao katika mwili hawawezi kumpendeza Mungu,wewe ni MTU mkubwa katika jamii na unaheshimika,hivi unaweza kufundisha somo LA kumsamehe adui yako?

Naomba uwe mfano wa kuigwa ili usipoteze kondoo unao waongoza,kumbuka maneno ya Yesu,akulazimishae kutembea maili moja tembea nae mbili,na akuny,ang,anyae koti mwachie na shati.
Watu wangekuwa na mawazo kama yako mpaka leo hii tungekuwa tunatawaliwa na mkoloni au idd amini angekuwa bado yupo madarakani na angekuwa analishikilia eneo aliloteka tanzania na tungemuongezea kwa kufuata maneno yako
 
Gwajima,waumini wake na walimu pamoja na wanakijiji wa kolomije watakao kwenda ni mafyatu...

Gwajima sio muda atakuwa kama kakobe!!
 
Waumini wa gwajima nao ni mafyatu tu!!
Unapeleka siasa kanisani,unahubiri siasa kanisani kwa zaidi ya wiki mbili,kiongozi wa dini unakuwa na hasira na mambo ya ajabu ajabu!

Sasa tumechoka!
Alichokozwa lakini,tumuombe tu asamehe,sio siasa anajitetea
 
Mimi kama mkristo, na uelewa wangu mdogo juu ya biblia
Sisi kama binadamu tunapaswa kusamehe 7×70
Na yeyote yule akufanyiae mabaya
Sasa napata shida sana
Ninapoona mtumishi wa Mungu
Anapoendeleza vita na yule anayeamini akumtendea vyema
Kuna haja kwa serikali kuingilia na kuyachunguza haya makanisa na viongozi wake
Baadhi yao wanatia shaka sana
Kama kweli wapo kwa kazi ya Mungu au ni njia ya kujitengenezea kipato
Kupitia watanzania
Ambao kiukweli wengi wao wanaishi katika lindi la matatizo na umaskini mkubwa
Wajanja utumia imani katika kuwaadaa na kuwaibia rasilimali zao ndogo walizonazo
Gwajima yupo kwenye process za kusamehe
 
Back
Top Bottom