Gwajima: Mbele yetu sisi kama CCM kuna hatari, Mungu ataingilia kati ili awatetea watu wake

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,850
Reaction score
6,030
Gwajima ameongea mambo mazito mno, na nashindwa kuendelea kuandika, kwani amesema Mungu ataingialia kati Waminya haki, siku si nyingi, Mbele yetu sisi kama CCM kuna hatari mbele kwa sababu Mungu ataiingilia kati, atajua afanye nini, ili haki itawale

Your browser is not able to display this video.
 
😂😂 Jasusi wa mbinguni anatapatapa
 
Yaani yeye anawasiliana na Mungu kujua nani atakufa lini kwa ajili ya nini,haya na ni nyamaze nisubiri kuona
 
Kumekuchaaaaa!!!
 
Huu utabiri itakuwa wa pili.wa kwanza ni ule wa sheikh ambaye alitabiri kuwa Kuna mwanamama atakuja kuongoza Tz lakini ataongoza vibaya na Kwa muda mfupi tu na kung'atuka Kwa aibu na atapatikana mzalendo ambaye atainyoosha nchi kutokana na uharibifu wa huyo mwanamama
 
Umetia chumvi ndugu...

Hajatamka neno "WATAULIWA" au "MUNGU ATAUA"...

Amesema, mamlaka za kibinadamu zinapoacha kutenda haki, kusikiliza malalamiko na shida za wananchi, MUNGU huingilia kati, kutoa hukumu yake kwa haki...

Hukumu gani ya haki anaweza kuitoa Mungu..?

Bila shaka yaweza hata kuua (kama walivyouwawa wafalme wenye kiburi kadhaa mfano Farao, Sauli, John Pombe Magufuli, Iddi Amini, Mobutu Seseseko, Saddam Hussein, Bashar Al Asad nk)

Aidha yaweza kuwa kupigwa stroke kwa viongozi, kupigwa wazimu, kunyang'anywa madaraka na kutupwa porini na kula nyasi kama mnyama pori kama ilivyotokea kwa mfalme Nebukadneza nk...

Alimalizia kusema, kwa jeuri na kiburi hiki cha serikali hii chini ya CCM, basi haina shaka yoyote kuwa mwisho wa CCM ni mbaya na aibu na tayari umeshafika...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…