Gwajima ni mtu makini sana Hilo halina ubishi.
CCM Kwa kweli isipoangalia itaingia kwenye siasa rasmi 2025.
CCM kikiwa Chama Cha kisiasa kama kilivyosajiliwa ni wazi kuwa kiraungama na vyama vingine vya siasa kwenye kampeni za Urais 2025.
CCM kukubali TU kuwa Sasa hakuna haja za kulinda Neno CCM huku nchi ikiwa inaangamizwa na wale wanaojifanya kuwa ni wamilimi wa Neno au Jina Hilo CCM .
Najiuliza hivi CCM ikisambaratika au ikifa Kada Fulani atakufa, au KJ atakufa Kwa sababu CCM imekufa, au Wanachama wake watakufa au nchi ya Tanzania itaondoka kwenye Ramani ya Dunia?
Jibu ni hapana ,CCM ni chama kama kilivyo chama kingine chochote.
Nilikua nataka kusema kuwa, Wale wanaCCM na hata wapinzani na waumini wa dini zote nchini ambao Kwa nafsi zao na Kwa dhati kabisa waliwahi kusimama hadharani na kumsifu Magufuli Kwa mambo aliyoyafanya na Kwa jinsi alivyowakemea wezi na kuwaondoa kwenye nafasi za uongozi wale walofisidi fedha za umma basi 2025 wajitokeze wazi kabisa Kupinga kundi la walamba asali kuendelea kushika uongozi kwenye nchi hii. Wasimame kidedea bila kupepesa macho watuletee watu wenye uwezo wa kukemea Wahalifu na kuwafukuza wezi kwenze ofisi za umma .
Itakua ni unafiki mkubwa wanaCCM wengi ambao Leo kama sio JPM wasingerudi Bungeni Wala kwenze udiwani Wala kwenye serikali za mitaa kukubali kakundi ka watu wachache watumie fedha kumchagua JPM na uadilifu wake na uzalendo wake.
Kukaa kimya JPM atukamwe na kuitwa mwizi ni kuliua Taifa hili na kujenga Taifa la hovyo kabisa Duniani.
Leo hii hakuna mtu anayeweza Tena kuwa muadilifu popote Kila anapotafakari kuwa kama JPM akiyejitoa mhanga kwa ajili ya N chi hii anakashifiwa na kikundi Cha watu wachache waliokalia fedha za umma na kuzichezea wanavyotaka huku wakiwagawia pesa wapinzani ili nao watumie muda Mwingi kumtukana na kukejeli kazi alizozifanya Hayati JPM.
Haiwezekani kuwa na Taifa linaloenzi wizi na kuwadharau mashujaa wake Kwa sababu TU Kuna kikundi Cha watu kimeamua kutumia Chama Cha Mapinduzi kumiliki hii nchi . Hapana.
Kama Kuna sijui Sukuma Gang ,sijui Gwajima Gang , sijui Wamachinga , Sijui wajasiriamali wadogo, sijui madereva bodaboda, sijui ,wanyonge wote na wale wote wanaopinga vitendo vichafu vya ushoga Kwa dhati kabisa , wachukia ufisadi wote ni vyema kabisa waungane waichachafye CCM bila kujali kuwa itaanguka au itasambaratika lakini walimusuru Taifa hili na kesho ya vizazi vyetu.
CCM hii na serikali yake ni hatari kubwa sana Kwa Taifa hili.
Gwajima anajitahidi kuihubiri Injili ili anagalu watawala na Wananchi waamke na kusimama katika Haki na uadilifu na kutenda mema Kwa ajili za wanyonge.
Tumuombe Rais Mh. Samia alinusuru Taifa hili Kwa kujitenga na siasa chafu za kutumia nguvu kubwa ya fedha na Dola kuilinda CCM na urais wake.
Mungu alikomfikisha ni pakubwa sana . Makamu wa Rais miaka Mitano, Rais miaka minne ni heshima kuwana sana na jambo kubwa sana Mwenyezi Mungu alilomjalia. Wala asitumie hila yoyote kukufuru na kuharibu heshima kuwa aliyotunukiwa na Mwenyezi Mungu katika nafasi za juu kabisa katika Taifa hili.
Mungu akikujalia kuwa juu kabisa hata Kwa Mwaka mmoja basi ni jambo la kushukuru sana na heshima kubwa.
Watanzania tunaimani kubwa sana na Uadilifu na Uzalendo wa Mh. Mpina, Mh.Msukuma , Polepole, Kabudi, Lukuvi, Kishimba, Lisu, John Mnyika, Heche, Msigwa, Lema, Dr.Slaa , Wakili Kibatara ,Wakili Madereka, Mtaka, Majaliwa Kasimu , Mkuu wa Majeshi mstaafu Mabeyo,Gwajima ,Rais Hussein Mwinyi na Philip Mpango, Warioba, Makongoro Nyerere , Joseph Sokoine . Hatuna mashaka na uadilifu wao kabisa.