Uchaguzi 2020 GWAJIMA: Mgombea wa CCM anayeumiza vichwa vya Wapinzani

Uchaguzi 2020 GWAJIMA: Mgombea wa CCM anayeumiza vichwa vya Wapinzani

kudamademede

Member
Joined
Jan 1, 2020
Posts
62
Reaction score
241
Chama cha Mapinduzi mwaka huu kimepata kazi ya ziada tangu kilipofungua mlango kwa watia nia kuchukua fomu za kuomba nafasi ya kugombea ubunge.

Tangu tarehe 14 mwezi huu ofisi za chama zimekuwa busy kutoa fomu kwa watia nia na wengi wao wamekuwa wakirudisha fomu tayari kwa mchakato wa ndani ya chama kumpata mgombea. Leo zoezi la kurudisha fomu limekamilika na watia nia 165 kati ya 166 waliochukua fomu wamerudisha fomu zao.

Jimbo la Kawe watu wengi wameonekana kulikimbilia na hivyo kufanya idadi ya watia nia kuwa kubwa kufika sasa. Miongoni mwa wengi ni Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ambaye mpaka sasa amerudisha fomu hiyo aliyoichukua siku ya kwanza ya ufunguzi.

Ikumbukwe kuwa jimbo la Kawe limekuwa chini ya himaya ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa miaka 10 sasa. Hii pengine inaweza kuwa moja ya sababu kwanini kuna msululu mrefu wa watia nia katika jimbo hilo.

Kila mtu anasubiri nani atapeperusha bendera ya CCM kumkabili mpinzani wao wa siku zote Halima Mdee wa CHADEMA. Huu bado ni mtihani mkubwa kwa CCM ukizingatia kuwa wengi waliopewa nafasi hiyo wamegwaya.

Upinzani unakabiliwa na ushindani wa aina yake kutoka kwa Askofu Gwajima ambaye tangu ametia nia kumekuwa na mashambulizi ya hapa na pale mitandaoni mengi yakiwa yanalenga kumpunguzia nguvu.

Ni kweli Mdee ameishajua matokeo yake kabla ya kupanda jukwaani kushindana na hoja nzito za Gwajima. Halima ambaye pamoja na kushinda kura za maoni, bado ameweka mguu kwenye nafasi ya viti maalum; pengine Halima ameishajiandaa kutinga bungeni kwa mlango huu akishapokea konde zito la Gwajima. Katika kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi, haikwepeki kwamba upepo wa mzee wa amfifiro unavuma kwa kasi ya ajabu huku watia nia wengi wakitumia njama nyingi kushindana na kiungo huyu mpya aliyeingia kuipa ushindi team ya CCM jimbo la Kawe.

Nini hasa hofu ya upinzani dhidi ya Gwajima? Ukipita kwenye kurasa mbalimbali utaona mashambulizi mengi yakielekezwa kwake. Mtaji alionao Askofu Gwajima ni mkubwa sana na ni faida kubwa kwa CCM. Tunasubiri kwa hamu sana kuona mafuriko ya kampeini kutoka kwa mzee wa kuwakusanya. Mpaka sasa Askofu Gwajima anashikilia rekodi katika kufanya mikutano yenye watu wengi sana.

Huu ni ushauri wangu. Magufuli Askofu Gwajima ni mtaji mkubwa kwenye kampeini zako mwaka huu; anakubalika mpaka nje ya jimbo, muite akuongezee nguvu hasa kwenye maeneo tata hapa nchini.

Abdallah Kiosha Mwinyi
Kunduchi Beach
 
Oh uko Sahihi KABISA Mkuu, Gwajima anapambaa Moto ,Nchi nzima imezizima ,KILA blogs za mtandao Ni Gwajima TU ,Yule jamaa Ni hatari aisee
 
Safi kabisa kwa mwaka huu Gwajima shikamoo endelea kuwachachafyaaaaaaaaa. Gwaji kam ananawaaa .wa upande wa pili wataipata fresh.
 
Kwa kweli kwa kiungo huyu CCM wanamtaji wa kutosha kabisa hakika Jimbo linarudi CCM.
 
Yani hapa Gwajima pale JPM aahh Tanzania Mambo Ni fireeeeeee
 
Ila kwa mwaka huu Gwajima ni kiboko ya siasa Tanzania mzima, tusemage ukweli, imezizima Gwajima ni shidaaaaaa.
 
Humu JF kuna watu wajinga kupitiliza, below zero, eti Gwajima ni mtaji, wa CCM? Hv mnaijua CCM au? Mkome CCM haina njaa ya wanachama au kujitangaza eti huyu mtaji, tena hajawahi kuwa CCM, alikuwa Chadema, sasa hivi ndio anajikomba komba CCM,

Gwajima ni opportunist tu, kwanza ana kashfa kwenye ile list ya wauza unga ya Makonda, asijifanye ni mwema, wamedhibitiwa no drugs, wamekaukiwa sasa wanaona ubunge ndio dili,

askofu fake kazi kukimbizana na siasa.. Ana kashfa kibao za ngono pia, hafai huyo. Labda anajiona msukuma anajiona Mwenyekiti atampitisha, hilo asahau, tena Mh. Mwenyekiti wetu hana hayo mawazo hata kidogo. Katika list number one ya watu fake, huyu namweka no. 1
 
Huyu jamaa ni mtu mmoja mwenye ushawishi mkubwa hapa Tanzania.

Uwezo wake wa kupanga hoja na kupangua mashambulizi ni wa kiwango cha juu.

Ni asset kubwa katika nchi hii
 
Back
Top Bottom